Maboresho ya JF - 2019

Maboresho ya JF - 2019

Leo ujiite Daudi de classic na kesho ujiite “Daudi de Classy” na keshokutwa ujiite “Mtambaa Panya” wiki mbili baadae ujiite “Mrembo wa Kigogo” mwezi mmoja baadae ujiite “Nyongo Mkalia Ini” baada ya miezi 2 ujiita “Mkapa Mpya” miezi 3 baadae ujiite “Cha Upele” etc?

Hapana, kwa JF tunajaribu kudhibiti hili!
Ha ha, alafu mkuu mbona huwa huonekani onekani humu??, huwa tunakuona kwa dharura tu kama hvi. Jichanganye na sisi bhanaaaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Khantwe sasa huo ni utoto. Ucomment halafu ujipe like? Hapa wanasema ni Great thinkers not kids corner. Usinitupie madongo.
Dah...raha jipe mwenyewe bana

Sent using Beretta ARX 160
 
Fanya maboresho unapokuwa Facebook, Twitter, au Instagram ukifuata links zilizopo zielekee kwenye jamiiforums app na sio browser. Itapendeza sana. Maana hapo huhitaji ku log in kwenye browser bali app pekee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fanya maboresho unapokuwa Facebook, Twitter, au Instagram ukifuata links zilizopo zielekee kwenye jamiiforums app na sio browser. Itapendeza sana. Maana hapo huhitaji ku log in kwenye browser bali app pekee

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo ni nje ya uwezo wetu. Mara ya kwanza ulipotembelea links hizo uliulizwa unataka ziwe zinafunguka kwa App au kwa Browser? Ukachagua browser!

Kama unatumia Android, hii inaweza kuwa msaada:

Open links in corresponding app instead of browser
 
Hii comment nimecheka hahahahahahaha
Leo ujiite Daudi de classic na kesho ujiite “Daudi de Classy” na keshokutwa ujiite “Mtambaa Panya” wiki mbili baadae ujiite “Mrembo wa Kigogo” mwezi mmoja baadae ujiite “Nyongo Mkalia Ini” baada ya miezi 2 ujiita “Mkapa Mpya” miezi 3 baadae ujiite “Cha Upele” etc?

Hapana, kwa JF tunajaribu kudhibiti hili!
 
Maboresho mnayofanya nahisi ingekuwa faida kubwa sana kwa JF na kiasi kwa watumiaji ambao wangetaka kutumia JF kama sehemu ya kupata takwimu za kijamii, kisayansi na kibiashara endapo munge tengeneza JF API.

Hii itaikuza sana JF kama biashara kubwa mfano wa facebook. Kwa mfano inaweza kutumika kama njia ya ku subscribe/sign-up service zingine kupitia JF account.

Labda hapa wasiwasi wa madhara hasi yanaweza kuwa jinsi ya kuimarisha usalama au usiri wa utambulisho wa mteja.

Facebook ipo hai na imekuzwa sana baada ya kuwa na API.
Twitter na wengine wa jamii ya JF karibu wote wana API.

Pia hii inaweza kuongeza kipato chenu kwa baadhi ya service flani kutumiwa na wengine kibiashara kupitia API yenu.

KEY:
API :- Application Programming Interface.

CC: Maxence Melo
 
Tuna karibia siku za chaguzi.... bado nakumbuka namna JF ilivyoshambuliwa wakati wa siku za chaguzi mihula iliyopita! Kwenye hizo infrastructure mnazokusudia... hakikisha mnaweka "mi-algorithm " ya kutisha... kiasi kwamba atakaye jaribu kuichezea... mashine iliyotuma komandi iungue zaidi ya vi'solola' vya maharage ya Mbeya.
===
Nakutakieni kila la heri kwenye maboresho hayo.
 
Hongera 👏 Mexence 🙌

Naomba haya endapo ukipata uwezo wa kuyatenda.
_ UI kwa app na web iweze kuwa sparkling theme. Maana hii Blue (Sky blue) inaumiza kwa web. UX ifanye balanced upunguze size kwa app iwe smooth na more attractive.
_ Jukwa la Sanaa. Ndio Art 😉 ilikuwezesha mjumuiko wa vitu hivo kupatikana humo (sculptures, paintings, merch design, calligraphic works, illustrations, digital arts...).
_ Social Media links kupitia kwa profile/account details kama ilivyo lakini kwa sasa ongeza Instagram, Bēhance, Dribbble, Vimeo, YouTube, Medium ... maana kwa sasa Facebook na Twitter.
_ Jukwa la Diplomatic maana wengi masuala ya Diplomasia wanayahusisha na siasa ilhali ni vitu tofauti.
_ Verification tick ifanye improvement kuwa badge and more attractive even easier to see.
_ Ruhusu ars./naming prons. (ÔÉĆ) wakati wa kusajiri/kufungua account. Pia members apatiwe username eg. www.jamiiforums.com/user/sajorsergiosjanic
_ Usisahau kuondoa Google+ 😀

Serge 😉
 
Wakuu,

Naomba kuwafahamisha kuwa siku si nyingi tutafanya maboresho kidogo kwenye mwonekano na matumizi ya JF.

Lengo ni kuzingatia mahitaji ya wadau (ambayo yamekuwa yakiombwa), kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia na kuimarisha zaidi uimara wa platform.

Aidha, maboresho hayo yataenda hadi kwenye kuimarisha miundombinu (infrastructure) ili kuongeza uimara wa kukabiliana na hali yoyote.

Mabadiliko mengine ya aina hii yanaweza kufanyika 2021 au 2022.

Asante kwa ushirikiano mnaoendelea kutupa.
Tuko pamoja Mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MKUU Maxence Melo post ni ndefu lakini soma yote tafadhari

Muendelezo wa API ...
==========<<<<<>>>>>>=========
Mifano ya matumizi ya API ya JF
ni kama nikitaka kukusanya (query) michango threads na/au posts zinazo husu mada flani toka kwa user flani au wote au za kwangu kwa interval ya muda na tarehe flani n.k.

JF inaweza kutumika kama data source ya tafiti za kijamii, kisayansi, na kibiashara.

Mfano kampuni flani inaweza kuwa na project ya kutengeneza product ya deep learning na AI ikatumia baadhi ya data kutoka JF kwa kuilipa JF kiasi flani au kuwa acknowledge JF na kuvutia watu wengi zaidi nje ya Tanzania na kuifanya advertising network kubwa mkapiga pesa ndefu ya matangazo.

Tanzania kampuni chache sana wanafaidika na matumizi ya Business Intelligence (BI) lakini miaka michache sana karibu kila kampuni makini ya biashara na taasisi za kisiasa na serikali hapa Tanzania na duniani kote watalazimika kutumia hii teknolojia ya BI kwa ajili ya kufanya strategic decision. Hata sasa tayari makampuni makubwa ya simu hapa ndani (TZ) yana hangaika kuimarisha Datawarehouse zao kwa ajili ya BI.

Siasa: wanasiasa duniani kote wana hangaika na data za kijamii kama za JF na Facebook au Twitter ili kuweza kufanya kampeni mitandaoni za kuwabadili mawazo wapiga kura wao wakilenga makundi ya kijamii kiumri na kijiografia. Mfano hii kashifa ya FB kutoa data kwa kampuni flani zilizo tumika ktk kampeni za uchaguzi USA. Hapa Tanzania JF ina nguvu sana ktk siasa na watu hutoa maoni huru guvyo inaweza kutumika ktk tafiti za kampeni.

Ni rahisi sana kutambua mawazo au mahitaji ya vijana kupitia michango yao au vitu wanavyo share kupitia thread hata zile 'tunazoita za kijinga' za chit chat au MMU. Huku utaona mahitaji ya vijana na matatizo yao kama unataka kuanzisha kiwanda cha bidhaa za wakubwa chumbani n.k.

Kama unaifanya forum flani ya JF kuweza kuunganishwa na device au application zingine za watu binafsi kupitia JF API na kutumika na application na home device kama vile mfano wa Alexa inavyokusanya data Amazon au Apple Siri inavyokusanya sehemu nyingine kwa kulipia huduma basi JF inaweza kujiongezea kipato kwa kutoza watumiaji wa huduma yaani subscribers. Humu kuna taarifa nyingi sana za matukio na biashara kama kule kwe burudani, JF doctor, JF matangazo madogo madogo ya biashara, Breaking news n.k.

Mfano hapo kwenye breaking news kampuni za media zinaweza kujiunga kupitia API kama sehemu ya kupata news tip kisha kuwatuma waandishi wao walio karibu na tukio. Sasa hapa atakae ingia JF website kawaida na wa mobile app yenu inakuwa bure kabisa kama ilivyo hivi sasa lakini hawa watakao tumia API yenu wanalipia wanapo nunua API key iwe wana renew service kwa kila baada ya muda flani.
Sababu hawa wanapata huduma maalumu kibiashara kwa upendeleo. Na sisi wa kawaida tunatumika kuwafaidisha ninyi JF kwenye JF kutumika kama advertising network hivyo hatulipii kama ilivyo sasa.

Hawa nasema huduma maalum ya upendeleo sababu hivi sasa inawezekana kabisa mtu anaefuatilia kitu flani JF kikampita bila kusoma au akakiona siku kadhaa zimepita. Na notification zinaweza kuwa nyingi sana ni rahisi kuziondoa bila kupitia zote lakini kwenye API zinakuwa filtered kupata specific subject au keywords flani na muda flani kutokana na mtakavyo implement API na mtumiaji atakavyo chagua features wakati anafanya configurations. Hii sijui niifananishe na Microsoft Azure Events Handler au Azure Events Hub.

Unaweza kuona hii idea ni bado sana kufanya kazi kwa bongo lakini ifanyeni kama vile mtu anavyonunua kiwanja/shamba kisha miaka michache anasifiwa aliona mbali sana, alifanya investment kubwa kwa gharama ndogo sababu alikuwa ahead of time.

Kuna siku utakuja kuombwa structured data za mambo flani na taasisi kubwa za kimataifa kama za UN au google kwa malipo flani ndipo JF mtakumbuka huu ushauri wangu. Pengine hadi sasa tayari mmeshaombwa data.

Mniwie radhi kwa makosa (typos) mengi ya kuandika sababu ya keypad na screen ndogo ya simu, pia mtiririko mbaya wa hoja lakini nafikiri nimeeleweka.
 
Back
Top Bottom