Elections 2015 Mabadiliko Chanya ya Ujio wa Lowassa: CHADEMA Kuhama Ufipa!, Kuwa Makao Yake, Kituo cha TV na Redio!

Pasco unanipa mashaka katika ukuwaji wako. Naamini umemshushia heshma mama yako si mara moja. umenifanya niamini kwa jinsi mama yako alivyo bomba enzi zake,lakini toka alipo mkubalia baba yako kukutafuta wewe na ndugu zako wengine.
kwa sasa umekua anaanza kumsema vibaya mama yako.huku ni kukosa adabu kwa wazazi wako.
Pia kukosa adabu kwa chama kilicho kupokea
 
Kwa hiyo na nyie mnamkana leo kwa sababu tu kaja CHADEMA, mbona hamjamfukuza uanachama miaka yote hiyo huku mkijua fika kwana ni Fisadi na Mwalimu kumkataa.

Kwani akija CHADEMA ufisadi unaisha? Matusi hayo kaanza anasema kiofisi chenu siyo hadhi yake unasemaje?
 
 
Ndugu Pasco

Kalamu yako inaweza kumponza EL. Kuliko kuibua masuala yasiyo ya msingi kwa sasa saidia kuharmonise ujio wake na misimamo na harakati za CHADEMA. Nadhani makao makuu ya CHADEMA yamesaidia kukiweka chama karibu na wananchi-ambao wengi ni walalahoi. Wewe unasema makao hayo siyo hadhi ya EL !! Ni kweli kwa sababu huenda ukombozi wa wananchi ndicho kipaumbele cha CHADEMA SIYO MAGHOROFA. CHADEMA ni chama cha wanainchi siyo chama cha dola chenye mirija kwenye hazina na taasisi zote kuu za serikali(kumbuka EPA na BOT na Evergreen). Kama unamsemea EL fikiria sana na kutumia kalamu yako kumjenga siyo kumbomoa. Utitiri wa mali za EL unazozungumzia bila ukakasi ndiyo nguvu kubwa ya EL lakini pia udhaifu wake mkubwa. Sehemu kubwa ya rasilimali hii imetumika CCM kwa miaka zaidi ya 10 kuusaka( kuununua Uraisi) lakini ndiyo ikawa njia ya anguko lake(kiCCM) . Na wanaCHADEMA wengi bado wanapata taabu kubwa kukubaliana na ujio wake kwa kuhofia chama kurubuniwa na kupoteza misimamo na malengo yake. Lakini kisiasa wamekubali kwa sababu EL ni political heavywieght. Hivyo ni pigo kwa CCM. Halafu pia katika siasa, hakuna adui au rafiki wa kudumu-Masilahi ndiyo hudumu. Vile vile CHADEMA imekuwa ikipambana na mfumo wa kifisadi ambao hivi sasa ni systemic-siyo individuals. Tafadhali Pasco elimisheni jamii along these lines.
 
Kwani akija CHADEMA ufisadi unaisha? Matusi hayo kaanza anasema kiofisi chenu siyo hadhi yake unasemaje?
yote tisa, kumi jiandaeni kufurusha virago toka kwenye ofisi takatifu ya wananchi mliyoifanya gulio la wanyanganyi.
 
Msomeni vizuri kuna message hapo,si mnakumbuka issue ya zitto kutaka hesabu za vyama vya siasa vikaguliwe ilivyowaudhi kina mbowe?
 
Wanahama ofisi ya kupanga na wanaenda ofisi ya lowassa, watapata radio na tv ya lowassa. Sasa hapo chdema imepiga hatua gani? Unahama kutoka chumba ulicho panga na kuhamia kwenye chumba cha mwenye nyumba.
 
Samahani Pasco, hivi ni Kwa nini una like kila post (kwenye hii thread) ni Kwa sababu wamechangia au umekubali hoja zao? Maana naona zote unatwanga like tu
 
chama kimeshatekwa na mafisadi hicho...

muda si mrefu hata magwanda mtaacha kuvaa mtaanza kugonga mashati ya linen kama kubwa la maadui, the don himself a.k.a mamvi...

poleni kwa kuuza chama kwa sarafu chache...mtagundua wakati gamba limeshashika ngozi na hapo ndipo utakuwa mwisho wenu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…