Mpeni majibu aelewe jamani msimzodoe
Mkuu kazi ya ac ni kupoozesha au kuongeza joto la hewa, kuongeza unyevu wa hewa au kupunguza ( humidification or drying, heating or cooling), mantiki ya kufunga madirisha ni kuwezesha ac kufanya kazi ktk uwezo wake halisi ( load capacity ) kama kukiwa kuna hewa inayoingia na kutoka kwa gari ac itazidiwa uwezo, kumbuka ile hewa iliyopoozwa itakua bado inazunguka ndani ya gari hivyo ac itatutmia nguvu kidogo kuendelea kupooza hewa iliyopo ndani, mkifungua madirisha maana yake ni mnailazimisha ac ipooze dunia yote, haiwezi kwa hiyo itazidiwa uwezo, ndio maana kila ukitaka kuwasha ac hakikisha umefunga madirisha ( ac yenyewe inauwezo wa kuingiza hewa ndani na kuipooza na kuisambaza kwa hyo ata ukifunga madirisha poa tu)