SoC04 Maboresho ya Dawati la Jinsia ndani ya Idara ya Polisi, litaongeza Usalama kwa Watanzania

Tanzania Tuitakayo competition threads

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,141
4,309
Dawati la Jinsia ni kitengo kinachopambana na Ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto kilichopo ndani ya Idara ya Polisi Tanzania na kitengo hiki hupatikana katika vituo vingi vya polis hapa nchini.
Dawati hili mbali na kushughulika na kesi za Ukatili, lakini pia kimekuwa kikitumika kwa ajili ya kutoa elimu kwa jamii juu ya ukatili wa kijinsia.

Ktika viteo vya polisi, kitengo hiki kimekuwa kikihudumiwa na Askari ambao wamekuwa waivali kiraia ili kuongeza ukatribu kati yao na raia wanaoenda polisi kwa lengo la kureport kesi za ukatili wa kijinsia au ukatili dhidi ya Watoto.

Tofauti na vitengo vingine ndani ya jeshi la polisi,kitengo hiki kimekuwa kikijitenga kidogo na kuwa umbali fulani kutoka eneo kuu la polisi, na dawati hili limewekwa hivyo kwa sababu ya kupunguza uoga kwa watu pindi wapelekapo kesi za ukatili wa kijinsia.

Maafisa wengi kutoka katika dawati hili wamekuwa wakitoa huduma nzuri ya kushughulikia wahanga wa ukatili .lakini licha ya huduma nzuri na njia nzuri ambazo askari wa dawati hili wamekuwa wakitumia wakati wa kuzungumza na muhanga wa ukatili, changamoto kubwa inayokumba kituo hiki ni kukosekana aina ya Wapelelezi wanaojitegemea.

Wapelelezi wanaoshughulikia na kesi hizi ni wapelelezi wa kawaida ambao wanatoka katika katika idara ya kawaida ya polisi, hali ambayo inapelekea wakati mwingine kuwepo kwa longolongo na zungusha zungusha nyingine.

Ili kuongeza ufanisi na utendaji kazi mzuri, ni bora sasa serikali ya jamhuri ya Muunagno wa Tanzania, kukipa mamlaka kitengo hiki ili kiweze kujitegemea chenyewe hadi katika upelelezi , na maafisa upelelezi wa dawati la jinsia wabaki kushughulika na kesi za ukatili peke yake.

Hiyo itasaidia wapelelezi kutokuwa na mzigo wa kesi nyingi tofauti tofauti.
Kwani kwa sasa unaweza kukuta askari anaepeleleza kesi ya ukatili ndo huyo huyo ana mafaili ya kesi ya wizi, hivyo askari huyo kutokuwa na ubobezi zaidi katika kushughulika na ishu za ukatili
Lakini pia,uwepo wa wapelelezi wanaojitegemea utaongeza uzoefu mzuri kwa askari hao.
Na pia wapelelezi hao wapewe mafunzo zaidi kama wanavyopata maafisa wa Dawati la jinsia ili waweze kuwa na uwajibikaji zaidi pindi wanapomuhoji muhanga au mtuhumiwa waukatili wa kijinsia.

Pia katika kufanyia maboresho ya idara hii, serikali iweke mfumo wa kidigital kwa kila kituo ili iweze kusaidia kupatikana kwa urahisi kwa mafaili yote yanayohusu kesi za ukatili wa kijinsia.kwani kuna wakati mtu binafsi anataka kufuatilia kesi lakini anapokwenda kituoni anakutana na tarifa ya kutokuonekana kwa faili la kesi fulani ya ukatili.
Mfumo wa kidigital utasaidia pia kurahisisha mawasiliano kati ya Idara hiyo ya Kupambana na ukatili wa kijinsia.

Pia katika kufanya maboresho ya idara hii, serikali itakuwa imefanya jambo la muhimu kama litaipa meno idara hii kwa kuwahusisha maafisa usalama wa taifa,jeshi la Wananchi kuwa sehemu ya kikosi maalumu cha kupambana na ukatili wa kijinsia katika nchi yetu.

Maafisa usalama watumike kufuatilia kwa siri kuhusu zozote za ukatili zilizorepotiwa na ambazo kwa sababu mbalimbali zimekuwa zikifichwa bila ya kuwekwa wazikutokana na sababu mbalimbali ikiwemo rushwa na vyeo vya watu,kwani imeonekana mara kadhaa watu fulani wakishinda kesi hizi kwa sababu tu ya vyeo walivyo navyo.

Kwa sababu ukatili umekuwa ukipoteza maisha ya watu wengi sana,uwepo wa maafisa usalama na Jeshi la Wananchi utasaidia kuongeza nguvu kubwa ambayo itafanya ukamataji kuwa wa kiwango cha juu zaidi hasa kwa wale wanaofanya matukio ya ukatili wa kijinsia.

Katika kuweka maboresho zaidi katika idara hii ya dawati la jinsia, jeshi la polisi linaweza kutengeneza Maafisa polis ambao watakuwa ni wataalamu wa afya ya Akili ambao watakuwa wakitoa msaada wa kisaikolojia kwa wahanga wa waliofanyiwa ukatili wa kijinsia

Kwa sababu moja ya madhara makubwa ambayo yanaweza kumpata mtu nikuathirika kisaikolojia pindi anapokufanyiwa ukatili wa kijinsia,hali ambayo imepelekea watu wengine kujiua kutokana n aina fulani ya ukatili waliofanyiwa.

Kuwepo kwa maafisa TAKUKURU watakaofanya kazi moja kwa moja na idara hii itasaidia pia kupunguza mianya ya Rushwa katika idara hii kwani baadhi ya watu wamekuwa wakikosa haki yao kutokana na kuwepo kwa rushwa ambazo zinapelekea aliefanyiwa ukatili kubaki na maumivu makubwa katika moyo wake.
Katika kuongeza mapambano zaidi, serikali inaweza kuja na muongozo maalumu ambao utatumika kuwaongoza watanzania na kujua namna gani ya kufuatili kesi hizi, na kesi hizi zifanywe kuwa ni haki ya mtu yeyote kuifuatilia na kutaka kujua kinachoendelea bila ya kuwepo changamoto zozote.

Mwisho kabisa, serikali itenge bajeti ya kutosha kwa dawati la jinsia kuwa na vipindi vya kutoa elimu ya Ukatili kwa watanzania.
Elimu ambayo inaweza kutolewa kupitia vyombo vya habari mikusanyiko ya watu,misikitini,makanisani,masokoni na sehemu nyingine zile.
 
Katika kuweka maboresho zaidi katika idara hii ya dawati la jinsia, jeshi la polisi linaweza kutengeneza Maafisa polis ambao watakuwa ni wataalamu wa afya ya Akili ambao watakuwa wakitoa msaada wa kisaikolojia kwa wahanga wa waliofanyiwa ukatili wa kijinsia
Hao maaskari wanaweza labda kupatiwa zile ABC tu lakini suala la afya ya akili wahanga wapewe rufaa kuwaona wataalamu husika.

Kitu kizuri sio kuwa na mtu mmoja anafanya kazi nyingi, bali kuziunganisha 'orchestrate' kazi zote na idara zote za serikali zifanye kazi kiumoja kama kiumbe mmoja

Kuwepo kwa maafisa TAKUKURU watakaofanya kazi moja kwa moja na idara hii itasaidia pia kupunguza mianya ya Rushwa
Uwajibikaji wa taasisi na uwajibishwaji wa wakatili vikiendana na

na kesi hizi zifanywe kuwa ni haki ya mtu yeyote kuifuatilia na kutaka kujua kinachoendelea bila ya kuwepo changamoto zozote.
Uwazi, wenye kizingatia taratibu za kimahakama na faragha

Vitasaidia sana.

Na kama ulivyoelezea kwamba kitengo kifanye kazi yake na nimeongezea tu kwamba kama bado hatujaweza kuwapata watu mahsusibkwa kitengo pekee basi hata kutumia mifumo iliyopo ya utoaji huduma haki, upelelezi na ushauri nasaha itumike ipasavyo. Ahsante
 
Back
Top Bottom