Mabere Marando ni nani?

Mabere Marando ni nani?

1.Mabere Marando alikuwa Usalama wa Taifa idara ya Mambo ya Nje.
2. Alikuwa akishughulikia wapigania uhuru wa kusini mwa Afrika.
3. Alifukuzwa usalama na Rais Julius Nyerere kwa sababu hakuwa na kadi ya Tanu, enzi hizo bila kuwa na kadi hiyo, unatimuliwa serikalini.
4. NCCR ilisambaratishwa na Lyatonga Mrema ambaye alikuwa akitaka kuifukuza Kamati Kuu ya NCCR na Marando na wenzake hawakukubaliana upuuzi huo.
5. Marando alisomea sheria Chuo Kikuu cha Dar (UDSM).
6. Aliwahi kufanya kazi Shirika la Sheria tanzania baada ya kufukuzwa na Kambarage usalama.
7. Marando, Mapalala, Ndimara Tegambwage, Said Fundikira na wengine ndio waanzilishi wa mageuzi hapa nchini walipounda kamati yao iliyoitwa NCCR.
8. Marando ndiye aliyemtoa jela Mapalala kwa njia ya mahakama baada ya kuwekwa kizuizini na Nyerere bila kufikishwa mahakamani, aliwekwa kizuizini Jela ya Kisiwani Mafia. Hayo machache yanatosha.
5. Mrema ambaye naye aliwahi kuwa usalama wa taifa naye akatimka NCCR akaenda TLP nako akaanzisha fujo akawatimua waanzilishi akina Lwekamwa na Tao.
 
Si kweli kuwa Marando ni pandikizi, wala hawajahi kurudi au kuwa mwana CCM
 
Gentamycne alijitahidi sana kumuelezea huyo hanspope wa msimbazi.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
1.Mabere Marando alikuwa Usalama wa Taifa idara ya Mambo ya Nje.
2. Alikuwa akishughulikia wapigania uhuru wa kusini mwa Afrika.
3. Alifukuzwa usalama na Rais Julius Nyerere kwa sababu hakuwa na kadi ya Tanu, enzi hizo bila kuwa na kadi hiyo, unatimuliwa serikalini.
4. NCCR ilisambaratishwa na Lyatonga Mrema ambaye alikuwa akitaka kuifukuza Kamati Kuu ya NCCR na Marando na wenzake hawakukubaliana upuuzi huo.
5. Marando alisomea sheria Chuo Kikuu cha Dar (UDSM).
6. Aliwahi kufanya kazi Shirika la Sheria tanzania baada ya kufukuzwa na Kambarage usalama.
7. Marando, Mapalala, Ndimara Tegambwage, Said Fundikira na wengine ndio waanzilishi wa mageuzi hapa nchini walipounda kamati yao iliyoitwa NCCR.
8. Marando ndiye aliyemtoa jela Mapalala kwa njia ya mahakama baada ya kuwekwa kizuizini na Nyerere bila kufikishwa mahakamani, aliwekwa kizuizini Jela ya Kisiwani Mafia. Hayo machache yanatosha.
5. Mrema ambaye naye aliwahi kuwa usalama wa taifa naye akatimka NCCR akaenda TLP nako akaanzisha fujo akawatimua waanzilishi akina Lwekamwa na Tao.

Salute kubwa!

Ahsante sana, umeeleweka sana, maana naona miaka yote ile 3 wamezunguka tu bila majibu sahihi.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Tiss ukiingia ni hadi pumzi yako ya mwisho, hakuna mapumziko wala rikizo.
Kwa hiyo hapo mfanyakazi anakuwa ni mtu wa kazi kwa kwenda mbele, ukisikia/ukahakikishiwa kuwa fulani anafanya kazi huko tuelewe tu kuwa huyo ni mfanyakazi hadi kifo.

Yaani hiyo kazi (kitengo) ni zaid ya ndoa ya Kanisani kuwa hakuna talaka.

wakuu naomba uchambuzi wa kina Juu ya mwanasheria huyu.

1. Alisomea sheria wapi na kuhitimu mwaka gani?

2. Yeye kutamka hadharani kua ni mwanausalama na athari zake kisiasa ndani ya chadema

3. Amewahi kufikia rank gani ndani ya usalama na operesheni alizoshiriki.

4. Mchango wake katika kuinusuru au kuisambaratisha NCCR mageuzi.

5. Uwepo wake CHADEMA na uwezekano wa kuisambaratisha au kuiimarisha.

6. Mafunzo ya ujasusi aliyapatia wapi?

7. kama bado ni agent wa TISS mpaka sasa.
Nayafahamu vizuri hizo namba 2,3,6 na 7 ila sitaweza kukujibu
 
Uzalendo wa Marando umetukuka sana , kabla hajaumwa aliahidi kutoa matokeo ya uchaguzi kwa kadri yatakavyotililshwa na wananchi ndani ya box la kura , ndiye aliyechangia kukimbia kwa mamluki Mrema na wenzake NCCR MAGEUZI .

Huyu ndiye aliyefuta ule mpango wa kishamba wa Mwigulu na wenzake wa kumbambikia John Mnyika SMS za kutungwa ili ionekane kaziandika John .

Mazuri ya Marando kwa cdm ni mengi mno , mengine si vema kuyaweka hapa .
 
Hahaha hahahaa hahahaaaa !
Kwa uwepo wa Mabere Marando pale CHADEMA , Kama ikienda IKULU mwaka huo wanaousema wao 2015 mnichome MOTO !

Kwani hata Uchaguzi wa mwaka ule 2010 Dr Slaa mnadhani hakushinda ? Ameshapewa chake Billions of Money mtabakia WANAHARAKATI tu....

Kuna siku moja mwaka 2010 Mzee mmoja mtu mzima alinieleza kuwa Chama cha Kukiondoa CCM madarakani bado hakijaanzishwa....nlimshangaa sana na sikumuelewaa LAKINI kwasiku zilivyozidi kwenda mpaka leo Mwaka 2013 NIMESHAELEWAA... Nimeshamwamini maneno yake, CHADEMA ina Mapandikizi mengi sana wao wanawaita MAKAMANDA....
Ninaiangalia post ya The Fixer kwa jicho jipya haswa baada ya uchaguzi wa 2015.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom