Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 18,683
- 22,270
Huu ni mfululizo wa kudanganyana na wanaotudanganya wanatuona sisi ni washamba, nimemsikiliza kiongozi mmoja akiendelea kutetea mabehewa duni yaliyoletwa.
Kiongozi huyo akifafanua huku akijiamini alisema kuwa mabehewa yanayosafiri yana vitanda na hoteli! Nikweli zipo treni zenye mabehewa yenye vitanda, hizi ni zile za viwango vya juu sana na ni vyumba vyenye kitanda meza kochi na bafu na ni chache sana, hapa Afrika ni huko Afrika kusini.
Mabehewa tunayoyatumia Tanzania na nchi nyingi sana yana makochi ambayo usiku hutumiwa kama vitanda vya dabodeka, TRC wanalijua hilo hata yale mabehewa ya zamani ya kifahari yaliyojulikana kwa jina maarufu la Aluminium kutokana na rangi yake ndivyo yalivyokuwa.
TRC tuambieni ukweli kuhusu mabehewa yaliyoletwa badala ya kuanza kutuchanganya na mipango ya kutandaza SGR nchi nzima mpaka Ruvuma na kwingineko, kwetu sisi vitanda si hoja, hoja ni ubora wa mabehewa ya SGR.