Ushuhuda wa waliomdharau mpaka kumtukana mzazi wa kiume jinsi maisha yanavyowatafuna

LA7

JF-Expert Member
Aug 26, 2019
457
1,746
Nipo na kaka zangu na wadogo zangu zaidi ya 10 ila Kuna wale walifikia hatua ya kumdharau baba na kumtukana wazi wazi bila hofu,

Kwa sasa hakuna hata mmoja ambaye ameweza hata kufikia hata robo ya mafanikio au hata kununua tu hata huo mkweshe wa piki piki ambayo waliipa jina hilo, ambayo mzee wetu ameweza kumiliki,

Kweli wazazi wanakosea lakini sio kufikia hatua ya kumtukana huku ukiwa bado unakula ugali wake, ni heri ujikatae tu kuepusha vurugu nyumbani,

Baba ametutoa mbali licha ya kutuzaa lakini Kuna wakati walidhalilika ili mradi tu sisi tule, leo tumekuwa na akili nyingi mpaka kiasi cha kuwadharau hawa wazazi wa kiume,

Kumbuka pia wewe umezaa na una watoto, ngoja wakue.
 
Back
Top Bottom