Mabehewa ya treni za safari fupi hayana vitanda, mabehewa ya treni za safari ndefu yana vitanda

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,568
22,172
Huu ni mfululizo wa kudanganyana na wanaotudanganya wanatuona sisi ni washamba, nimemsikiliza kiongozi mmoja akiendelea kutetea mabehewa duni yaliyoletwa.

Kiongozi huyo akifafanua huku akijiamini alisema kuwa mabehewa yanayosafiri yana vitanda na hoteli! Nikweli zipo treni zenye mabehewa yenye vitanda, hizi ni zile za viwango vya juu sana na ni vyumba vyenye kitanda meza kochi na bafu na ni chache sana, hapa Afrika ni huko Afrika kusini.

Mabehewa tunayoyatumia Tanzania na nchi nyingi sana yana makochi ambayo usiku hutumiwa kama vitanda vya dabodeka, TRC wanalijua hilo hata yale mabehewa ya zamani ya kifahari yaliyojulikana kwa jina maarufu la Aluminium kutokana na rangi yake ndivyo yalivyokuwa.

TRC tuambieni ukweli kuhusu mabehewa yaliyoletwa badala ya kuanza kutuchanganya na mipango ya kutandaza SGR nchi nzima mpaka Ruvuma na kwingineko, kwetu sisi vitanda si hoja, hoja ni ubora wa mabehewa ya SGR.
 
Hayo ni used na yamepitwa na wakati
 
Kuna siku mama alisema" tutanunua yaliyotumika ambayo kwa wenzetu hayahitajiki tena(Mitumba) akaongeza japo kwetu yanatufaa na pia tutanunua mapya" Nafikiri haya ndiyo yale used alikuwa anamaanisha so huyo mkurugenzi hasituone hamnazo
 
Serikali inanunuaje vitu vya mtumba?
Basi wanunue gari zao za kiofisi za mitumba siyo zile mpya za kifahari 'Toyota Land Cruiser V8'.
Sheria yetu ya manunuzi ya umma inaruhusu hicho kitu? Mimi sijui naomba kujuzwa.
 
Hivi mna wezaje kuandika makala yote hii bila uchambuzi wa picha? Au mifano?
 
Vitu vingine Nshindwaga kuelewa, sijui muheshimiwa haoni au asikii, sijui lakin wenda ni mmoja wao au ndo mfumo, ixo behewa kwa mwendo kasi mwisho tuje tusikie moja limechomoka
 
Mnapolazimishwa kuwa hayo ni long range missile zinafika hata drc kwa saa moja

Wanajua wanaodanganywa ni wale wale watapiga kelele na wao wanapiga hela tofauti mnaiona hapo

Kila mmoja anajitahidi apate ajira huko ili nae atudanganye na kuiba
Kuna mmoja alisema wakinichagua watalimia meno
Yaliyotokea tunajua
 
Nchi inatakiwa uwepo mfumo wa kuwajibisha wezi bila kutegemea kauli ya Rais ndio ije hizi mambo kiongozi Mkuu asipoongea waswahili wanaendelea kutafuna Nchi haiwezekani waagize yale mabehewa Nje cha maana pale ni zile Karatasi ambazo hamtaki zitumike kufungia hata karanga wahuni wametufungia kwenye behewa lililopakwa rangi...
 
Hivi mna wezaje kuandika makala yote hii bila uchambuzi wa picha? Au mifano?
Tatizo lako unashinda JF, jaribu kusikiliza taarifa za habari na kusoma magazeti, nilichokiandika kiko kwenye magazeti ya leo na taarifa za habari, hapa nimeleta tujadiliane baada ya mimi kunyoosha kidole muda mrefu lakini mtangazaji akanikaushia.
 
Serikali inanunuaje vitu vya mtumba?
Basi wanunue gari zao za kiofisi za mitumba siyo zile mpya za kifahari 'Toyota Land Cruiser V8'.
Sheria yetu ya manunuzi ya umma inaruhusu hicho kitu? Mimi sijui naomba kujuzwa.
Sheria hiyo ilipitishwa kwa vitu kama hivyo.
 
Back
Top Bottom