Elections 2015 Mabadiliko Chanya ya Ujio wa Lowassa: CHADEMA Kuhama Ufipa!, Kuwa Makao Yake, Kituo cha TV na Redio!

Pasco unanipa mashaka katika ukuwaji wako. Naamini umemshushia heshma mama yako si mara moja. umenifanya niamini kwa jinsi mama yako alivyo bomba enzi zake,lakini toka alipo mkubalia baba yako kukutafuta wewe na ndugu zako wengine.
kwa sasa umekua anaanza kumsema vibaya mama yako.huku ni kukosa adabu kwa wazazi wako.
Pia kukosa adabu kwa chama kilicho kupokea
 
Kwa hiyo na nyie mnamkana leo kwa sababu tu kaja CHADEMA, mbona hamjamfukuza uanachama miaka yote hiyo huku mkijua fika kwana ni Fisadi na Mwalimu kumkataa.

Kwani akija CHADEMA ufisadi unaisha? Matusi hayo kaanza anasema kiofisi chenu siyo hadhi yake unasemaje?
 
Wanabodi,

Kama ilivyo kawaida yetu, wewe kama mwana JF, be the first to know kuwa ujio wa Lawassa kujiunga Chadema, unaandamana na mambo mengi mazuri, moja kubwa ni kuhama kwa Makao Makuu ya Chadema kwenye kijumba cha kupangisha pale Mtaa wa Ufipa Kinondoni Dar es Salaam, hadi kwenye moja ya majumba yenye hadhi inayolingana na Edward Lowassa.

Hali hii ni kufuatia hali iliyojitokeza jana, wakati Edward Lowassa alipofika Makao Makuu ya Chadema, mtaa wa Ufipa, kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia Chadema, kufuatia umati mkubwa wa wafuasi wa Chadema kufurika kwa wingi hali iliyoleta shida na kero mtaa mzima, kutokana na location ya ofisi hizo zilipo, zilionekana ni kama kichochoroni!. Na hapo hao waliojitokeza ni wafuasi tuu wa Chadema, bado tsunami ya wafuasi wa Lowassa hawajatia timu!, wakitia timu kama hali ilivyokuwa uwanja wa Sheikh Amri Abedi, then nyumba zote huo Mtaa wa Ufipa, zinahatari ya kubomolewa kwa makundi ya watu!.

Kumbe ile ofisi ya Makao Makuu ya Chadema pale Ufipa ni nyumba ya kupanga!. Ukipiga hesabu ya jumla ya ruzuku yote ambayo Chadema imeishalipwa, ingetosha sana kujenga jengo la hadhi na mahali penye hadhi, na kama ni kupanga, hakukuwa na sababu kupanga kwenye kijumba kama kile hadi sasa Chadema ni chama kikubwa!. Hali hii ya Chadema kuendelea kuwepo kwenye kajumba hako, ni kufuatia upangaji mbovu wa vipaumbele vyake, hivyo kupelekea matumizi mabovu ya ruzuku, hali iliyopelekea Chadema kukumbwa na ukata siku zote, na kulazikika kuendelea kupanga kwenye kajumba kale pale Uswahili au Uzwazi Ufipa kwenye kabarabara ka uchochoro madimbwi mwamzo mwisho!.

Kufuatia Lowassa kuwa ni tajiri mkubwa, mwenye hadhi ya hali ya juu, huku akimiliki majengo lukuki, yenye hadhi, kwenye maeneo ya maana 'prime areas', ujio wake utapelekea Ofisi za Chadema kuhama uchochoroni, na kuhamia kwenye jengo la maana litakalo endana na hadhi ya Lowassa na tena haswa kwa kuzingatia Chadema ndicho kinakwenda kugeuka Chama tawala!.

Mabadiliko hayo chanya sio tuu kwa Chadema kumiliki jengo lake lenyewe, pia Chadema itamiliki kituo chake cha Redio na Televisheni pamoja na magazeti yake yenyewe, kwa sababu Lawassa hapo alipo tayari anamiliki Redio na TV!, hivyo sasa vitatumiwa na Chadema kwa kuanzia wakati mchakato wa umiliki rasmi wa vyombo vyake yenyewe ukiendelea!.

Ama kweli mgeni njoo, mwenyeji apone!.

Hongera sana Lowassa!.

Hongera Chadema.

Ikulu 2015 ni ya UKAWA!.

Mungu Ibariki Tanzania.

Pasco


Source ya Taarifa hii ni observation yangu binafsi.[/QUOTE
Kwani ukubwa wa jengo unauhusiano gani na ufanisi? Utajiri wa Lowasa sio wa CHADEMA, unadhani amepokelewa kwa sababu ni tajiri?
 
Ndugu Pasco

Kalamu yako inaweza kumponza EL. Kuliko kuibua masuala yasiyo ya msingi kwa sasa saidia kuharmonise ujio wake na misimamo na harakati za CHADEMA. Nadhani makao makuu ya CHADEMA yamesaidia kukiweka chama karibu na wananchi-ambao wengi ni walalahoi. Wewe unasema makao hayo siyo hadhi ya EL !! Ni kweli kwa sababu huenda ukombozi wa wananchi ndicho kipaumbele cha CHADEMA SIYO MAGHOROFA. CHADEMA ni chama cha wanainchi siyo chama cha dola chenye mirija kwenye hazina na taasisi zote kuu za serikali(kumbuka EPA na BOT na Evergreen). Kama unamsemea EL fikiria sana na kutumia kalamu yako kumjenga siyo kumbomoa. Utitiri wa mali za EL unazozungumzia bila ukakasi ndiyo nguvu kubwa ya EL lakini pia udhaifu wake mkubwa. Sehemu kubwa ya rasilimali hii imetumika CCM kwa miaka zaidi ya 10 kuusaka( kuununua Uraisi) lakini ndiyo ikawa njia ya anguko lake(kiCCM) . Na wanaCHADEMA wengi bado wanapata taabu kubwa kukubaliana na ujio wake kwa kuhofia chama kurubuniwa na kupoteza misimamo na malengo yake. Lakini kisiasa wamekubali kwa sababu EL ni political heavywieght. Hivyo ni pigo kwa CCM. Halafu pia katika siasa, hakuna adui au rafiki wa kudumu-Masilahi ndiyo hudumu. Vile vile CHADEMA imekuwa ikipambana na mfumo wa kifisadi ambao hivi sasa ni systemic-siyo individuals. Tafadhali Pasco elimisheni jamii along these lines.
 
Kwani akija CHADEMA ufisadi unaisha? Matusi hayo kaanza anasema kiofisi chenu siyo hadhi yake unasemaje?
yote tisa, kumi jiandaeni kufurusha virago toka kwenye ofisi takatifu ya wananchi mliyoifanya gulio la wanyanganyi.
 
Msomeni vizuri kuna message hapo,si mnakumbuka issue ya zitto kutaka hesabu za vyama vya siasa vikaguliwe ilivyowaudhi kina mbowe?
 
Wanahama ofisi ya kupanga na wanaenda ofisi ya lowassa, watapata radio na tv ya lowassa. Sasa hapo chdema imepiga hatua gani? Unahama kutoka chumba ulicho panga na kuhamia kwenye chumba cha mwenye nyumba.
 
Samahani Pasco, hivi ni Kwa nini una like kila post (kwenye hii thread) ni Kwa sababu wamechangia au umekubali hoja zao? Maana naona zote unatwanga like tu
 
chama kimeshatekwa na mafisadi hicho...

muda si mrefu hata magwanda mtaacha kuvaa mtaanza kugonga mashati ya linen kama kubwa la maadui, the don himself a.k.a mamvi...

poleni kwa kuuza chama kwa sarafu chache...mtagundua wakati gamba limeshashika ngozi na hapo ndipo utakuwa mwisho wenu!
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom