Mabomu ya Machozi yatumika kuwasambazi wananchi pamoja na Wanafunzi Mjini Dodoma

Hiyo ni dalili mbaya,inapaswa kupingwa na wote wenye mapenzi mema. Huwezi kuzuia umma ambao ndo hasa wanaolengwa na muswada huo!
 
Nasikia milipuko ya mabomu huko bungeni na risasi kibao zinapigwa sijui kinachoendelea
 
Nasikia mabomu yanapigwa huko getini , sina hamu. Waloandaa walikosea kuweka ukumbi mdogo may be wali undermine watu. Na la pili hao wanafunzi wakati mwingine wanatakiwa kuelewa kama ukumbi hautoshi wangeondoka wasubiri muda mwingine, mchakato ndo unaanza, wao kila kitu fujo tu, wanapenda sana vurugu.

wanapenda amani na haki mama. tatizo ni serikali imeshindwa kujipanga na kuwa na nia ya kutoa haki kwa makundi ya wananchi kushiriki. Serikali ilidhani madai ya katiba mpya ni ya viongozi wa vyama vya upinzani. Serikali ilidhani kwa kuwa wananchi hawana access na vyombo vya habari kujieleza kama serikali inavyolazimisha vipindi maalumu kwenye tv basi wananchi hawataki katiba mpya. Serikali ilidhani wananchi hawataelewa maudhui ya mswada huu wa kutunga katiba mpya na hivyo kwamba inaweza kuwaburuza kama ilivyozoea.

Serikali kama ilikuwa na nia njema ya kutoa haki kwa makundi yote ya wananchi kutoa maoni yao kuhusu huu mswada wa kutunga katiba mpya, ilitakiwa ijipange kutoa fursa hizo kwa kila kundi kwa kutumia utaratibu na kuwawezesha.

Vurugu zinazoendelea Dodoma sasa hivi ni matokeo ya Serikali kukusudia kunyima wananchi fursa ya kushiriki na kusikilizwa kikamilifu. Wanafanya mambo kwa kutegea tegea, hadi wakiona hali inabadilika wanazidiwa ndipo wanabadilisha utaratibu.

Kwanza walipanga kufanya public hearing dodoma peke yake mara moja tu. Malalamiko yalipotokea wakasema na Dar na Zanzibar. Leo watu wamekuwa wengi Dodoma sasa wanasema maoni yatakusanywa kwa vikao viwili leo na kuendelea hadi siku tatu. Hata hizi hazitoshi

Yaani ni kama kusema huko serikali hakuna hata mtu mmoja anayeweza kufikiri na mwenye nia njema na wananchi!!
 
Tuwapongeze hata hao wana harakati walioitikia mwito kwa wingi na kuonyesha nini matamanio ya walio wengi maana bila wao FFU wasingesaidia kupaza hizi sauti kwaku kuza hili tukio. Hapo sasa wajitathmini kwa muda mfupi uliotumika kutoa hilo tangazo bado mwitikio ni mkubwa kiasi hicho je sasa baada ya hapa hiyo information ita flow kwa rate ipi na kwa tafsiri ipi hasa baada ya watu kupigwa mabomu? Tayari wamejifunga goli bila kujua. Sasa ndiyo watashuhudia jinsi watanzania wasivyotaka masihara na kuwa hawachukulii vitu for granted.
 
This is too much for ccm and Dr JM kikwete to handle... Nothing is ever perfect with these people ...why whyy!!

They dont ave even a bit, of objectivity ..to organise this kind of things with diginity and respect for all peolple to attend!!

What do they xpect us to think of them...????
 
polisi wametumia mabomu kutawanya wanaharakati dakika chache zilizopita. Kwa mara nyingine tena serikali inakandamiza haki za raia!
Sio kweli Muhosin, Ukumbi hautoshi wangekaa wapi? na bunge ni sehemu ya kuheshimiwa wao wana mabango wanawaza vurugu tu, katika hili natetea kwasababu nashuhudia, ukumbi ni mdogo, kosa labda ni kuchagua ukumbi that all.
 
Kwani Bunge hawakujua kuwa hapo ni mahali pa dogo na je public hearing unaitafsiri vipi hayo mabango si ndiyo sauti zenyewe ama ulitaka waongeeje wote wanaweza ongea hata kama kutakuwa na kupewa nafasi? Acha ushabiki wewe watu tuko serious we unaleta diplomacy pasipo mahala pake?
 
haya sasa! kumekucha, FFU wamewasha risasi za mpira na kuanza kufurusha watu toka kwenye geti la bunge.....

wanasafisha njia yote, vijana na wanaharakati wamevuka na kuingia upande wa pili wa barabara, askari wanaranda randa.

it has been an embarasment kwa umma kwani mh godbless lema aliitwa aje azungumze na vijana. akapewa pendekezo kuwa chimwaga hall itumike, vijana wametaka jamhuri stadium instead...

vijana wametaka waliomo ndani wasitishe zoezi na lifanyike upya mara moja hapo jamhuri stadium....

vijana na wanaharakati wana sababu ya msingi.....

1. wakina mama waliopewa dozi na mama kombani washaingia ukumbini

2. watu wanaingia kwa kuwa identified.....eg viongozi wa ccm

3. mbunge wa dodoma mjini mheshimiwa malole mapema asubuhi alileta champion mbili zilizojaa wanafunzi wa shule yake ya city kuja kuunga mkono muswaada. (ikumbukwe kuwa mheshimiwa malole aliwatumia hawa hawa wanafunzi kushinda kura za maoni na kuteuliwa kuwa mbunge)

4. vijana na wanaharakati wamefika tangu saa moja asubuhi na kuambiwa kuwa ukumbi umejaa....

ntaendelea kuwajuza!
 
Hizi tv za tz bomu kweli kweli. Wamejazana hapa na makamera yao muda mrefu lakini hakuna live coverage. Hata Star tv ambao wanatangaza live kutoka Dodoma hawaoneshi yanayojiri ukumbi wa bunge ambayo ni historia kubwa sana. Wananchi wameamua kufanya public hearing yao nje ya bunge barabarani baada ya kuzuiwa kuingia ndani

hapo ndipo kunapotokea mgongano na uhuru wa vyombo vya habari na mwananchi mwenye akili timamu anayejua haki yake ya msingi ya kujua habari, unaweza kuamini mpaka sasa mabomu ya machozi ya rushwa mawili kwa ajili ya kusambaratisha wananchi ambao direct wanahitaji kuchangia mawazo muhimu juu ya katiba.
 
Kundi kubwa na Askari wa FFU limetumika kuwatawanya wanafunzi pamoja na wanafunzi walikuwa wakitaka kuingia ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma kwa ajili ya kutoa maoni ya mswada wa tume ya raisi ya kuchukua maoni yake. Kundi kubwa la wanafunzi wao wengi wao walikuwa toka katika Chuo cha UDOM hivyo kufanya eneo nzima la bunge kuleta taharuki kubwa.. Wanafunzi walikuwa wanadai kuwa wengi wamekataliwa kuingia ndani na kutoa maoni ya tume. Hivyo askari waliamua na kuanza kuwatawanya wanafunzi kwa mabomu mpaka katika maeneo ya stendi kubwa.
 
Hatutaki kuanzishwa tume bali kwamba kuanzishwe Baraza la Taifa kuratibu mchakato wa kuundwa kwa katiba mpya. Hivyo ni hiyo baraza ndio itakayounda Tume ya kukusanya maoni na kurudisha kwa baraa la taifa na wala si Kikwete in the picture!!!!!!!!1

Sasa kama ukumbi hautoshi,mnataka watu waruhusiwe kuingia ili wakakae wapi?

Public hearing hii inafanyika kwa siku 3 mfululizo,sio lazima kila mtu aingia leo...waweke utaratibu wa wale waliojiandikisha kutoa maoni yao juu ya muswada ndio waingie ndani kwa zamu kulingana na uwezo wa ukumbi kubeba watu. Wakimaliza watoke na kuwapisha wengine wenye maoni yao. Wengi wa waliojazana pale ni mashabiki na washangiliaji-wale hawana haja ya kuwemo ndani,wanaweza kufuatilia proceedings hizo kwa kutumia PA system nje ya ukumbi na kwenye vyombo vya habari-radio ONE wanarusha live.

Kwa wale walioamua kuendesha public hearing yao nje,ni counter-productive kwasababu maoni yao hayatafika yanapotakiwa kufikishwa...sana sana wanapoteza muda wao.

By the way,mjadala wa leo ni kuhusu Muswada wa kuanzisha tume ya Katiba, na sio kujadili Katiba yenyewe...hivyo inputs/ideas/critique inatakiwa ku focus kwenye vifungu vilivyo ndani ya Muswada wenyewe.
Baada ya kusema haya mimi nina wazo moja japo kwa mchakato unaoendelea sasa linaweza kuwa limepitwa na wakati. Kwa nini zisiwepo mechanism nyinginezo za kukusanya maoni juu ya muswada husika kama vile wananchi kuruhusiwa kutoa maoni yao kwa njia ya barua, e-mail,social network platforms etc

Kwa kuruhusu hizo njia nyingine,hata watu wasioweza kufika Dar,Dodoma au Zanzibar physically wataweza kutumia haki yao ya kutoa maoni pasipo kulazimika kuwepo kwenye maeneo yanapofanyika shughuli hiyo
 
it has been a sewrious embarrasment kualikwa kwa mbwembwe kujadili muswada halafu kuchapwa mabomu! actually my clothes are now muddy!
 
Kweli Tanzania ina kazi kubwa sana na hasa katika kuleta ustawi wa watu na jamii yake katika kutoa maoni yao
 
hasira zimenijaa hapa yani basi tu...... walitakiwa hii kitu ipelekwe tz nzima ingeanzia ngazi ya wilaya watu wakajadili huko...sasa hii ni ubabaishaji wa hali ya juu....watu wanajitokeza bado wanapigwa mabomu
 
Sihitajii kufkiria vsivyofikirika kwa sasa... hata ingesemwa unafanyikia uwanja wa Taifa pasingetosha bado lawama zingeliendelea...
WATANZANIA HATUNA MIPANGO! SI SERIKALI WALA SISI WENYEWE TUPOTUPO TU!

Hatujipangi ili tufanye jambo TUNAKURUPUKA tu na HAYA NDIO MATOKEO YAKE... hajumjui adui yetu mpaka leo!!!
 
Vyombo vya habari ovyoooõo kabisa. Kazi kufuatilia gossips na siyo mambo ya maana.
 
wana mawazo finyu sana hawa wao walidhani kuwa watakuja watu wachache na kuwa huo ukumbi unatosha.....ni upuuzi wa hali ya juu kabisa.......mimi na wanakijiji wenzangu huku usokami nasi tunataka kutoa maoni........kuchukua mikoa miwili bara na mikoa mingine kuwakilishwa na mikoa miwili na dharau sana
 
wanashindwa kutofautisha Tanzania ya ndio mzee na siyo mzee hapa kazi ipo.
 
Back
Top Bottom