Mabomu Arusha: Makachero wayafichua mapya

Mabomu Arusha: Makachero wayafichua mapya

Mulongo si mtu makini hata kidogo na kesha poteza credibility siku nyingi na kila asemacho yeye ni kuisaidia CCM
 
Makachero from China?
Huo uchunguzi nao utakuwa ni wa kichina china tu. Hakieleweki kitu hadi serikali iunde Judicial Commission huku ikiwa na mandate maalum na si huu mchezo wa kichina.
 
Kama tatizo ni CDM waipe Arusha yote itawale, kupanga na kusimamia shughuli za maendeleo kisha baada ya miaka 10 wawatathmini kama wameweza au la. Barabara, shule bure, afya bure, wasimamie madini na mlima Meru, baadhi ya mbuga za wanyama, pamoja na rasilimali zote; kisha wananchi waamue kuendelea na CDM au kurudi kundini. Hii itakuwa pilot kwa CDM kwa kuwa hata tukijiuliza katika majimbo ambayo CDM imechukua, je kumeonekana hata fununu za maendeleo? Ajira, kipato kwa wananchi wake nk?
 
Polepole tutafika.

Hizi longo longo zote tunazozisoma hapa JF za baadhi ya watu kusema wanawafahamu













waliosababisha haya maafa ya kinyama Arusha lakini wakiambiwa na wapenda AMANI wawataje kwa majina au kuonyesha tu sura zao na ushahidi, lakini wanashindwa kufanya hivyo.

Hii ni sawasawa na genge la wizi ambao wakiiba wanaanza kupiga kelele na kumnyoshea vidole yule waliyemwibia huku wakipiga kelele na kusema mwizi, mwizi, mwizi ili wasijulikane katika macho ya sheria kama wao ndiyo wezi.

They can't fight TRUTH with LIE.
Mkuu maneno yako ulioangika kwa kizungu ya mwisho kabisa ndilo jibu linalokufaa usiku mwema na presha yako.
 
Mbona Hakuna jipya inaonekana dhahiri kinachoendelea ni propaganda za kisiasa!.

Watuhumiwa ndio wanaochunguza, nchi hii!

Hawa watu watatupeleka pabaya!
 
*Wataalamu kutoka China watua kuchunguza

*P
olisi watamba kufichua siri ya milipuko yote

TAARIFA za awali kutoka kwa makachero wa Jeshi la Polisi nchini zimefanikiwa kubaini mtandao wa ulipuaji mabomu katika jiji la Arusha, imefahamika. Mpaka sasa taarifa zinadai mtandao uliohusika na milipuko miwili iliyotokea kwa nyakati tofauti jijini hapa ulipangwa ndani ya jiji la Arusha.

Mlipuko wa kwanza ulitokea katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Olasiti, Mei 5, mwaka huu na kuua watu watatu, wakati mlipuko wa pili ulitokea Uwanja wa Soweto Juni 15, mwaka huu na kuua watu wanne, huku majeruhi wa matukio yote wakifikia zaidi ya 100.

Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Arusha (RCC) jana jijini hapa, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, alisema mbinu hizo zimejulikana kutokana na wananchi waliojitokeza kuwasilisha ushahidi kwa vyombo vya dola.

Alisema mpaka sasa ushahidi unaonyesha kuwa mtandao wa waliolipua wa mabomu hayo ulianzia jijini Arusha, na kikubwa kabisa wanawashukuru wakazi wa Arusha waliokuwa wakifika kutoa ushahidi wa wahusika.

“Ukweli wa mambo haya utajulikana hivi karibuni na Serikali itamchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kuhusika na mtandao huo, bila kujali wadhifa wake. Mambo haya yamedhalilisha na kufedhehesha Taifa,” alisema Mulongo.

Akiwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, aliendelea kubainisha kuwa upelelezi wa matuko hayo mawili unaendelea kwa umakini mkubwa na kikubwa kinachoangaliwa ni kuepuka kukamata watu wasiohusika.

“Tunachukua umakini ili waliofanya hivi vitendo vya kinyama wasiendelee kutamba, kwani wanajua tukikamata wasiohusika wao watajiona wameshinda hawajakamatwa,” alisema Mulongo.

Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa aliwataka pia wanasiasa nchini kutoigeuza milipuko ya mabomu hayo kama njia ya kujitafutia umaarufu wa kisiasa.

“Kugeuza tukio hili la kinyama kuwa agenda ya kisiasa kunaidhalilisha Tanzania nje ya nchi na kuleta athari za kupoteza wageni,” alisema Mulongo.

Mulongo alisema taarifa za awali za kikachero zinaonyesha kuwa bomu lililorushwa katika viwanja vya Soweto lilitengenezwa China.

Mkuu huyo wa mkoa alisema, tayari wataalamu kutoka China wamekwisha wasili jijini Arusha kwa ajili ya kufanya utambuzi wa taasisi iliyonunua bomu hilo.

Mulongo katika hotuba yake aliendelea kuwataka wanasiasa kuacha dharau na kueneza maneno yasiyo na ukweli juu ya Serikali, badala yake aliwataka kuheshimu taratibu za nchi ili vyombo vya dola visilazimike kutumia nguvu kukabiliana na watu au kikundi kitakachovunja sheria zilizowekwa.

“Hivi ndugu zangu, lazima tufike mahali tujiulize hawa wanasiasa wanaotumia uongo na nguvu nyingi kuchafua nchi huko duniani, wanafanya hivi kwa faida ya nani?” alihoji Mulongo.

Bomu hilo lilirushwa katika mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendelo (CHADEMA), wakati kikihitimisha kampeni zake za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata nne jijini Arusha Juni 15, mwaka huu.

Hata hivyo, siku mbili baada ya mlipuko huo, chama hicho kilitoa shutuma nzito dhidi ya Jeshi la Polisi na kueleza kuwa askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), ndiye aliyerusha bomu hilo.

Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe, aliwaeleza waandishi wa habari kuwa chama chake kinao ushahidi wa picha na sauti unaothibitisha kwamba polisi ndio wahusika wa mlipuko huo.

Hata hivyo, chama hicho kimegoma kukabidhi ushahidi huo kwa jeshi hilo kwa maelezo kuwa ushahidi huo hauwezi kutolewa kwa polisi, ambao ni watuhumiwa wa tukio hilo.

Chama hicho kilitoa sharti kwa Rais Jakaya Kikwete kuunda Tume ya Mahakama itakayohusisha majaji waadilifu na kusema kuwa kipo tayari kutoa ushahidi huo mbele ya tume hiyo na si polisi.

Mbali na bomu hilo, bomu jingine lilirushwa katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Olasiti na kusababisha watu watatu kufariki ambapo nalo liligundulika kutengenezwa nchini Urusi.

Habari kutoka Gazeti la Mtanzania.
eeh ka ni ukichaa basi umepanda kichwan kabisa, eti wanahutumiwa kuratibu hyo mipango ya kishetan nao wanataka kutuonyesha wamekuwa makachero bigwa..........!!! iko wapi mipango dhabiti ya kudhibiti hayo majanga kabla hayajatokea????? uongozi dhaifu, mambo yako hovyo kabisa!!!!
 
Magese mulongo ni muongo nani janga la taifa.ana wasiwasi kibarua kitaota nyasi baada ya mbinu zao zote chafu dhidi ya chadema kutofanikiwa.hasa bosi wake kikwete atamhamisha soon maana ameshindwa kuidhoofisha chadema ndani ya jiji la arusha.
 
Polepole tutafika.

Hizi longo longo zote tunazozisoma hapa JF za baadhi ya watu kusema wanawafahamu waliosababisha haya maafa ya kinyama Arusha lakini wakiambiwa na wapenda AMANI wawataje kwa majina au kuonyesha tu sura zao na ushahidi, lakini wanashindwa kufanya hivyo.

Hii ni sawasawa na genge la wizi ambao wakiiba wanaanza kupiga kelele na kumnyoshea vidole yule waliyemwibia huku wakipiga kelele na kusema mwizi, mwizi, mwizi ili wasijulikane katika macho ya sheria kama wao ndiyo wezi.

They can't fight TRUTH with LIE.

Bado Mwigulu, Mungu hachezewi

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ia-maisha-mh-msigwa-afariki-dunia-ghafla.html
 
Polepole tutafika.

Hizi longo longo zote tunazozisoma hapa JF za baadhi ya watu kusema wanawafahamu waliosababisha haya maafa ya kinyama Arusha lakini wakiambiwa na wapenda AMANI wawataje kwa majina au kuonyesha tu sura zao na ushahidi, lakini wanashindwa kufanya hivyo.

Hii ni sawasawa na genge la wizi ambao wakiiba wanaanza kupiga kelele na kumnyoshea vidole yule waliyemwibia huku wakipiga kelele na kusema mwizi, mwizi, mwizi ili wasijulikane katika macho ya sheria kama wao ndiyo wezi.

They can't fight TRUTH with LIE.

...........Kaka, unataka Polisi wapewe huo ushahidi si unataka ushahidi upotelee hewani. Mara ngapi serikali wameomba ushahidi hata Bungeni lakini wamepiga kimya? Mara ngapi Mwakyembe kapeleka taarifa za kundi la watu kutaka kumdhuru na akawataja, hao Polisi walichukua hatua gani?

Tusimung'unye maneno, tusijitie upofu wala tusijitie uchizi tusiokuwa nao, inajulikana kabisa kuwa serikali/ccm wamehusika kwa namna moja au nyingine katika ulipuaji wa mabomu hayo kwa nia ya kuuwa watu kama walivyomuuwa Mwangosi na wengineo.

Mulongo kashaanza kutoa taarifa kuwa Bomu lililorushwa katika mkutano wa Chadema lilitengenezwa China na lile lililorushwa kanisani lilitengenezwa Urusi. Kumbuka kuwa hata Mwakyembe kwenye maelezo yake alidai sumu aina ya Polonium iliyomdhuru iliingizwa Bongo na Jasusi kutoka moja ya nchi zilizokuwa chini ya Jamhuri ya Urusi ya zamani akishirikiana na makachero vibaraka wa CCM (Taarifa za uzi unaoelezea hili suala uliwahi kuwekwa hapa JF)......ukijaribu ku-connect dots kwenye uhusika wa bomu kutoka Urusi na sumu ya kumdhuru Mwakyembe kutoka Urusi, bila ya shaka utajua kuwa huu ni muendelezo wa sarakasi na sambasoti za ccm na serikali yake ambao hawaishi kujitekenya na kucheka wenyewe kila siku.

Nachoona mimi hapa mnajaribu kukwepesha ukweli kwa kuwaweka watu wanaoweza kuficha huu ukweli katika timu za uchunguzi kama akina Chgonja ila mwisho wa siku ukweli utajulikana, nyeupe itakuwa nyeupe na nyeusi itakuwa nyeusi. Watanzania tuendelee kumuomba Mungu atupe amani na awafichue wahusika halisi wa uovu unaotokea ili tuepukane na stori za uchunguzi unaendelea kila kukicha bila ya kupatiwa majibu ya maana.
 
Ama kwa hakika ccm na serikali yake wamechoka kama alivyosema waziri mkuu Pinda.Drama zinaendelea kila kukicha.

Kutoka FBI hadi kwa wachina!? Report itakayotolewa haitakuwa na lolote jipya ama kubaini walipuaji wa mabomu Arusha. Sanasana wachina wataisaidia ccm kuuficha ukweli ambao ni dhahiri kuwa wao ndio walinunua silaha China na kuzitumia kuwalipua wananchi wa Arusha.
 
CCM na Wachina CDM na Mungu.! Sauti ya wengi ni sauti ya MUNGU. waache waendeleze Ngonjera ila ukweli utabaki kuwa ukweli siku zote.....kila lenye Mwanzo hakika lina Mwisho.

MULONGO ni janga la Arusha.shida ya huyu mkuu wa mkoa ni Ukada uliomjaa sana. Ndio maana aliambiwa anatembea kama yuko kwenye Send off!!
Wanachotaka kufanya ni kujitahidi kuufiche ukweli ila watawaficha binadamu lakini MUNGU wa haki anajuwa kila kitu. Na waliouawa ni binadamu wala sio mbwa!

Jamani hata kuuwa Mbwa wa mtu unahitaji Kibali. Sasa hawa wanaouwa watu halafu bado wanaleta siasa, je Mungu atawavumilia!!?

Uzuri wa Mungu yeye anajuwa kila kitu na siku moja watu wataulizwa damu walizomwaga. Eti watu wanatafuta Umaarufu wa kisiasa! Hivi jamani ni kiongozi gani wa CDM sio maarufu?
Labda Mulongo ndie anaetafuta umaarufu kwa mgongo wa CDM.

Mbona Padri aliuawa Zanzibar na ni FBI ndio waliitwa kuja kuchunguza?...mbona Bomu lililolipuliwa Kanisani pia waliitwa FBI? Kwanini hili la mkutano wa CDM ni Wachina ndio wachunguze?

Huo mchezo unaopangwa kuchezwa hautafanikiwa maana Biblia inasema wazi kuwa Kila Pando lisilopandwa na MUNGU litangolewa.

CCM NA WACHINA!!
CDM NA MUNGU!!!
 
kwa hayo maneno tu ni dhahiri hapa kuna mtu ameishaingizwa mtegoni.
Jamaa anajua majibu tayari maana hapa anaizungumzia chadema kwa tafsiri yangu ila haki lazima ishinde hata km ni miaka elfu moja
 
Kwa sasa nchi hii kila kitu feki ni kile cha KICHINA, kama msemo huu ni wa kweli vipi hawa makachero nao si feki pia? Halafu tujiulize katika dunia hii vyombo vya uchunguzi vya nje vinavyotambulika katika uchunguzi wa matukio ,bali mbali duniani ni Interpool, FBI au CIA hawa wachina wametokea wapi?
 
CCM ni wajinga kweli, yaani uongo wautungao huwa unawatosha kuwadangany wao wenyewe.....nani kawaambia wageni wana time n ahayo mabomu yao?ndio shida ya kuwa detached na reality..hata pakistani ugaidi wake wageni wanakwenda kula raha..Mwigulu na mulongo wanajidanganya sana.
 
unajifariji tu ni sawa na kuoga kwenye shamba la matembele halafu ukadhani uko salama huonekani,

Mlisema mnaushahidi utoweni sasa tuone au pelekeni kwa rafiki zenu german,damu za watu malizo mwaka zitawaandama mpaka mwisho.

Dvr ina kila kitu ndugu mjumbe wa nyumba kumi , pole sana maana mapovu yanayokutoka yanaashiria kifafa chako cha kurithi !
 
Maelezo marefu lakini ukiyachambua neno kwa neno unagundua kuwa hakuna neno lililobeba ushahidi zaidi ya udaku wa kwenye vijiwe vya kahawa na ofisi za bavicha.

Ni vigumu sana wakati mwingine kugenga hoja objectively na kueleweka kwa mtu ambaye kwake udaku ndiyo ukweli kwa maana nyingine, fikra zake niza kibavicha bavicha.

Kama mpangilio wa sentensi kwako ni bado ni somo ambalo unahitaji mwalimu, utawezaje kujenga hoja yenye kubeba mantiki ili ijibiwe kimantiki.

Inawezekana hoja yako haikunilenga mimi na hata kama ilinilenga mimi basi sina budi kusema samahani kwa sababu siwezi kuipa majibu kadri unavyotaka kwa vile haina mantiki.

Endelea na ndoto zako za mchana zinazosindikizwa na empty rethoric ukidhani kupiga kelele nyingi ndiyo kupata kile unachokiota kwenye ndoto zako za mchana.
Wewe ni mtu wa mwisho kunipa lecture. Natumia kichwa kufikilia...wewe unatumia tumbo. So we dont belong together. Huwezi kujibu hoja sababu huna majibu.
Mbona sikukuona na hizo objective na subjective kwenye press conference ya Obama?
Huipendi nchi yetu ndo maana unaisaliti kwa tumbo lako.
 
Back
Top Bottom