SoC03 Mabadiliko ya mifumo ya elimu katika kupambana na changamoto ya ukosefu wa ajira

Stories of Change - 2023 Competition

Mammamia23

New Member
Jun 28, 2023
1
1
Ukosefu wa ajira umekua ni changamoto kubwa Katika nchi ya Tanzania na nchi nyingine nyingi duniani.

Changamoto hii Kwa kiasi kikubwa imechangiwa Kwa kiasi kikubwa na mifumo mibovu ya elimu Katika nchi yetu ambayo haikidhi vigezo vinavyohitajika kwenye soko la ajira na Dunia inayokuwa Kwa kasi.

Kupambana na changamoto hii serikali lazima ifanye mabadiliko na maamuzi magumu Katika sekta hii Kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya serikali na watu wake.

Andiko hili limelenga kuonyesha nini serikali inatakiwa kufanya Kwa ajili ya kuleta mabadiliko Katika nchi.
1.KUUBADILI MFUMO MZIMA WA ELIMU.

Hapa serikali inatakiwa kuboresha mitaala itakayoendana na mahitaji ya soko la ajira kwa kufundisha ujasiriamali na ufundi stadi Kwa wanafunzi wawapo mashuleni.

Mfano mzuri ni kwamba ingekua watoto wanasoma shule ya msingi kuanzia darasa la kwanza hadi la sita na darasa la Saba watafundishwa ufundi wa kuanzia mwaka mzima Kisha wanahitimu.

Sekondari pia iwe mwisho kidato cha tatu kile cha nne mwaka mzima wanafundishwa ufundi stadi mwaka mzima ndio wahitimu hii itachangia kufungua akili Za watoto na kuwawezesha kuchagua njia Za kwenda na masomo ya kuendelea kusoma vyuoni.

Kidato cha tano na sita iwe ni Kwa wale watakaoenda vyuo vikuu lakini wanaenda tayari wakiwa na misingi ya kuanzia hivo hawatakosa cha kufanya hâta watakapmaliza masomo vyuoni.

2. Kuendana na ulimwengu wa sayansi na teknolojia uliopo Sasa hivi walimu waliopo waboreshwe Kwa kuwapa mafunzo na mishahara inayostahili na mafunzo haya yawe endelevu hii ni muhimu kwa kua itahakikisha walimu waliopo wanasifa na si waliopata maksi Za chini Katika mitihani ndo wawe walimu.

3. Elimu yenye ubora itolewe inasikitisha ni miaka 60 toka uhuru lakini bado kunashule wanafunzi wanakaa chini wengine hakuna kanisa madarasa wanasoma nje na kukalia mawe iwapo serikali itatua swala hili kukawa na mazingira rafiki ya kusoma, serikali kutoa ufadhili Kwa wanafunzi kwenda kujifunza teknolojia mpya ,mafunzo kwa vitendo kwa wingi kutafanya wazalishwe wataalamu wenye ujuzi mkubwa wanaohitajika Katika soko la ajira.

4. Elimu ya ujasiriamali Kwa wanaoanza itiliwe mkazo na wapewe mafunzo,mitaji na ufuatiliaji Bila será kandamizi mfano Kodi Hadi watakaposimama wenyewe hii itachochea ubunifu zaidi na kutengeneza ajira mpya nyingi Kisha kukuza uchumi wa nchi

5. Serikali ifadhili tafiti mbali mbali Katika vyuo zinazoweza kuleta gunduzi zenye tija kwa taifa.

6. Kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji kibiashara na viwanda na kuweka será zitakazolinufaisha taifa mfano kaja mchina kujenga kiwanda cha feni labda au simu wazawa ndio inabidi wawe nguvu kazi na wafundishwe pia simu inatengenezwa vipi.

7. Wafanyabiashara wadogo na makampuni madogo yawezeshwe kiuchumi na elimu ya maendeleo ya biashara na serikali yakue Ili yatengeneze ajira na kuongeza ubora wa bidhaa na wigo mpana wa soko kimataifa Ili Sisi tupeleke bidhaa nje badala ya kuleta ndani.

Mwisho kabisa Kwa juhudi za makusudi mambo haya yakifanyika yanaweza kutatua changamoto Za ukosefu wa ajira na kujenga taifa la wasomi na wafanyabiashara hodari.
 
Back
Top Bottom