Mabadiliko Chanya ya Ujio wa Lowassa: CHADEMA Kuhama Ufipa!, Kuwa Makao Yake, Kituo cha TV na Redio!


Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
28,826
Points
2,000
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
28,826 2,000Wanabodi,

Kama ilivyo kawaida yetu, wewe kama mwana JF, be the first to know kuwa ujio wa Lawassa kujiunga Chadema, sio tuu utakipaisha Chadema to unimaginable dimentions kutokana na ufuasi mkubwa wa watu walio nyuma yake, bali ujio huo, unaandamana na neema kubwa ya mambo mengine mengi mazuri, moja kubwa ni kuhama kwa Makao Makuu ya Chadema toka kwenye nyumba ya iliyopo Mtaa wa Ufipa, Kinondoni Dar es Salaam, hadi kwenye eneo jingine lenye nafasi zaidi kufuatia idadi kubwa ya watu wanaotarajiwa kujiunga na Chedema kufutia ujio wa Edward Lowassa kwenye chama hicho.

Hali hii ni kufuatia hali iliyojitokeza jana, wakati Edward Lowassa alipofika Makao Makuu ya Chadema, mtaa wa Ufipa, kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia Chadema, kufuatia umati mkubwa wa wafuasi wa Chadema kufurika kwa wingi hali iliyoleta shida na kero mtaa mzima, kutokana na location ya ofisi hizo zilipo eneo lililozunguka ofisi hizo ni eneo dogo kufuatia ofisi hizo kuwepo kwenye eneo la makazi ya watu. Na hapo hao waliojitokeza ni wafuasi tuu wa Chadema, bado tsunami ya wafuasi wa Lowassa hawajatia timu!, wakitia timu kama hali ilivyokuwa uwanja wa Sheikh Amri Abedi, then Mtaa wa Ufipa, unahatari ya kupata bughudha ya umati mkubwa wa watu.

Ukipiga hesabu ya jumla ya ruzuku yote ambayo Chadema imekuwa ikipokea, na kulinganisha ruzuku hiyo imefanyia nini, utakubaliana na mimi, kuwa fedha hiyo, ingetosha kabisa kujenga jengo jingine kwenye eneo la kutosha. Hali hii imetokana na upangaji mbovu wa vipaumbele vyake, hali iliyopelekea matumizi mabovu ya ruzuku, kama yalivyofafanuliwa kwenye ripoti ya CAG.

Mabadiliko hayo chanya sio tuu kwa Chadema kumiliki jengo lake lenyewe, pia Chadema itamiliki kituo chake cha Redio na Televisheni pamoja na magazeti yake yenyewe, kwa sababu Lawassa hapo alipo tayari anamiliki by proxy wa familia kubwa ya media, yenye vituo vya Redio, TV na magazeti lukuki!, hivyo sasa pia vitatumiwa kuisupport Chadema kwa kuanzia tuu, wakati mchakato wa umiliki rasmi wa vyombo vyake yenyewe ukiendelea!.

Ama kweli mgeni njoo, mwenyeji apone!.

Hongera sana Lowassa!.

Hongera Chadema.

Ikulu 2015 ni ya UKAWA!.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali

Source ya Taarifa hii ni observation yangu binafsi.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu nchini (CAG) amebaini mapungufu katika vitabu vya mahesabu ya CHADEMA na kuhitimisha kwa kuipa CHADEMA hati yenye mashaka &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Qualified opinion' kutokana na mahesabu yake ya mwaka wa fedha unaoishia Ju June 30, 2013.

1)Pamoja na mambo mengine, katika mwaka wa fedha uliomalizika June 30, 2012, CHADEMA ina akaunti zaidi ya 200, ikijumlisha akaunti za Makao Makuu, Kanda, Mikoa, Wilaya na Majimbo lakini Mkaguzi hakuona salio la kufungia kitabu likihusisha akaunti zote zinazotumia jina la CHADEMA.

2)Mkaguzi anasema katika ripoti hiyo kuwa Chadema kilionyesha kina mali zenye thamani zaidi ya Sh650 milioni, ambazo ni magari, mashamba, nyumba na pikipiki. Hata hivyo, CAG anasema hakuona kitabu cha usajili wa mali hizo.

3)Mahesabu ya mwaka unaoishia June 30, 2013 yalionyesha shilingi milioni 40 ambazo hazikuwa na vitabu vyenye mahesabu ya makusanyo yake.

4) CAG alihoji manunuzi ya magari 10 (Ford Ranger) yaliyofanywa bila kuhusisha Kamati ndogo ya chama inayohusika na utoaji wa zabuni za chama (Tender Committee).

5) CAG alihoji ununuzi wa generator yenye thamani ya shilingi milioni 27 bila kuhusisha mchakato wa zabuni.

6)CAG alihoji pia mahesabu yanayoonyesha deni la milioni 47 linalohusiana na vifaa vya ujenzi wakati hata havijawasili kutoka kwenye kampuni ya kichina.
NB. Pakali sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, hajawahi kujiunga na chama chochote cha siasa, sio mfuasi, mshabiki wala mkereketwa wa chama chochote au mwanasiasa yoyote, ila kuna baadhi ya wanasiasa ambao ninawakubali sana akiwemo Edward Lowassa. Ila sijawahi kuwa team Lowassa wala kuhudhuria tukio lolote lililomhusu Lowassa, wala sina mpango wowote, wa kumfuata yoyote, popote, kazi yangu ni to tell nothing but the truth, with objectivity, impartiality and balance from all sides!.


attachment-php-jpg.272685
mmgl2160-jpg.272692
 
Lisa Rina

Lisa Rina

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2010
Messages
1,839
Points
2,000
Lisa Rina

Lisa Rina

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2010
1,839 2,000
Pasco vipi slaa kweli kaonndoka CHADEMA?
 
Bramo

Bramo

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2009
Messages
10,267
Points
2,000
Bramo

Bramo

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2009
10,267 2,000
Pasco na uchumia tumbo wote amepanga Mbagala Kibonde Maji
 
Last edited by a moderator:
Mr.Venture

Mr.Venture

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2014
Messages
1,607
Points
1,500
Mr.Venture

Mr.Venture

JF-Expert Member
Joined Jan 2, 2014
1,607 1,500
Media ni silaha kubwa sana katika siasa. Ikiwa ni kweli basi ujio wa Lowassa utaambatana na rapid expansion ya CHADEMA na UKAWA.
 
Kimbunga

Kimbunga

Platinum Member
Joined
Oct 4, 2007
Messages
13,536
Points
2,000
Kimbunga

Kimbunga

Platinum Member
Joined Oct 4, 2007
13,536 2,000
Pasco

Mkuu Pasco unataka niamini kwamba ulikuwa hujui kuwa CHADEMA wanapanga pale ufipa au ndio michimbezo ya kumpata mgeni?
 
Last edited by a moderator:
Jay One

Jay One

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2010
Messages
12,558
Points
2,000
Jay One

Jay One

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2010
12,558 2,000
Lowassa....Chademaaa, Ukawaaaaa....yaani tunabadili gia juu kwa juu...yaani Ukawa wamecheza game hili kama MESSI VILE... maana ushindi wa kishindo ni saa 2 asubuhii...

Maskini CCM hawa hawajui nn kinaendelea, wako ktk coma...butwaa...wanakanana wenyewe kwa wenyewe...daahh..!!
 
Emmanuel R. Ntobi

Emmanuel R. Ntobi

Verified Member
Joined
Sep 23, 2014
Messages
680
Points
1,000
Emmanuel R. Ntobi

Emmanuel R. Ntobi

Verified Member
Joined Sep 23, 2014
680 1,000
Pasco,
Kama huelewi kitu ni bora kuuliza, we ni mwandishi mkongwe, FYI makao makuu ya CHADEMA si nyumba za kupaga, hizo ni mali za CHAMA toka 2012.

Na pia hakuna mpango wa kuhama, lengo ni kuitoa CCM madaraka si kuwa na HQ ya kifahari
 
Last edited by a moderator:
Julius Kaisari

Julius Kaisari

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Messages
1,175
Points
1,225
Julius Kaisari

Julius Kaisari

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2010
1,175 1,225
Pasco bhana,
Anyway,hata ukiongea common sense tu,nitakuheshimu,regardless ni fact or not. Kwamaana uyanenayo mengi huwa. Hivyo tutegemee jumba la HQ lenye hadhi ya El-premier!
 
Last edited by a moderator:
P

Precise Pangolin

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2012
Messages
12,497
Points
2,000
P

Precise Pangolin

JF-Expert Member
Joined Jan 4, 2012
12,497 2,000
Pasco

Wakinamama na wanafunzi wanavujiwa kwenye hospital na shuleni halafu wewe unaleta mambo ya anasa mpumbavu kweli ofisi zitakuwa mioyoni mwa watanzania
 
Last edited by a moderator:
K

KipimaPembe

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2007
Messages
1,284
Points
1,225
K

KipimaPembe

JF-Expert Member
Joined Aug 5, 2007
1,284 1,225
Chadema kilikuwa chama cha Ukombozi mpaka alipoingia Lowasa sasa kimekuwa Chama cha Matumaini! Kwa chama cha matumaini, ni vizuri wahamie kwenye magorofa marefu kule Samora ndo kwao. Wawaachie wakombozi ufipa yao!
 

Forum statistics

Threads 1,285,935
Members 494,834
Posts 30,879,450
Top