Yajue mambo yanayofanya kiyoyozi (AC isifanye kazi vizuri

yusto chaula

New Member
Aug 21, 2019
3
3
MAMBO YANAYOCHANGIA AIR CONDITIONER (KIYOYOZI) KUSHINDWA KUFANYA KAZI VIZURI

Imeandaliwa na Eng:Yusto chaula

Air conditioner au kiyoyozi ni kifaa kinachotumika kutoa nje hewa ya joto na kuingiza ndani hewa ya ubaridi au kuingiza hewa ya joto na kutoa hewa ya ubaridi.Kifaa hichi kimekuwa kikitumika sana hasa maeneo yenye jotoridi kubwa na yale yenye baridi kubwa ili kuufanya mwili uwe vizuri,maana kama joto likizidi huwa kero kwa binadamu na baridi ikizidi pia humuathiri binadamu.Kwa nchi Yetu maeneo mengi yenye joto watu hupenda kutumia AC,kwa ajili ya kuwasaidia kuondoa joto na kupata hewa ya ubaridi ambayo itawafanya watu wawe comfortable.AC hufungwa majumbani ,ofisini,mahospitalini,mashuleni,vyuoni n.k.
AC imeundwa kwa vitu vikuu vitano vya msingi ,vinavyoisaidia kufanya kazi navyo ni

Na AC hufanya kazi Kama ifuatavyo;

*Refrigerant* huwekwa kwenye system ,hii ni gas ambayo hutumika kwa ajili ya kupoozesha vitu ,refrigerant au gas(damu ya AC) huingia kwenye *Compressor*(moyo wa AC) na kwa Kuwa gas huwa katika namna ya mvuke wenye pressure ndogo hivyo compressor huifanya gas kuwa na pressure kubwa kwa kuicompress ,hivyo hutokea mvuke wenye pressure kubwa.Husafirishwa na kusukumwa na compressor hadi kwenye *Condenser*
ambapo condenser huifanya hiyo gas kubadilika kuwa kimiminika chenye pressure kubwa ,huendelea kusafiri hadi kwenye
*Expansion valve* hapa gas hii iliyogeuzwa kuwa kimiminika hupunguzwa pressure na kuwa na pressure ndogo,huendelea hadi kufika kwenye
*Evaporator*(area to be cooled) refrigerant hii iliyokatika kimiminika huanza kufyonza hewa ya joto kuzunguka evaporator coil(au coil hufyonza hewa yenye oto)na hujikuta imepata joto na kugeuka tena kuwa mvuke wenye pressure ndogo na hupita hadi kwenye compressor kwa mzunguko mwingine.Na eneo evaporator ilipo hu toa hewa ya joto na kupokea hewa ya ubaridi.
Hivyo ndivyo AC inafanya kazi.
Kutokana na technology kukua,watu waliendelea kugundua system mbalimbali za air conditioning ilitokana na pia kupunguza gharama za matumizi ya nishati.Na hivyo,kuna aina sita za AC nazo ni;

*A:Central Air Conditioners.*
Hii ni aina ya AC ambayo ,Compressor,Condenser coil na Evaporator coil zimewekwa sehemu moja,huwekwa juu ya dari au slab.duct hutoa hewa ya joto nje na kuingiza ndani hewa ya ubaridi.

*B: Puctless,mini-split Air conditioners.*
Hii ni AC ambayo compressor na condenser coil zipo nje kwenye outdoor unit.haina ducts,haitumii nishati kubwa lakini ni gharama.

*C:Window Units Air Conditioners.*
Ni AC ambayo compressor,condenser coil,evaporator coil,na Expansion valve zimefungwa pamoja.

*D: Portable unit Air Conditioner.*
Inatumia window kutoa nje hewa isiyotakiwa.Aina hii ya AC huhamishika haikai sehemu moja.

*E:Hybrid Air Conditioner.*
Aina ya AC ambayo inatumia nishati ya fossil fuel au umeme,inasaidia katika kubana matumizi ya nishati.

*F:Geothermal heating and cooling.*
Ni aina ya AC ambayo hutumia joto la ardhini kuingiza ndani na kutoa baridi ya ndani au hutoa joto ndani na kulirudisha ardhini.Hii ni moja ya Best AC duniani pia hukaa muda mrefu.

Pia unapohitaji kufungiwa AC hakikisha unaangalia vitu vifuatavyo
*+budget yako*
*+Eneo husika*
Inakusaidia kuweka AC aina gani na yenye ukubwa upi na idadi ipi.
*+SEER ratings(Seasonal Energy Efficiency Ratio)*
Hii itasaidia either msimu wa joto au baridi,kuifanya AC yako ifanye Kazi vizuri kwa matumizi kidogo ya nishati.AC yenye seer ratings 15 ni nzuri sehemu zenye joto Kali.
*+ Matumizi madogo ya nishati*
Pia angalia AC yenye power consumption au matumizi madogo ya nishati hasa umeme ,kuondoa gharama za nishati Mara kwa mara.
*+Position zinapifungwa AC hasa outdoor units*
Wengi hufunga kwenye uelekeo wa jua na kujikuta AC inatumia umeme mkubwa kutokana na joto kali,pia sehemu zenye msongamano wa nyumba au vitu ,husababisha joto kuongezeka ,funga in free space na sehemu isiyo na jua muda wote.

Baada ya kuangalia utangulizi kuhusu AC ,yafuatayo ni mambo yanayofanya AC isifanye kazi vizuri au ishindwe kufanya kazi,nayo ni;

1: GAS KUPUNGUA/LOW REFRIGERANT

Gas kupungua Husababishwa na kuwekwa kiwango kidogo cha gasi aukuvuja kwa pipe za gas ,hivyo compressor hufanya kazi kubwa ya kusukuma gas na gas huwa na joto kubwa na pressure kubwa na huharibu pia compressor(moyo wa AC) na Compressor ikifa AC haiwezi kufanya kazi,lakini pia husababisha Ac igandishe ,maana hakuna kiwango cha gas(liquid) chenye pressure ndogo kuweza kufyonza joto katika evaporator.

2: FROZEN EVAPORATOR COILS

kazi ya evaporator coil ni kufanya gas ivyonze joto na kutoa hewa ya ubaridi,kama ikiganda Ina maana air system flow inakuwa imeziba na kufanya AC isifanye kazi yake vizuri hivyo coil hazipati hewa ya kutosha ili kufyonza joto.AC kugandisha husababishwa na
-Kukosa air system flow
-Uchafu kwenye air filters
-Uchafu kwenye evaporator coil.
-kupungua kwa gas.

3: PIRTY CONDENSER COIL/UCHAFU KWENYE COIL YA CONDENSER
kazi ya condenser ni kugeuza vapour gas yenye pressure kubwa kuwa Liquid ,hivyo coil zikiwa chafu gas itapita bila kugeuzwa kuwa liquid au kimiminika hivyo,hupelekea AC kushindwa kufanya kazi,maana sehemu zq AC zinategemeana kuweza kufanya kazi.(team work).Pia evaporator coil zikiwa chafu husababisha zizifyonze hewa yenye joto vizuri.

4: FAN KUSHINDWA KUZUNGUKA

kazi ya fani ni kusaidia kutoa nje hewa isiyotakiwa yenye joto ,Hi vyo isipozunguka husababisha AC ishindwe Ku perform vizuri na kupelekea hata compressor kufanya kazi Sana na kuharibika mapema.Hewa itakuwa inaingia haitoki.Hewa inatakiwa iingie na kutoka kwa msaada wa fan imara.

5: GAS KUVUJA KUPITIA DUCTS

Refrigerant line zikitoboka hupelekea gas kuanza kuvuja ,na hupunguza au humaliza kabisa gas.Na gas ikipungua huanza kusababisha matatizo Kama kuganda n.k, hivyo AC itashindwa kufanya vizuri.

6: TATIZO LA THERMOSTAT/THERMOSTAT PROBLEM

Thermostat ni kama sensor kwenye AC huhisi kiwango cha joto kilichopo na kuruhusu AC iwake au izime na hufungwa karibu na evaporator coil,hivyo ikiwa na shida hupelekea kuwaka muda wote na kusababisha ku overcool na inaweza isiwake pia kutokana na ubovu wa thermostat.Haitakiwi thermostat iguse evaporator coil ,maana itaendelea kuwaka bila kuzima na kupelekea over cooling na kutumia nishati kubwa Sana hata compressor itakuwa hatarini.

08 PRAINAGE PROBLEM

Baada ya evaporator coil kuibadili liquid refrigerant kuwa mvuke huacha baadhi ya maji,na katika kitendo hicho Maji hayo hutolewa nje kwa kupitia drainage hose pipe au pipe. Kama maji yatashindwa kutoka itasababisha njia kufunga na kupelekea maji kukosa kwa kwenda hivyo yataharibu performance ya AC.na mara nyingi husababishwa na AC kufungwa vibaya inayopelekea drainage tube kushindwa kutoa maji nje kiurahisi.

09: MATATIZO YA UMEME

AC ili ifanye kazi inahitaji nishati na zilizo nyingi hutumia nishati ya umeme.compressor huhitaji umeme na fan pia hutumia umeme.Kama umeme utasumbua husababisha AC isifanye kazi vizuri au ishindwe kufanya kazi kabisa.Hata capacitor ikifa hufanya AC ishindwe kustart na Ku run.Hivyo kagua Mara kwa Mara system ya umeme.

10: POOR INSTALLATION AND IMPROPER SIZING
AC kufungwa kwenye sehemu yenye nafasi ndogo(nyumba au vitu Vingi) hupelekea kufanya kazi muda mrefu Kutokana na sehemu hizo kuwa na joto jingi na pia ikifungwa uelekeo wa kupigwa na jua pia husababisha compressor kupata joto zaidi na kushindwa kufanya kazi pamoja na coil. Pis kama itafungwa bila allignment nzuri za mountings zake husababisha drainage hose kushindwa kutoa maji vizuri.

11: KUTUMIA REFRIGERANT PIPE ZISIZO SAHIHI

Kama pipe zimechoka na zikabadilishwa zingine za size ndogo au kubwa kuliko ile ya mwanzo hupelekea AC kuanza kufanya kazi chini ya kiwango.Unashauriwa unapofanya repair ya pipes tumia size ambayo manufacturer aliitumia.

12: KUWEKA GAS NYINGI KUPITA KIPIMO SAHIHI

Kila kitu kikizidi huleta shida,hata gas ya AC ikiwekwa nyingi sana kuliko kiwango kilichopendekezwa husababisha pia AC kushindwa au kufanya kazi chini ya kiwango.

13: KUZIBA KWA PIPE ZA GAS
pipe za refrigerant zikiziba husababisha gas isipite kwa urahisi au isipite kabisa na hupelekea AC ishindwe kufanya kazi vizuri.Mfano pia thermal expansion valve zikishindwa kufunga na kufungua husababisha kiwango cha gas kuathirika.

14: SERVICE ILIYOCHINI YA KIWANGO
Service inatakiwa ifanywe na mtu aliyebobea na anayeifahamu vizuri AC ,pia kutofanya service ya uhakika hupelekea air filters kuwa chafu,vumbi kujaa,coils kuwa chafu.Hivi vyote husababisha AC ishindwe kufanya kazi vizuri.

15: KUFUNGUA MILANGO NA MADIRISHA WAKATI AC INAFANYA KAZI
Kama milango au madirisha yamefunguliwa wakati AC inafanya kazi kwenye eneo husika,hupelekea AC kuioverload ,hufanya kazi bila kusimama kutokana na outside hot air kuendelea kuingia na kufanya compressor ichoke pia hata fan huchoka kutokana na wear(as rotating material),hivyo hupelekea AC kushindwa ku perform vizuri.

16: KUTUMIA GAS AU REFRIGERANT TOFAUTI.
Jambo jingine lililoua AC nyingi au kusababisha zishindwe Kufanya kazi ni pamoja na kutumia gas iliyotofauti na ile ya mwanzoni iliyopitishwa na manufacturer kutokana na aina na uwezo wa AC.Tumia gas iliyopendekezwa kwenye AC husika.

17: ELECTRONIC CARD KUFA AU KUTOFANYA KAZI
AC hutumia kadi kama kifaa cha kucontroll ufanyaji kazi wake,na Mara nyingi kadi kufa ndio umekuwa ugonjwa mkubwa.kadi ikifa husababisha AC kutofanya kazi.


Hadi hapo tumefikia mwisho wa makala yetu kwa Leo,tukutane tena wiki ijayo kwa makala nyingine.
 
Back
Top Bottom