Mabinti wanaomaliza vyuo na kurudi nyumbani wananyanyapaliwa sana na wazazi kuliko vijana wa kiume

Hebu fanya kuweka mawasiliano ya hao wawili, kuna vikazi kibao vya kujiskiza hii dar.

Ni ajabu binti kusema hana kazi dar ni ajabu mno, mabinti wanaajirika sana kwenye sekta nyingi.

Ujue mzazi anamchoka kwakua ni kula kulala, at 25yrs kua kula kulala haipendezi aisee.
Ajishkize hata kwenye shughuli yoyote walau awe anatoka asubuhi na kurudi jioni, atapata tu akili ya kusepa.

Sisi ndo tubadili mindset, ila kuwalaumu hao wazazi ni kazi bure.

Niko single, niunganishe na mmoja wapo nipate jiko mie. #joke
Mmoja anafanya kazi ila still home wanaona kama "BADO HAITOSHI".... Yani mama mtu ana kitu moyoni anatamani akiseme lakini ndo ivo hawezi kukisema directly..
 
Wanateswaje?
Wananyanyaswaje?
Hakuna watu wanaojua kutia huruma kama hao wanaokaa nyumbani, hizo ni mbinu tu wanazitumia ili wasaidike kwenye mambo yao.
 
Inategemea na aina ya familia !! Mzazi anayejitambua hupenda kuona yaliyo mazuri kwa uzao wake !!
 
Ni uzembe was Hali ya juu ukamaliza chuo ukarudi nyumbani yaani UZEMBE MKUBWA SANA!!!

IWE KWA KIJANA WA KIUME AU KIKE DON'T GO BACK HOME!!

Ukifika mwaka was pili kafanye field za kimkakati huko unapoenda field Jenga urafiki na in service was pande hizo,chukua namba and keep in touch!!
Ukimaliza nenda kajitolee huku ukiomba KAZI in advance ikitokea pale pale,uwe ni teacher,uwe ninmwanasheria uwe nani just nenda kajitolee pale chapa kazi huku ukimuomba mungu aiseh utapata fungu lako!!!

Mi nilipomaliza chuo niliambiwa nirudi sijui Kuna kuvuna alizeti sijui vitu Gani,nikasema Kuna mchongo nafukuzia!!

Nikapiga mzigo was kutosha,Hadi naenda job nilikua kama na laki tisa za kuanzia life ongeza na za kujikimu 1.5 million nikapanga geto langu,Hadi seniors wakaniona mtamu kama mcharo vile!!

Yaani kitanda,sofa,jiko la gesi makapeti aiseh I was good those days!!hadi member mmoja akataka ni msajili!!!

DON'T GO BACK HOME!! DON'T I SAY!!!
 
Hili huenda likakushangaza lakini ndiyo ukweli wenyewe. Hii hali ipo sana sana mijini, nimeshashuhudia mabinti kadhaa hasa wanaotoka familia za kati na duni wakiwa wanaishi kwa tabu sana na wazazi pindi wanaporudi nyumbani baada ya kumaliza vyuo.

Wa kwanza alimaliza SUA mwaka 2020. Akarudi kwao Dar kwa mzazi wake aliyebaki hai ambaye ni mama. Yule binti mateso na manyanyaso aliyopitia mpaka ilifika kipindi akataka kuondoka kwao, ila hakuwa na pa kwenda. Bahati nzuri akapata kazi serikalini, baada ya kupata kazi ndiyo angalau wameanza naye ni mtu.

Wa pili kamaliza chuo mwaka jana tu hapo UDSM. Huyu wazazi wake wote 2 bado wako hai. Mzee wake alishastaafu ila mama bado anafanya kazi. Kwa jinsi anavyoteswa na wazazi wake yupo kwenye hatua za mwisho kuondoka kwao aende anakokujua akajitafutie maisha. Na hana boyfriend, ananiambiaga wazi angekuwa naye basi angeshasepa kitambo akaishi naye.

Huyu hata akitokea mtu akamuambia muda huu njoo tuishi wote anaenda. Vituko na visa anavyofanyiwa na wazazi wake mpaka huwa namuuliza "Una uhakika hao ni wazazi wako? Maana wameshafikia mpaka hatua ya kumuambia aondoke ndani mwao. Cha kushangaza ni kwamba hapo nyumbani yupo kaka yake na anasema huwa hapewi harrassments kama anazopewa yeye.

Wa 3 huyu naye yuko Dar. Alisoma Diploma ya Sheria kisha akawa yupo tu nyumbani hajabahatika kuajriiwa mpaka sasa. Huyu naye ni yaleyale, ameteswa kisaikolojia na wazazi mpaka sasa ukimuona amekonda mno. Ilifikia mpaka kipindi alitaka kufanya suicide kwa sababu ya psychological torture aliyokuwa anapitia toka kwa wazazi wake.

Je, hii ni wakeup call kwa mabinti walioko vyuoni kuhakikisha hawamalizi vyuo bila wenza, na wasirudi makwao maana hawataepuka mateso? Maana kulingana na nature yetu waafrika, ni rahisi sana kuishi na kijana wa kiume nyumbani kuliko binti. Yani binti ambaye umeshafika miaka 26+ kukaa na wazazi nyumbani ina tension kubwa kwa wazazi kuliko kuishi na kijana wa kiume.
Ndio ujikute unaona mbwa kama hao utajuta akijipata siku za mbeleni
 
Sijasoma post yako yote
Ila baadhi ya mabint huwa na matumizi ya hali ya juu sana wawapo vyuoni ukilinganisha na watoto wa kiume
Fikiria anatoka familia masikini lakini pamoja na kupata pengine 80% ya mkopo hawa wenzetu wakiwa vyuoni hujisahau na kujifananisha na watoto wa walamba asali. Sasa kwa kuwa familia (Masikini) inatumia uwezo wake wote hali inayopelekea kukopa na pengine kuuza mbuzi, kuku nk ili bint asome kwa raha...hii hufanya Familia imuone mzigo anapo rudi nyumbani baada ya masomo

Watoto wa kiume wengi wao, husoma tu kwa kuunga unga hata kama amepata mkopo wa 60% hivyo hata akimaliaza haonekani kuwa mzigo saaana...
 
Hili huenda likakushangaza lakini ndiyo ukweli wenyewe. Hii hali ipo sana sana mijini, nimeshashuhudia mabinti kadhaa hasa wanaotoka familia za kati na duni wakiwa wanaishi kwa tabu sana na wazazi pindi wanaporudi nyumbani baada ya kumaliza vyuo.

Wa kwanza alimaliza SUA mwaka 2020. Akarudi kwao Dar kwa mzazi wake aliyebaki hai ambaye ni mama. Yule binti mateso na manyanyaso aliyopitia mpaka ilifika kipindi akataka kuondoka kwao, ila hakuwa na pa kwenda. Bahati nzuri akapata kazi serikalini, baada ya kupata kazi ndiyo angalau wameanza naye ni mtu.

Wa pili kamaliza chuo mwaka jana tu hapo UDSM. Huyu wazazi wake wote 2 bado wako hai. Mzee wake alishastaafu ila mama bado anafanya kazi. Kwa jinsi anavyoteswa na wazazi wake yupo kwenye hatua za mwisho kuondoka kwao aende anakokujua akajitafutie maisha. Na hana boyfriend, ananiambiaga wazi angekuwa naye basi angeshasepa kitambo akaishi naye.

Huyu hata akitokea mtu akamuambia muda huu njoo tuishi wote anaenda. Vituko na visa anavyofanyiwa na wazazi wake mpaka huwa namuuliza "Una uhakika hao ni wazazi wako? Maana wameshafikia mpaka hatua ya kumuambia aondoke ndani mwao. Cha kushangaza ni kwamba hapo nyumbani yupo kaka yake na anasema huwa hapewi harrassments kama anazopewa yeye.

Wa 3 huyu naye yuko Dar. Alisoma Diploma ya Sheria kisha akawa yupo tu nyumbani hajabahatika kuajriiwa mpaka sasa. Huyu naye ni yaleyale, ameteswa kisaikolojia na wazazi mpaka sasa ukimuona amekonda mno. Ilifikia mpaka kipindi alitaka kufanya suicide kwa sababu ya psychological torture aliyokuwa anapitia toka kwa wazazi wake.

Je, hii ni wakeup call kwa mabinti walioko vyuoni kuhakikisha hawamalizi vyuo bila wenza, na wasirudi makwao maana hawataepuka mateso? Maana kulingana na nature yetu waafrika, ni rahisi sana kuishi na kijana wa kiume nyumbani kuliko binti. Yani binti ambaye umeshafika miaka 26+ kukaa na wazazi nyumbani ina tension kubwa kwa wazazi kuliko kuishi na kijana wa kiume.
Tabia zao ndizo Zina wafanya wazazi wawachukie, kama bint karudi nyumbani na tabia zake nzuri lazima ataishi vizuri, Mabinti wengi wakitoka chuo wakirudi nyumbani
Hebu fanya kuweka mawasiliano ya hao wawili, kuna vikazi kibao vya kujiskiza hii dar.

Ni ajabu binti kusema hana kazi dar ni ajabu mno, mabinti wanaajirika sana kwenye sekta nyingi.

Ujue mzazi anamchoka kwakua ni kula kulala, at 25yrs kua kula kulala haipendezi aisee.
Ajishkize hata kwenye shughuli yoyote walau awe anatoka asubuhi na kurudi jioni, atapata tu akili ya kusepa.

Sisi ndo tubadili mindset, ila kuwalaumu hao wazazi ni kazi bure.

Niko single, niunganishe na mmoja wapo nipate jiko mie. #joke
Huku Marekani, mzazi anakata huduma kwa mtoto kuanzia miaka 18, ataendelea tu kumsaidia kama bado anasoma! Awe wa kike au wa kiume, hata km anaishi kwake lazima achangie rent au alipe rent nzima. So sio habari ya umaskini bali ni human nature japo uchumi wa Tz hauruhusu. Technically mtoto akienda chuo anatakiwa kutoka hukohuko na kujitafuta hamna kurudi tena nyumbani akirudi maana yake hajapevuka! Period
Mkuu tabia zao za kutaka kuishi maisha ya chuo wakiwa Chini ya wazazi, yani wanataka wafanyiwe kazi zote za Nyumbani na wao kazi yao ni kutembea na kurudi muda wanao utaka.
 
Binti kamaliza chuo at 23-25, analala tu siku nzima ni kuchat tu hana analowaza, yupo ki slay queen hata vyombo tu ndani haoshi, lazima mzazi uone umebeba mzigo ndani, actually sio mabinti tu, hata vijana wa kiume wamekuwa namna hiyo hiyo, lazy affair, kula na kulala tu, hawawasikilizi wazazi wao. Usitegemee baba anayejitambua kukuangalia na kukuchekea.

Pamoja na hayo, umasikini wa kipato unachangia, huwezi kuona hayo kwenye familia za uchumi wa kati au juu.
 
Kuna binti nilikutana nae mrembo sana anatafuta kazi ,alikuwa ana stress nikaongea nae akaanza kulia ,nikamuacha alie kwanza
Nikamuuliza kwanin usirudi nyumbani kwenu Tabora mi nitakupa nauli ,hapa mwanza anaishi tu kwa wazazi wa rafiki yake,akasema bora akae tu kwa watu kuliko nyumbani ni shida sana akanisimuliza visa vya baba ake na mama yake wa kambo!
Ila wazazi tubadilike tufanye nyumbani iwe sehemu amani ya kwa watoto wetu warudi wanapotaka ilimradi wawe na adabu
 
Ukiwaonea huruma ukaoa na kuwaweka ndani siku akipata ajira na kuneemeka kwa mafanikio kifedha anaanza kukuona fakeni si taipu yake, hakuna rangi utaacha kuona hata kama mmepata mtoto naye anajitenga na wewe akawe single mama au akaolewe na mtu taipu yake. Cha kufanya ni kumpigisha chapchap watoto wawili hadi watatu awe mzito asikuache. Masela wengi huwa hawaoi mama mama mwenye watoto wengi wanaogopa mzigo wa kulea watoto wasio wao
True
 
Mkuu shida ya wazaz wengi wa saivi nikupenda kukimbia majukumu sana sana wanajua mtu akila tu ndo kamaliza kilak2 na hata uyo mzaz wako ukiwa huna kazi anakudharau ila ukipata utaona atakavokua na adabu kwako ila kabla ya hapo wanakuona wew ni takataka tu
Aisee umesema kwl kipindi jobless nilikuwa nambiwa nikaoshe mbwa baada ya kupata kazi cijawai osha mbwa..jmn tutafute hela
 
Umaskini ni fedheha. Wazazi wa kiafrika ni shida. Ukihoji unatishiwa kulaaniwa. Wazazi wengi wanawatendea vibaya watoto wao ambao bado hawajajipata kiuchumi. Mtoto aliye vizuri kifedha huheshimiwa na kusikilizwa. Watoto ambao bado hawana kazi wanapitia mengi sana kutokana na upuuzi wa wazazi. Jamii nayo huishia kusema mzazi hakosei. Mimi ninashauri kama watu wazae kwa mpango kuliko kuleta duniani watoto watakaokuja kuishi kifukara. Na kama wewe bado ni maskini sana tumia condom au jiunge CHAPUTA.
Umeandika upumbavu
 
Kuna binti nilikutana nae mrembo sana anatafuta kazi ,alikuwa ana stress nikaongea nae akaanza kulia ,nikamuacha alie kwanza
Nikamuuliza kwanin usirudi nyumbani kwenu Tabora mi nitakupa nauli ,hapa mwanza anaishi tu kwa wazazi wa rafiki yake,akasema bora akae tu kwa watu kuliko nyumbani ni shida sana akanisimuliza visa vya baba ake na mama yake wa kambo!
Ila wazazi tubadilike tufanye nyumbani iwe sehemu amani ya kwa watoto wetu warudi wanapotaka ilimradi wawe na adabu
Duh changamoto.
 
Wale waliotoka vijijini ndiyo huwa wanapata shida mara 2, maana kwanza atarudi nyumbani na kukuta age mate woote wameolewa, pia maisha ni ya tofauti na maisha waliyozoea mjini. Ndo maana ukifanya ka survey utagundua mabinti wengi wa vijijini wanaograduate huwa hawarudi makwao, ni either wanaenda kwa ndugu walio mijini au wanajibebesha kwa jamaa yeyote wafanye sogea tuishi✅
 
Back
Top Bottom