G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Wakati Tundu Lissu akiondoka nchini kwenda Ubelgiji kwa matibabu leo, amesindikizwa na mabalozi watatu ambao ni balozi wa Marekani, Ujerumani na Ubelgiji.
Washirika hawa watatu kwa hakika upo ujumbe wanaoutuma kwa serikali ya Tanzania.
Baada tu ya Tundu Lissu kuondoka nchini salama, balozi wa Marekani kwenye ukurasa wake rasmi wa Twitter ameonyesha kufurahishwa na tukio hilo. Aidha anasema kuwa Tundu Lissu anaelekea Ubelgiji kwa matibabu. "Nimefurahi kuwa hatimaye Tundu Lissu ameondoka salama kwenda Ubelgiji" amesema balozi huyo.
Tundu Lissu alibebwa ndani ya gari ya balozi wa Ubelgiji na msafara wao ulipita njiani kuelekea uwanja wa ndege bila kizuizi chochote kile.