Maaskovu Vs. Makamba na mgongano wa Arusha

kwani bibilia ina watu fulani wa kuitumia? Na sio kwa watu na mataifa yote?

kuwa muelewa. Tatizo lako wewe ni mbumbumbu. Wanasema asiitumie kwa kuhalalisha maovu na kuhadaa watu. Watu wanasom zaidi ya miaka 7 kuitafsiri hiyo. Kasomea wapi?
 
lkn mzee hii maada sio ya udini? Au kwa sababu inawafurahisha chadema? Askofu nani? Ni mwanasiasa. Mchumi au? Acha jazba

mjitahidi kuwa wadadisi wa mambo b4 kukurupuka hata kama kaudini kanawapush kwa ndani. Kikatiba na hata decralation ya un ya haki za binadamu na tz akiwa mwanachama wake inataka mtu atambuliwe kama mtu kwanza kabla ya sheria au kitu chochote. Askofu ni mtanzania na hupiga kura kama mtanzania mwingine. Hulipia bill ya umeme na maji zikiwemo kodi zake zote. Hununua sukari na mchele kama wewe. Ana haki ya kuhoji chochote kile ili mradi havunji sheria za nchi. Au sheikh yhy tu ndo ahoji?
 
Unajua maaskofu na mapadre vile vile wana TAALUMA kwani wengine ni Madokta(MD), wamesomea sheria(sio sharia), political sc, saikolojia, etc, kwa hiyo kinapotokea Tatizo linalohusu taaluma yake ikipindishwa ama yeye kuwa na upeo hii inafanya mtu aweze kutetea na kuwa mkali ili nafsi isije kumsuta
 
- Ukiona mwenye akili kama wewe anatumia muda wake kumjibu asiye na aikili kama mimi, Ina maana kwamba ujumbe umefika ahsante sana mkuu kwa kukubali ujumbe, kwamba ukiona viongozi wa taifa wanatumia Biblia, badala ya Katiba kuhalalisha vitendo vya serikali, basi ujue viongozi hao na serikali nzima ni mufilisi, na wanahitaji kuondoka madarakani mara moja!

- Naona message sent, delivered! & Received, tumekusikia mkuu!


William

Ukiwaona the so called great thinkers, hawaoni tatizo la viongozi wa dini kuingilia mambo ya siasa na kutugawa watanzania basi ujue tunakokwenda siko. Yaani GT can not think beyond udini....Hawa viongozi wa dini wameshakosea mara ngapi ? Sasa wakiambiwa ukweli wafuasi mnakua wakali, ndio maana waliwaambia Kikwete ni chaguo la mungu...
 
kuwa muelewa. Tatizo lako wewe ni mbumbumbu. Wanasema asiitumie kwa kuhalalisha maovu na kuhadaa watu. Watu wanasom zaidi ya miaka 7 kuitafsiri hiyo. Kasomea wapi?
Siasa za tanzania, tangu kikwete alipotulisha unga wa ndele basi watanzania wote
Hatusikii hatuewi, dini kwenye kampeni za 2010, zilikuwa propaganda , ilikuwa kama mtaji wa Ccm, ila kwa sa7a itak0wa kiboko kwao
 
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Arusha, Thomas Laizer amesema Katibu wa CCM, Yusuph Makamba ana uelewa finyu wa Biblia.

Akizungumza katika ibada ya kuwaaga watu wawili waliofariki dunia kwa kupigwa risasi na polisi Uwanja wa NMC jana, Askofu Laizer alisema tafsiri ya Makamba toka katika biblia ya kuwataka viongozi wa dini kuheshimu mamlaka ya viongozi waliopo madarakani, inapotosha.

"Miaka yote viongozi wa dini wamekuwa ni washauri wa Serikali hivyo Makamba kutumia Biblia kutaka kuwafumba midomo ni jambo lisilowekezana na ana uelewa finyu wa Biblia,"alisema Askofu Laizer.

Alisema maaskofu wamesikitishwa na kauli yake na pia kauli ya Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda kuwataka wavue majoho na kuingia katika siasa kwani huku ni kuwavunjia heshima.

Askofu Laizer alisema migogoro ya kisiasa Arusha, imeanza siku nyingi tangu katika mchakato wa kura za maoni ya ndani ya CCM katika nafasi za ubunge na udiwani.

"Hapa kuna migogoro, haijaanza leo, imeanzia CCM wamegawanyika na ikaendelea katika wakati wa kutangaza ushindi wa mbunge na sasa kupata Meya wa Jiji la Arusha,"alisema Laizer.

Askofu Laizer alisema anaamini mgogoro huo utamalizika katika kufutwa kwa matokeo ya meya na kurudiwa upya kwa uchaguzi huo na maaskofu hawana tatizo na mgombea aliyeshinda kihalali
 
- Ukiona viongozi wa taifa wanaanza ku-quote Biblia badala ya Katiba ya Jamhuri, katika kuhalalisha vitendo vya serikali maana yake ni moja tu kwamba hao viongozi na serikali nzima ni mufilisi, wanahitaji kuondolewa mara moja!

William.

great one.thx
 
kikwete.jpg

mod huu sio udini?
 
Ukiwaona the so called great thinkers, hawaoni tatizo la viongozi wa dini kuingilia mambo ya siasa na kutugawa watanzania basi ujue tunakokwenda siko. Yaani GT can not think beyond udini....Hawa viongozi wa dini wameshakosea mara ngapi ? Sasa wakiambiwa ukweli wafuasi mnakua wakali, ndio maana waliwaambia Kikwete ni chaguo la mungu...

Hao ni wenye upeo mdogo wanafikiri kuchonganisha watu kutoka na imani zao za kidini
 
- Ukiona mwenye akili kama wewe anatumia muda wake kumjibu asiye na aikili kama mimi, Ina maana kwamba ujumbe umefika ahsante sana mkuu kwa kukubali ujumbe, kwamba ukiona viongozi wa taifa wanatumia Biblia, badala ya Katiba kuhalalisha vitendo vya serikali, basi ujue viongozi hao na serikali nzima ni mufilisi, na wanahitaji kuondoka madarakani mara moja!

- Naona message sent, delivered! & Received, tumekusikia mkuu!

William

Unaonekana kale kasprit ka Utanganyika hakajakatika hata baada ya kupigwa chini 1995 mdingi wa Mtera huku akijiita Jumanne.

Karibu sana William maana kama wamekukataa huko inaonesha wewe hauko kimaghumashi.
 
Wakati mwingine kama hatuna comments kuhusiana na post iliyotolewa ni busara zaidi kutochangia naona wachangiaji wengi kwenye hii mada hawakuitendea haki.
 
makamba ni mjinga sana na hana akili yule mzee

Sana kabisa..sasa sielewi kwanini watu wazima na akili zao wamsikize whether ana-quote Biblia au kitabu chochote kile..Huyu mzee alitakiwa asipewe platform yeyote kwene vichwa vya watu wenye akili timamu. Kumjadili ni kumpaisha wakati si lolote si chochote.
 
Hao maaskofu ndio waliopotosha watanzania kwa kutumia biblia bale walipowambia watanzania Kikwete ni chaguo la mungu!!
 
Maaskofu wa madhehebu ya Kikristu mkoani Arusha wamemkemea Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba, kwa kuitumia Biblia takatifu kuhalalisha uovu; wakamtaka aache tabia hiyo mara moja.

Maaskofu hao wakiongozwa na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Thomas Laizer, aliyezungumza kwa niaba wenzake katika mazishi ya wahanga wa maandamano ya Arusha, alisisitiza kwamba wataendelea “kuikosoa serikali na chama chochote kile pindi kinapokosea.”

Kauli ya Makamba iliyowakera maaskofu hao, na ambayo amekuwa akiirudia mara kwa mara, ni ile aliyotumia kuwakejeli kwa kunukuu maandiko matakatifu ya Kurani na Biblia akisema “tiini mamlaka iliyo kuu.” Walisema ufahamu wa Makamba ni finyu katika kutafsiri maana halisi ya neno hilo.

“Kama serikali wameamua kutuvunjia heshima, basi wasimame kwenye majukwaaa kutetea uovu wao, na sisi tutasimama kwa ajili ya kupinga uovu wao, tuone Mungu atamsikia nani” alisema Askofu Laizer.

''Maaskofu wamesikitishwa na kauli yake na pia kauli ya Katibu wa CCM mkoa wa Arusha, Mary Chatanda kuwataka kuvua majoho na kuingia katika siasa kwani ni kuwavunjia heshima,'' alisema askofu Laizer.

Source: Tanzania Daima


Huyu jamaa ni anti-Christ wa hali ya juu,sijawahi sikia akikashifu mashehe
 
samahani alikuwepo kiongozi wa kiislam ktk mazishi hayo alietoa hotuba?

Walikuwepo kama watano:1) Ustaadh Allawi-Aliyesoma Du'a
2)Sheikh Abdallah-Aliyetoa wosia
3)Wengine siwakumbuki majina ila wao hawakuongea
 
Back
Top Bottom