Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,503
- 113,616
- Thread starter
- #181
Ukipiga hesabu ya jumla ya ruzuku yote ambayo Chadema imekuwa ikipokea, na kulinganisha ruzuku hiyo imefanyia nini, utakubaliana na mimi, kuwa fedha hiyo, ingetosha kabisa kujenga jengo jingine kwenye eneo la kutosha. Hali hii imetokana na upangaji mbovu wa vipaumbele vyake, hali iliyopelekea matumizi mabovu ya ruzuku, kama yalivyofafanuliwa kwenye ripoti ya CAG.
Mabadiliko hayo chanya sio tuu kwa Chadema kumiliki jengo lake lenyewe, pia Chadema itamiliki kituo chake cha Redio na Televisheni pamoja na magazeti yake yenyewe, kwa sababu Lawassa hapo alipo tayari anamiliki by proxy wa familia kubwa ya media, yenye vituo vya Redio, TV na magazeti lukuki!, hivyo sasa pia vitatumiwa kuisupport Chadema kwa kuanzia tuu, wakati mchakato wa umiliki rasmi wa vyombo vyake yenyewe ukiendelea!.
Paskali
NB. Japo Pakali ni mwanachama wa chama cha siasa, na ni kada wa Chama cha Mapinduzi CCM, huyu ni kada mzalendo wa kweli wa taifa hili kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa, kazi yangu ni to tell nothing but the truth, with objectivity, impartiality and balance from all sides!.
Mkuu johnthebaptist, kiukwelihoja yako hii ni hoja ya muhimu sana, Chadema wana tatizo kubwa la kutokuona mbali, myopia, hivyo wanashindwa kupanga vipaumbele vyake. Angalia jambo muhimu kama hili, mimi niliwashauri lini katika uzi huu.Kushindwa kurusha mahojiano ya maalimu Seif pale Clouds tv ni salamu tosha kwa wapinzani kuwa tunakoelekea haitakuwa rahisi tena viongozi wa upinzani kualikwa na vituo vya habari vinavyomilikiwa na wanaccm.
Ikumbukwe pale Clouds media Rostam Aziz aliwahi kufanya uwekezaji wake na hata magazeti yake ya Mtanzania yameacha kuandika propaganda za Chadema baada ya Lowassa kuondoka.
Ni swala la muda tu habari za Mbowe na wapinzani wengine tutazisoma kupitia Tanzania Daima tu na hapa Jf.
Kwanini Chadema hamkuliona hili na kuanzisha luninga yenu kama wale akina Mwamposya na Mwingira?.....ni sehemu ndogo sana ya ruzuku ingefanya kazi hii.
Maendeleo hayana vyama!
P