Ndugu yangu zomba,Kwani Bibilia ina watu fulani wa kuitumia? Na sio kwa watu na Mataifa yote?
nipo tayari kushiriki uanndishi wa kitabu chenye hii title kwa historia ya vizazi vijavyo,
- ukiona viongozi wa taifa wanaanza ku-quote biblia badala ya katiba ya jamhuri, katika kuhalalisha vitendo vya serikali maana yake ni moja tu kwamba hao viongozi na serikali nzima ni mufilisi, wanahitaji kuondolewa mara moja!
william.
Ndo hayo Maaskofu wanakukatazeni !!!kwa akili ndogo uliyo nayo kujua watu wa mataifa kwa biblical context wewe huwezi elewa!! waingereza wanasema hivi'' no research no right to speak mimi naongeza no right to comment''you cannot be an authority to everything when it comes to intelectual thinking be it science or religious!!! nimesoma majibu yako kuhusu malipo ya DOWANS ulionekana kujibu kila hoja mimi nikafikiri wewe ni lawyer tena aliye specialize ktk international businnes leo hii unataka kuwa theologist yaani unaweza kujibu Maaskofu kwa kutumia Biblia,I think that is pathetic you cannot know it all!! Makamba type!!! Maneno mengi akili kidogo , tafakari kabla ujasema na jiulize je do I have enough knowledge on the subject matter at hand, If not keep your mouth shut!! there is no harm!! and your will have done a great service to you as a person and your readers . It is simply some piece of advice that is if your brain is still intact.
Sorry if I offended you.
Maaskofu wa madhehebu ya Kikristu mkoani Arusha wamemkemea Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba, kwa kuitumia Biblia takatifu kuhalalisha uovu; wakamtaka aache tabia hiyo mara moja.
Maaskofu hao wakiongozwa na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Thomas Laizer, aliyezungumza kwa niaba wenzake katika mazishi ya wahanga wa maandamano ya Arusha, alisisitiza kwamba wataendelea kuikosoa serikali na chama chochote kile pindi kinapokosea.
Kauli ya Makamba iliyowakera maaskofu hao, na ambayo amekuwa akiirudia mara kwa mara, ni ile aliyotumia kuwakejeli kwa kunukuu maandiko matakatifu ya Kurani na Biblia akisema tiini mamlaka iliyo kuu. Walisema ufahamu wa Makamba ni finyu katika kutafsiri maana halisi ya neno hilo.
Kama serikali wameamua kutuvunjia heshima, basi wasimame kwenye majukwaaa kutetea uovu wao, na sisi tutasimama kwa ajili ya kupinga uovu wao, tuone Mungu atamsikia nani alisema Askofu Laizer.
''Maaskofu wamesikitishwa na kauli yake na pia kauli ya Katibu wa CCM mkoa wa Arusha, Mary Chatanda kuwataka kuvua majoho na kuingia katika siasa kwani ni kuwavunjia heshima,'' alisema askofu Laizer.
Source: Tanzania Daima
Ukweli n kwamba Biblia ni kitabu cha wote. Lakini "wote" hapa ina maana kuwa kinasema na kila mtu, sio kwamba kila mtu ana uwezo wa kuifafanua. Hata sheria za nchi ni kwa ajili ya wananchi wote, lakini sio wote wenye mamlaka ya kutafsiri sheria ila mahakama. Kufasiri Biblia ni taaluma kubwa inayosomewa, somo la kufasiri Biblia huitwa "HERMENEUTICS." Na watu hupata hata Phd kwa hilo. Sasa Makamba amesoma wapi theolojia? Kwa taarifa yako wanatheolojia humnyamazia tu, lakini hufanya makosa mengi katika kutafsiri kwake, mojawapo ni hilo andiko lililonukuliwa.