Mabomu Arusha: Makachero wayafichua mapya

Mabomu Arusha: Makachero wayafichua mapya

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2013
Posts
5,536
Reaction score
2,268
*Wataalamu kutoka China watua kuchunguza

*P
olisi watamba kufichua siri ya milipuko yote

TAARIFA za awali kutoka kwa makachero wa Jeshi la Polisi nchini zimefanikiwa kubaini mtandao wa ulipuaji mabomu katika jiji la Arusha, imefahamika. Mpaka sasa taarifa zinadai mtandao uliohusika na milipuko miwili iliyotokea kwa nyakati tofauti jijini hapa ulipangwa ndani ya jiji la Arusha.

Mlipuko wa kwanza ulitokea katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Olasiti, Mei 5, mwaka huu na kuua watu watatu, wakati mlipuko wa pili ulitokea Uwanja wa Soweto Juni 15, mwaka huu na kuua watu wanne, huku majeruhi wa matukio yote wakifikia zaidi ya 100.

Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Arusha (RCC) jana jijini hapa, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, alisema mbinu hizo zimejulikana kutokana na wananchi waliojitokeza kuwasilisha ushahidi kwa vyombo vya dola.

Alisema mpaka sasa ushahidi unaonyesha kuwa mtandao wa waliolipua wa mabomu hayo ulianzia jijini Arusha, na kikubwa kabisa wanawashukuru wakazi wa Arusha waliokuwa wakifika kutoa ushahidi wa wahusika.

"Ukweli wa mambo haya utajulikana hivi karibuni na Serikali itamchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kuhusika na mtandao huo, bila kujali wadhifa wake. Mambo haya yamedhalilisha na kufedhehesha Taifa," alisema Mulongo.

Akiwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, aliendelea kubainisha kuwa upelelezi wa matuko hayo mawili unaendelea kwa umakini mkubwa na kikubwa kinachoangaliwa ni kuepuka kukamata watu wasiohusika.

"Tunachukua umakini ili waliofanya hivi vitendo vya kinyama wasiendelee kutamba, kwani wanajua tukikamata wasiohusika wao watajiona wameshinda hawajakamatwa," alisema Mulongo.

Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa aliwataka pia wanasiasa nchini kutoigeuza milipuko ya mabomu hayo kama njia ya kujitafutia umaarufu wa kisiasa.

"Kugeuza tukio hili la kinyama kuwa agenda ya kisiasa kunaidhalilisha Tanzania nje ya nchi na kuleta athari za kupoteza wageni," alisema Mulongo.

Mulongo alisema taarifa za awali za kikachero zinaonyesha kuwa bomu lililorushwa katika viwanja vya Soweto lilitengenezwa China.

Mkuu huyo wa mkoa alisema, tayari wataalamu kutoka China wamekwisha wasili jijini Arusha kwa ajili ya kufanya utambuzi wa taasisi iliyonunua bomu hilo.

Mulongo katika hotuba yake aliendelea kuwataka wanasiasa kuacha dharau na kueneza maneno yasiyo na ukweli juu ya Serikali, badala yake aliwataka kuheshimu taratibu za nchi ili vyombo vya dola visilazimike kutumia nguvu kukabiliana na watu au kikundi kitakachovunja sheria zilizowekwa.

"Hivi ndugu zangu, lazima tufike mahali tujiulize hawa wanasiasa wanaotumia uongo na nguvu nyingi kuchafua nchi huko duniani, wanafanya hivi kwa faida ya nani?" alihoji Mulongo.

Bomu hilo lilirushwa katika mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendelo (CHADEMA), wakati kikihitimisha kampeni zake za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata nne jijini Arusha Juni 15, mwaka huu.

Hata hivyo, siku mbili baada ya mlipuko huo, chama hicho kilitoa shutuma nzito dhidi ya Jeshi la Polisi na kueleza kuwa askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), ndiye aliyerusha bomu hilo.

Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe, aliwaeleza waandishi wa habari kuwa chama chake kinao ushahidi wa picha na sauti unaothibitisha kwamba polisi ndio wahusika wa mlipuko huo.

Hata hivyo, chama hicho kimegoma kukabidhi ushahidi huo kwa jeshi hilo kwa maelezo kuwa ushahidi huo hauwezi kutolewa kwa polisi, ambao ni watuhumiwa wa tukio hilo.

Chama hicho kilitoa sharti kwa Rais Jakaya Kikwete kuunda Tume ya Mahakama itakayohusisha majaji waadilifu na kusema kuwa kipo tayari kutoa ushahidi huo mbele ya tume hiyo na si polisi.

Mbali na bomu hilo, bomu jingine lilirushwa katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Olasiti na kusababisha watu watatu kufariki ambapo nalo liligundulika kutengenezwa nchini Urusi.

Habari kutoka Gazeti la Mtanzania.
 
Kachero wenu ni Mulongo na Mwigulu ambao ni washukiwa wa kadhia hiyo,maccm hamna njia ya kunusurika na anguko lenu
 
Polepole tutafika.

Hizi longo longo zote tunazozisoma hapa JF za baadhi ya watu kusema wanawafahamu waliosababisha haya maafa ya kinyama Arusha lakini wakiambiwa na wapenda AMANI wawataje kwa majina au kuonyesha tu sura zao na ushahidi, lakini wanashindwa kufanya hivyo.

Hii ni sawasawa na genge la wizi ambao wakiiba wanaanza kupiga kelele na kumnyoshea vidole yule waliyemwibia huku wakipiga kelele na kusema mwizi, mwizi, mwizi ili wasijulikane katika macho ya sheria kama wao ndiyo wezi.

They can't fight TRUTH with LIE.
 
Niliposoma kichwa cha habari nilifikiria kwenye habari kutakuwa na mapya kwa mfano wamegundua ni nani wanahucka na kina nani wapo nyuma yao. Kumbe ni the same story ambayo tumeshackia.
 
ha ha ha ha gazeti Mtanzania,mleta kachero Mulongo watu wako kwenye centre ya ushetani wa maauaji watajipaka kinyesi usoni kufuta ukweli haiwezekiani ha ha any way diwani wa igoma hii habari ipo hapa jamvini tangu asubuhi ma ma nanii hajakuamsha akuona kilichopo jamvini
 
Hapo haihitaji hata elimu ya kiintelijensia,

Mwigulu alisema watu watakufa Arusha na wakafa, hamna alofanywa hadi sasa japo Igp kusema watafuatilia usemi wake,

Hizi oropaganda tunaanza kuzizowea, yaani jeshi la polisi na vyombo vya usalama wamekuwa wanasiasa tofauti na malengo yiyo anzisha hivi vyombo. Tytayasikia mengi halafu itatoka kauli HUU NI UPEPO UTAPITA.
 
Polepole tutafika.

Hizi longo longo zote tunazozisoma hapa JF za baadhi ya watu kusema wanawafahamu waliosababisha haya maafa ya kinyama Arusha lakini wakiambiwa na wapenda AMANI wawatage kwa majina au kuonyesha tu sura zao na ushahidi, lakini wanashindwa kufanya hivyo.

Hii ni sawasawa na genge la wizi ambao wakiiba wanaanza kupiga kelele na kumnyoshea vidole yule waliyemwibia huku wakipiga kelele na kusema mwizi, mwizi, mwizi ili wasijulikane katika macho ya sheria kama wao ndiyo wezi.

They can't fight TRUTH with LIE.

I doubt if you are not a problem!!
 
CHADEMA ipeleke ushhidi kwa FBI (kama wanao). Isije ikawa ule msemo wa mchagua jembe.........!
 
Kama mimi ndo niwe nimehusika halafu nisikie hiyo taarifa,ntakuwa naongelea timbuktu,kwanini wasiwakamate kama wameshajulikana,hamna haja ya kutuandaa kisaklojia kuhusu hao mtakaowakamata bila kujali wadhifa wao,WAKAMATENI TU KABLA HAWAJATOROKA.
 
Polisi wametamba????????????????????? Kufichua?????????????????????
 
Niliposoma kichwa cha habari nilifikiria kwenye habari kutakuwa na mapya kwa mfano wamegundua ni nani wanahucka na kina nani wapo nyuma yao. Kumbe ni the same story ambayo tumeshackia.

mie baada ya kuona mwandishi ni MwanaDiwani hata sikujsumbua kusoma
 
Last edited by a moderator:
Ha ha ha ccm ni chama cha kijamaa(kikomunist),mabomu yametoka urusi na china,.(mataifa ya kijamaa na rafiki wa ccm')..aliyeonekana kurusha bomu ni policcm! Sasa mulongo anachunguza nini?
 
CHADEMA ipeleke ushhidi kwa FBI (kama wanao). Isije ikawa ule msemo wa mchagua jembe.........!

fbi ni ya wamarekani hapa haihusiki,kama wapo watakua wameitwa kusaidia tu,cdm wapeleke hiyo video yao mahakamani kama kweli wanayo(ingawa ukweli ni kwamba hawana kitu kama hicho).
 
Hakuna jipya hapa badala yake naona ni siasa tu ya kupoteza machungu ya wananchi kwa kuwasahaulisha.
 
haya yote yatafika mwisho tu huwezi kufanya kitu tz usijulikane lazima siku moja wapatikane wote.
 
Hahahahahaha!!!
Mwanadiwani bana, mbona mnakimbia kivuli chenu wenyewe?
Bomu limetoka china Abdultembo Kindovu na mwenzake Mwigulu walitoka china kisha umamleta huyo mchina sijui aje kuangalia performance ya bomu lake ili aangalie kama ataliongezea au apunguze uzani, mnajua wenyewe.
Au unataka kutuambia FBI wa kichina wa zanzibar hawakufanya kazi vizuri mkaamua mkalete Wachina wenyewe?
Au unataka kutuambia jeshi la polisi linaendeshwa na wataalam kutoka china, jeshi letu la policcm halina wataalam kabisaaa?
Naona mnajaribu kuangalia upepo unavuma kutoka kusi au . . . .
Endeleeni kujidanganya wenyewe kwa wenyewe.
 
Nimekuja mbio nikijua ni wale makachero wa obama wameenda kutia nguvu ya kusaka wauwaji
daaah
 
Back
Top Bottom