Elections 2015 Mabadiliko Chanya ya Ujio wa Lowassa: CHADEMA Kuhama Ufipa!, Kuwa Makao Yake, Kituo cha TV na Redio!

Hivi kipaumbele kingekuwa kuwekeza katika nyumba au kuwekeza katika watu.Inawezekana CHADEMA kingewekeza kwenye nyumba kuliko watu,kazi waliyoifanya kwa ustadi mkubwa hata huyo Lowasa labda asingejiunga nao.Tafakari tena.
 
Mkuu Pasco kama umehifadhiwa na jirani kutokana na dhoruba (mafuriko) na ukafanikiwa kulaza kichwa siku mbili tatu, hupaswi utoe kashfa. Hata kama wataka kumsaidia mhifadhi, basi wasaidia kwa heshima; maana vyote ulivyonavyo sasa havikuweza kukupa hifadhi pale ulipoihitaji. Usianze kusema kwamba aah, nyumba yenyewe hii ya majani, huyu jamaa atakuwa anatumia mshahara wote kwenye pombe - lakini kumbuka hapo ndio umepata hifadhi.

Mkuu hizi kashfa zinaletwa na kitu kimoja, jirani uliyemwita choko, leo umemkaribisha ukamkabidhi nyumba, mke na watoto unadhani ataacha kukudharau?

Ndiyo haya maneno ataanza kusema mimi itabidi niihamishe hii familia kutoka kwenye hii nyumba kwa sababu haina hadhi ya mimi kulala humu, na mengine kibao, ili mradi akushushe thamani kama vile ulivyomshusha kipindi kile unamwita choko.
 
Hali hii ya Chadema kuendelea kuwepo kwenye kajumba hako, ni kufuatia upangaji mbovu wa vipaumbele vyake, hivyo kupelekea matumizi mabovu ya ruzuku, hali iliyopelekea Chadema kukumbwa na ukata siku zote, na kulazikika kuendelea kupanga kwenye kajumba kale pale Uswahili au Uzwazi Ufipa kwenye kabarabara ka uchochoro madimbwi mwamzo mwisho!.
.
Hivyo unavyoviita vipaombele vibovu ndiyo vilivyoifanya CHADEMA kuwa hapo ilipo na ndiyo vilivyomfanya Mh. Lowassa kuja na kuomba ridhaa ya kugombea URAIS kupitia baada ya kukatwa kimizengwe kule CCM.

Nafikiri CHADEMA wamemkaribisha EL si eti aje kuwajengea ofisi na kuwaletea fedha , kinachotakiwa ni UKOMBOZI kwa kweli kwa wananchi wa Tanzania na wameona kumtumia Lowassa malengo yatafikiwa mapema zaidi kuliko ilivyokuwa imekusudiwa.


 
Ina maana Lowasa kakabidhiwa chama sasa, hata kama ana roho nzuri kiasi gani hayo ni matusi makubwa kuwahi kutukanwa chama cha siasa.

Lugha unayotumia umeendelea kutukana, eti hawakua na mpango mzuri wa matumizi ya Ruzuku angalieni nyie wageni wa Chadema msihodhi chama.
 
Hivyo hiyo unavyoviita vipaombele vibovu ndiyo vilivyoifanya CHADEMA kuwa hapo ilipo na ndiyo vilivyomfanya Mh. Lowassa kuja na kuomba ridhaa ya kugombea URAIS kupitia.

Nafikiri CHADEMA wamemkaribisha EL si eti aje kuletea fedha na Majengo mapya, kinachotakiwa ni UKOMBOZI kwa kweli kwa wananchi wa Tanzania na si vinginevyo.

Usipanic hayo aliyoyasema yachunguze Pasco ni mtu wa karibu sana na Lowasa hicho ndicho alichokiona Tajiri mkubwa mwenye majumba mengi yenye hadhi Dar.

Mwl alimkataa Lowasa
 
1. Eti chama kiwe na ofisi ya hadhi ya mtu. . . . . .Sio mtu awe na hadhi ya chama. . . . .!!!!
2. Hii ni akili ya ukombozi hii??!!!
3. Mara oonh mwenyekiti kakiuzia chama magari yaliyotumika
4. Mara katibu mkuu kakopeshwa na chama
5. Sasa tena iwe chama kiko "nyumbani" kwa mtu. . . . . . .
6. Watumie Radio station na TV vya mtu. . . . . .

Eti tunataka kuondoa mkoloni mweusi. . . . . . .!!!!!
Haiwezi kuwa ni njia ya kutafuta uhuru bali ni kuuza uhuru, misingi na miundombinu yake kwa mtu binafsi


Kwa kwa kwa kwa kwaaaa

Hilooo roho zitawauma sana ikiwezekana mmeze chupaaa

Ingekua kwenu si ndo ingekua kicheko??

Acheni wivu wa kike ACT
 
Mkuu hizi kashfa zinaletwa na kitu kimoja, jirani uliyemwita choko, leo umemkaribisha ukamkabidhi nyumba, mke na watoto unadhani ataacha kukudharau?

Ndiyo haya maneno ataanza kusema mimi itabidi niihamishe hii familia kutoka kwenye hii nyumba kwa sababu haina hadhi ya mimi kulala humu, na mengine kibao, ili mradi akushushe thamani kama vile ulivyomshusha kipindi kile unamwita choko.
Nakubali mkuu. Naona jamaa kapewa CHAMA akitumie atakavyo...
 
Mkuu Pasco kama umehifadhiwa na jirani kutokana na dhoruba (mafuriko) na ukafanikiwa kulaza kichwa siku mbili tatu, hupaswi utoe kashfa. Hata kama wataka kumsaidia mhifadhi, basi wasaidia kwa heshima; maana vyote ulivyonavyo sasa havikuweza kukupa hifadhi pale ulipoihitaji. Usianze kusema kwamba aah, nyumba yenyewe hii ya majani, huyu jamaa atakuwa anatumia mshahara wote kwenye pombe - lakini kumbuka hapo ndio umepata hifadhi.

Well said
 
Last edited by a moderator:
Wanabodi,

Kama ilivyo kawaida yetu, wewe kama mwana JF, be the first to know kuwa ujio wa Lawassa kujiunga Chadema, unaandamana na mambo mengi mazuri, moja kubwa ni kuhama kwa Makao Makuu ya Chadema kwenye kijumba cha kupangisha pale Mtaa wa Ufipa Kinondoni Dar es Salaam, hadi kwenye moja ya majumba yenye hadhi inayolingana na Edward Lowassa.

Hali hii ni kufuatia hali iliyojitokeza jana, wakati Edward Lowassa alipofika Makao Makuu ya Chadema, mtaa wa Ufipa, kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia Chadema, kufuatia umati mkubwa wa wafuasi wa Chadema kufurika kwa wingi hali iliyoleta shida na kero mtaa mzima, kutokana na location ya ofisi hizo zilipo, zilionekana ni kama kichochoroni!. Na hapo hao waliojitokeza ni wafuasi tuu wa Chadema, bado tsunami ya wafuasi wa Lowassa hawajatia timu!, wakitia timu kama hali ilivyokuwa uwanja wa Sheikh Amri Abedi, then nyumba zote huo Mtaa wa Ufipa, zinahatari ya kubomolewa kwa makundi ya watu!.

Kumbe ile ofisi ya Makao Makuu ya Chadema pale Ufipa ni nyumba ya kupanga!. Ukipiga hesabu ya jumla ya ruzuku yote ambayo Chadema imeishalipwa, ingetosha sana kujenga jengo la hadhi na mahali penye hadhi, na kama ni kupanga, hakukuwa na sababu kupanga kwenye kijumba kama kile hadi sasa Chadema ni chama kikubwa!. Hali hii ya Chadema kuendelea kuwepo kwenye kajumba hako, ni kufuatia upangaji mbovu wa vipaumbele vyake, hivyo kupelekea matumizi mabovu ya ruzuku, hali iliyopelekea Chadema kukumbwa na ukata siku zote, na kulazikika kuendelea kupanga kwenye kajumba kale pale Uswahili au Uzwazi Ufipa kwenye kabarabara ka uchochoro madimbwi mwamzo mwisho!.

Kufuatia Lowassa kuwa ni tajiri mkubwa, mwenye hadhi ya hali ya juu, huku akimiliki majengo lukuki, yenye hadhi, kwenye maeneo ya maana 'prime areas', ujio wake utapelekea Ofisi za Chadema kuhama uchochoroni, na kuhamia kwenye jengo la maana litakalo endana na hadhi ya Lowassa na tena haswa kwa kuzingatia Chadema ndicho kinakwenda kugeuka Chama tawala!.

Mabadiliko hayo chanya sio tuu kwa Chadema kumiliki jengo lake lenyewe, pia Chadema itamiliki kituo chake cha Redio na Televisheni pamoja na magazeti yake yenyewe, kwa sababu Lawassa hapo alipo tayari anamiliki Redio na TV!, hivyo sasa vitatumiwa na Chadema kwa kuanzia wakati mchakato wa umiliki rasmi wa vyombo vyake yenyewe ukiendelea!.

Ama kweli mgeni njoo, mwenyeji apone!.

Hongera sana Lowassa!.

Hongera Chadema.

Ikulu 2015 ni ya UKAWA!.

Mungu Ibariki Tanzania.

Pasco


Source ya Taarifa hii ni observation yangu binafsi.


Ni nani mtoa leseni wa hivyo Vyombo? Ni Fisadi UKAWA/Lowasa pia?

 
Back
Top Bottom