Elections 2015 Mabadiliko Chanya ya Ujio wa Lowassa: CHADEMA Kuhama Ufipa!, Kuwa Makao Yake, Kituo cha TV na Redio!

Lukansola

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
5,445
1,250
Usipanic hayo aliyoyasema yachunguze Pasco ni mtu wa karibu sana na Lowasa hicho ndicho alichokiona Tajiri mkubwa mwenye majumba mengi yenye hadhi Dar.

Mwl alimkataa Lowasa
Mwalimu amkatae asimkatae kumbuka kuwa lengo ni kuing'oa ccm, jambo linalowatoa kijasho chembamba, pia usisahau Mwalimu alisema upinzani wa kweli utatoka ndani ya ccm, Kwa hiyo usikariri mistari, isome halafu changanya Na zako, ukizingatia wakati
 
Rich Pol

JF-Expert Member
Oct 11, 2013
7,826
2,000
Pasco,
Kama huelewi kitu ni bora kuuliza, we ni mwandishi mkongwe, FYI makao makuu ya CHADEMA si nyumba za kupaga, hizo ni mali za CHAMA toka 2012.

Na pia hakuna mpango wa kuhama, lengo ni kuitoa CCM madaraka si kuwa na HQ ya kifahari
Acha kupotosha umma nyimba hiyo siyo mali ya chadema bali ni nyumba ya Mtei na kitega uchumi chake ambacho chadema wamepanga na wanalipa kodi.
 
Last edited by a moderator:

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
13,584
2,000
Katika sakata hili la Lowassa kuhamia Chadema kuna vitu vya kuzingatia;

1. Mpaka sasa hakuna yeyote anayejadili sera ya kilimo, elimu , afya , miundombinu, uwekezaji , mambo ya nje, ulizi na usalama, michezo na utamaduni, hali ya hewa, nishati na madini, muungano na mambo mengine muhimu kwa taifa.
Hili ni kosa, lakini si kubwa sana kwa vile ilani za uchaguzi hazijaanza kutangazwa.
Hata hivyo, hapa tunajifunza kuwa ratiba ya kuchagua mgombea kabla ya kuwa na ilani sio sahihi. Inafanya mijadala ijikite kwenye personalities rather than real issues.

2. Kila upande unaweza kuathirika au kunufaika na maamuzi ya Lowassa kwenda Chadema kama ifuatavyo;
i) CCM
Faida
a) Kupunguza lawama za kuitwa chama cha mafisadi. Chadema wameshaanza kuondoa neno ufisadi na mafisadi kwenye kauli zao. Kauli yao mpya ni kubadili mfumo. Hata hivyo bado Chadema wana kibarua cha kuelezea wataubadili vipi mfumo kwa sababu mfumo sio chama cha siasa.

b) Kutoa fursa kwa wanasiasa wasio waaminifu kwa chama kukikimbia na kuacha wale walio tayari kukipigania chama. Rafiki wa kweli hujulikana kipindi cha changamoto.

c) Kupata fursa ya kuingiza wimbi kubwa la mamluki ndani ya upinzani kwa kisingizio cha kumfuata Lowassa. Hawa watapewa hero's welcome na kuaminiwa kirahisi.

Hasara
a) Siri zake za maandilizi ya uchaguzi zitafahamika kwa upinzani. CCM italazimika kufanya mabadiliko makubwa kwenye mikakati jambo ambalo litakigharimu chama.

b) Kupoteza baadhi ya watu ambao fundamentally wanaamini Lowassa ndio mtu pekee nchini mwenye uwezo na haki wa kuongoza. Ingawa kundi hili ni la watu wasielewa maana ya chama lakini lipo. Hawa wstamfuata Lowassa kokote anakoenda, wanasema "ulipo, tupo". Mrema alikuwa na watu wapatao 200,000 kwenye kundi kama hili. Lowassa anaclaim kuwa anao milioni moja. Hata hivyo inahitajika utafiti zaidi kuthibitisha idadi hii.

i) Chadema
Faida
a) Kupata mgombea tajiri ambaye ni high profile politician.

b) Kupewa siri za CCM.

c) Kupokea wafuasi wa Lowassa.

d) Kuongeza uhalali wake wa kuwa chama kikuu cha upinzani na kuweza kupata nguvu ya kusikilizwa Zanzibar. Lowassa ana wafuasi Zanzibar ambako Chadema hushindwa kuwa hata nafasi ya tatu kwenye uchaguzi.

Hasara
a) Kujenga sura ya kuthamini umaarufu na pesa kuliko misingi ya Chama.

b) Kukiri de facto kuwa hawakuwa na uwezo wa kuishinda CCM. Hapa watahojiwa je mtu mmoja ndio amewaletea uwezo? Je , kama mtu huyo ana nguvu kubwa kuliko Chama, mtamdhibiti vipi akiwageuka huko mbeleni?

c) Kuwakatisha tamaa wanaojitolea kwa ajili ya Chama. Kitendo cha Slaa kukatwa na kutokusikilizwa kitawafanya watu kama kamanda Mawazo wakae chini na kutafakari kazi wanayojitolea inalenga kubadili nini? Wengi wa wanaojitolea kwa nia njema huongozwa na misingi na itikadi ya Chama. Chama kinapotoka nje ya misingi , kinahatarisha kupoteza au kuwavunja nguvu watu hawa.

d) Kupunguza kuaminiwa na wananchi. Sura iliyojengeka ni kuwa Chadema inacheza tu mchezo wa siasa na hailengi hasa kuboresha maisha ya mtanzania. Mtu yeyote anayewapa pesa za uchaguzi watamtukuza ilimradi tu washinde. Kauli hizi za Mbowe hazijapokelewa vizuri na watanzania.

e) Kutumia nguvu kubwa kusambaza ujumbe mpya. Siku zote inafahamika ujumbe wa chadema ni kupinga mafisadi. Sasa kuna mabadiliko, tatizo sio mafisadi ila mfumo. Hii itahitaji resources nyingi kuwaeleza watu mpaka waikubali. Kwahiyo muda wa kuzungumzia masuala mengine ya maisha ya kila siku utakuwa mdogo kuliko wa kufafanua mabadiliko haya ya msimamo. Hii inaatarisha Chadema kuonekana Chama kinachotafuta madaraka bila kuwa na mkakati wa kuongoza nchi na kuboresha maisha.

f) Iwapo Chama hakitashinda uchaguzi kitakosa misingi ya kukiendeleza. Kitabaki kuonekana chama cha wajanjawajanja. Watu wa Lowassa ambao wameahidiwa vyeo serikalini itabidi watake vyeo kwenye Chama. Chama kitachukuliwa na watu wasiokijua wala kukijali kwa dhati.

3. Pamoja na kwamba watu hudhani siasa ni mchezo, lakini siasa ni taaluma. Katika haya yanayoendelea, mwenye taaluma zaidi ndiye atayejipatia faida zaidi kuliko hasara.

4. Sisi kama watanzania tunachotakiwa kuomba ni Mungu aendelee kuilinda nchi yetu iwe na amani na umoja kama taifa.
 
logician mkuu

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
795
0

Faida kubwa ni kumega CCM na kuweka vema systems za checks and balances

CCM imekuwa inashinda kirahisi sana chaguzi na kuwa na uwakilishi mkubwa bungeni zaidi ya 80%. Matokeo yake ni kukumbatia maslahi ya chama na kupuuza wananchi waliowapa ridhaa.

CCM wametaharuki kwa kuwa wanaona ukiritimba huu waelekea ukingoni. Tamaa yao ni kubaki madarakani hata kwa GOLI LA MKONO! Hilo linaonekana kuwa gumu kwa sasa. Uwezekano wa 80% bungeni ni Mdogo sana.

Hilo ni zuri kwa nchi. Tutaanza kuwa na bunge ambalo mambo hujadiliwa na kuamuliwa kwa hoja na si kwa kelele za NDIYOOOO
 
mwekundu

JF-Expert Member
Mar 4, 2013
21,670
2,000
Lowasa is a political liability not an asset mark my word MUDA utatuambia kuna chama hapa kinapoteza misingi yake na kingine kinajiimarisha
 
Susuviri

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
3,713
2,000
Lowasa is a political liability not an asset mark my word MUDA utatuambia kuna chama hapa kinapoteza misingi yake na kingine kinajiimarisha
Lingine ni kuwa asilimia 60 ya wapiga kura hawana chama na mpk sasa tunachosikia kutoka kwa Chadema ni "Tunaingia Ikulu" .. Imadhihirika na mgombea wamemchukua juzi tu na kumpa nafasi ya kuwania urais kwa kigezo hicho tu, huku wakibaki kumtukana Dr Slaa aliyewaletea kura za CCM na indepents kibao mwaka 2010!
Sasa CDM imebaki bila sera, mtazamo au dira - just "tunaingia ikulu"
 
Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,387
2,000
Ukitathmini hizi faida na hasara kwa kila pande, CHADEMA ndo wanaonekana kuthirika zaidi kuliko kunufaika
Inawezekana ndiyo au hapana.Muda ni dawa.Lakini nina uhakika wa upinzani kupata viti vingi bungeni.Ila kataa kubali Ununuaji wa uongozi si Lowassa pekee ona wabunge wenu wengi wanaotoa rushwa ili wapate ubunge.

Wakiingia bungeni watarudishaje pesa zao?

Tunaangalia mahali pamoja tumeshindwa kuangalia sehemu nyingine.Hatuhitaji viongozi wanaonunua madaraka.

Ya Lowassa kutoingia Ikulu wala haitaniuma.Mkakati unatakiwa kuhakikish wabunge wanaingia wengi bungeni.

Na hiyo ndiyo aim ya CDM..Msikilize vyema Lissu.Hajakataa kama Lowassa hana kashfa amesema wanajua ni mchafy period
 
Krama

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
272
195
Faida kubwa ni kumega CCM na kuweka vema systems za checks and balances

CCM imekuwa inashinda kirahisi sana chaguzi na kuwa na uwakilishi mkubwa bungeni zaidi ya 80%. Matokeo yake ni kukumbatia maslahi ya chama na kupuuza wananchi waliowapa ridhaa.

CCM wametaharuki kwa kuwa wanaona ukiritimba huu waelekea ukingoni. Tamaa yao ni kubaki madarakani hata kwa GOLI LA MKONO! Hilo linaonekana kuwa gumu kwa sasa. Uwezekano wa 80% bungeni ni Mdogo sana.

Hilo ni zuri kwa nchi. Tutaanza kuwa na bunge ambalo mambo hujadiliwa na kuamuliwa kwa hoja na si kwa kelele za NDIYOOOO
hizi ndio logic tunazozitaka hapa.. hapa kati ya mbowe na Lowassa kuna mutual benefits, Mbowe anataka chama chake na UKAWA kwa jumla waingize wabunge wengi mjengoni kuliko CCM, na Lowasa anataka kutimiza azma yake ya kuingia Ikulu, japokuwa kwa akili ya kawaida mr EL ana wakati mgumu kidogo ila kwenye ubunge im million percent sure that UKAWA wataingiza zaidi ya nusu ya wabunge kule mjengoni
 
Ronal Reagan

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,843
2,000
Katika sakata hili la Lowassa kuhamia Chadema kuna vitu vya kuzingatia;

1. Mpaka sasa hakuna yeyote anayejadili sera ya kilimo, elimu , afya , miundombinu, uwekezaji , mambo ya nje, ulizi na usalama, michezo na utamaduni, hali ya hewa, nishati na madini, muungano na mambo mengine muhimu kwa taifa.
Hili ni kosa, lakini si kubwa sana kwa vile ilani za uchaguzi hazijaanza kutangazwa.
Hata hivyo, hapa tunajifunza kuwa ratiba ya kuchagua mgombea kabla ya kuwa na ilani sio sahihi. Inafanya mijadala ijikite kwenye personalities rather than real issues.

2. Kila upande unaweza kuathirika au kunufaika na maamuzi ya Lowassa kwenda Chadema kama ifuatavyo;
i) CCM
Faida
a) Kupunguza lawama za kuitwa chama cha mafisadi. Chadema wameshaanza kuondoa neno ufisadi na mafisadi kwenye kauli zao. Kauli yao mpya ni kubadili mfumo. Hata hivyo bado Chadema wana kibarua cha kuelezea wataubadili vipi mfumo kwa sababu mfumo sio chama cha siasa.

b) Kutoa fursa kwa wanasiasa wasio waaminifu kwa chama kukikimbia na kuacha wale walio tayari kukipigania chama. Rafiki wa kweli hujulikana kipindi cha changamoto.

c) Kupata fursa ya kuingiza wimbi kubwa la mamluki ndani ya upinzani kwa kisingizio cha kumfuata Lowassa. Hawa watapewa hero's welcome na kuaminiwa kirahisi.

Hasara
a) Siri zake za maandilizi ya uchaguzi zitafahamika kwa upinzani. CCM italazimika kufanya mabadiliko makubwa kwenye mikakati jambo ambalo litakigharimu chama.

b) Kupoteza baadhi ya watu ambao fundamentally wanaamini Lowassa ndio mtu pekee nchini mwenye uwezo na haki wa kuongoza. Ingawa kundi hili ni la watu wasielewa maana ya chama lakini lipo. Hawa wstamfuata Lowassa kokote anakoenda, wanasema "ulipo, tupo". Mrema alikuwa na watu wapatao 200,000 kwenye kundi kama hili. Lowassa anaclaim kuwa anao milioni moja. Hata hivyo inahitajika utafiti zaidi kuthibitisha idadi hii.

i) Chadema
Faida
a) Kupata mgombea tajiri ambaye ni high profile politician.

b) Kupewa siri za CCM.

c) Kupokea wafuasi wa Lowassa.

d) Kuongeza uhalali wake wa kuwa chama kikuu cha upinzani na kuweza kupata nguvu ya kusikilizwa Zanzibar. Lowassa ana wafuasi Zanzibar ambako Chadema hushindwa kuwa hata nafasi ya tatu kwenye uchaguzi.

Hasara
a) Kujenga sura ya kuthamini umaarufu na pesa kuliko misingi ya Chama.

b) Kukiri de facto kuwa hawakuwa na uwezo wa kuishinda CCM. Hapa watahojiwa je mtu mmoja ndio amewaletea uwezo? Je , kama mtu huyo ana nguvu kubwa kuliko Chama, mtamdhibiti vipi akiwageuka huko mbeleni?

c) Kuwakatisha tamaa wanaojitolea kwa ajili ya Chama. Kitendo cha Slaa kukatwa na kutokusikilizwa kitawafanya watu kama kamanda Mawazo wakae chini na kutafakari kazi wanayojitolea inalenga kubadili nini? Wengi wa wanaojitolea kwa nia njema huongozwa na misingi na itikadi ya Chama. Chama kinapotoka nje ya misingi , kinahatarisha kupoteza au kuwavunja nguvu watu hawa.

d) Kupunguza kuaminiwa na wananchi. Sura iliyojengeka ni kuwa Chadema inacheza tu mchezo wa siasa na hailengi hasa kuboresha maisha ya mtanzania. Mtu yeyote anayewapa pesa za uchaguzi watamtukuza ilimradi tu washinde. Kauli hizi za Mbowe hazijapokelewa vizuri na watanzania.

e) Kutumia nguvu kubwa kusambaza ujumbe mpya. Siku zote inafahamika ujumbe wa chadema ni kupinga mafisadi. Sasa kuna mabadiliko, tatizo sio mafisadi ila mfumo. Hii itahitaji resources nyingi kuwaeleza watu mpaka waikubali. Kwahiyo muda wa kuzungumzia masuala mengine ya maisha ya kila siku utakuwa mdogo kuliko wa kufafanua mabadiliko haya ya msimamo. Hii inaatarisha Chadema kuonekana Chama kinachotafuta madaraka bila kuwa na mkakati wa kuongoza nchi na kuboresha maisha.

f) Iwapo Chama hakitashinda uchaguzi kitakosa misingi ya kukiendeleza. Kitabaki kuonekana chama cha wajanjawajanja. Watu wa Lowassa ambao wameahidiwa vyeo serikalini itabidi watake vyeo kwenye Chama. Chama kitachukuliwa na watu wasiokijua wala kukijali kwa dhati.

3. Pamoja na kwamba watu hudhani siasa ni mchezo, lakini siasa ni taaluma. Katika haya yanayoendelea, mwenye taaluma zaidi ndiye atayejipatia faida zaidi kuliko hasara.

4. Sisi kama watanzania tunachotakiwa kuomba ni Mungu aendelee kuilinda nchi yetu iwe na amani na umoja kama taifa.
Hongera ZeMarcopolo, uchambuzi mzuri.
Hili la Lowassa limebadili landscape ya siasa yetu kwa muda mfupi na muda mrefu. Hakuna aliyeliona miezi 12 iliyopita.
 
fredericko

JF-Expert Member
Apr 27, 2014
2,266
2,000
Mara nyingi wanasiasa na watu mbali mbali wamekua wakitumia kauli hii, eti 'ikulu ni mahali patakatifu'.
Sasa huyo aliyetoa kauli hii, Mwl Nyerere, yeye mwenyewe si mtakatifu, patakatifu ni mbinguni tu. Ukisema ikulu ni mahali patakatifu, utampata wapi mtakatifu awe rais ili aweze kuingia humo?
 
Madela Wa- Madilu

JF-Expert Member
Mar 24, 2007
3,070
1,195
Watu wanatamani sana IKULU wako tayari kuingia kwa gharama yeyote.
Kwa sababu wanajua ukisha tinga Ikulu basi MIFEDHA yote ni yako na makosa yako yote unalazimika kusamehewa.
Hili goli la kisigino kwamba Lowassa alitemwa kwa sababu ni Msafi na mwenye Dira na Magufuri alichaguliwa kwa sababu ni Pro Mafisadi?!!
Hivi Magufuli na Lowassa nani fisadi???
Kwenye ile list of Shame katolewa lini???

Inanionyesha wazi jinsi Watanzania tulivyo na short Memory hasa lupia ikipenyezwa kwenye mianya yetu.
Huo wimbo wenu wa Lowassa imbeni hata beti 10 mimi simo na kadi ya chadema sirudishi.

Tangu AICC mpaka Uwaziri mkuu ni shida tupu?

Mwili wa upinzani umekwisha wekwa kwenye jeneza harakati za kufunika jeneza zinaendelea punde kidogo tu upinzani utaanza na neno Marehemu.(Nina maana upinzani umekwisha kufa hapa tunachagua tarehe ya kuzikwa tu)

Doo!
 
MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,039
2,000
Ni katika mazingira ya kawaida bila hata kuumiza Kichwa LOWASSA anaenda kushinda kiti cha Urais kwa sababu hizi;
1.Anao mtaji mkubwa sana wa wapiga kura ambao ni watanzania wa kawaida mfano wa machinga, mamantilie, bodaboda.
2.Viongozi wa madhehebu yote ya dini nchini kutokana na ushirikiano anaowapa wa hali Mali.
3.Wanafunzi wengi kutoka vyuo vikuu vyote nchi kutokana na kuamini ile dhana yake ya kusema Ukosefu wa ajira ni bomu linalosubiri kulipuka,Kwahiyo wanaamini akiwa Rais ana uwezo wa kabiliana na hali hiyo.
4.Kura zote za wanachama wa vyama vinavyounda UKAWA zitaelekea kwake.
5.Wanachama wa CCM waliokua wakimuunga mkono wakati akiwa huko ambao watapiga kura ya kumchagua hata kama watabakia huko huko bila kuhama, hii itafanyika kutokana baadhi yao kuonekekana kua na hasira baada ya swahiba wao kutoswa ili kuiadhibu CCM kama walivyofanya kwa Membe maana mpaka sasa mtaani kuna wapo wanaosema liwalo na liwe hawahami CCM lakini kura ni kwa LOAWASSA.
 
clemence

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
594
195
Wanachokifanya wafuasi wa CCM ni kama vile mtu kuachwa na mpeziwe halafu akaanza kuona wivu baada ya mpeziwe huyo kuchukuliwa na mwingine,kuonyesha anaumia maneno maneno juu ya mpenzi wake huyo wa zamani hayataisha kila akikutana na mtu basi atamwongelea tu kwa kupenda ama anajikuta ameshamuongelea, hiyo ni kuonyesha wuvu na udhaifu mkubwa. Mi ningewashauri CCM wasimuongelee lowassa sana maana inaonyesha kuwa wameumia kuondoka kwake na zaidi kuuaminisha uma kuwa kweli lowassa alikuwa kiungo muhimu ndani ya CCM.
 
Top Bottom