Waziri wa mambo ya ndani E. Nchimbi amefika Jangwani kuongea na waandishi wa habari walioandamana kwa ajili ya kifo cha Mwangosi lakini amezomewa vibaya, na walipoulizwa waandishi ni wangapi wanataka awahutubie wote wamemkataa, ikabidi aondoke kwa aibu kubwa.
Nchimbi kafukuzwa kwa aibu na waandishi wahabari wanasema yeye kaja kuwapokea kama nani wakati hawajamwalika
- yeye amegoma kuondoka, sasa hapa fujo tu angalieni channel 10 laivu
Mabango yaanasema
"camera ya mwangosi ipo wapi"
"kamuhanda ni muuaji, kaua songea kaua iringa"
Nchimbia anaondoka.. Anawabeza kutokana na walivyomzomea laivu channel 10
Naskia baadhi ya mikoa yamepigwa marufuku
Huyu hapa wakati anaingia uwanjani
Hapa akiwa tayari katimuliwa anaondoka kwa aibu kichwa chini
Tunaomba mwenye access na maandamano ya wanahabari yanayoendelea hivisasa jijini Dar-es-Salaam watupe updates.
Waziri wa habari amefika Jangwani kuongea na waandishi wa habari walioandamana kwa ajili ya kifo cha Mwangosi lakini amezomewa vibaya, na walipoulizwa waandishi ni wangapi wanataka awahutubie wote wamemkataa, ikabidi aondoke kwa aibu kubwa.
Hongereni sana ila angalieni jamaa wapo mbele wanawasubiria. Mtakula kichapo hadi mkome ubishi.