Jamani kwa sasa ushabiki unaohusu imani za watu tusiufanye, 7bu mambo haya kwetu ni mageni, lakini ndo yaliyoleta shida huko Nigeria, Sudan, Rwanda, Kenya (Mombasa), Uganda, na kwingineko. Dalili zote za kujitokeza hapa kwetu zimeshaanza kiasi kwamba hata kama sisi tutayaepuka, wanetu yatawatesa sana.
Ndo sababu ukifuatilia katika nchi hizo zote inasadikiwa kwamba vyombo vya mawasiliano vilisaidia kueneza chuki hasa radio nyingi zilifungiwa. Tusiwaumize zaidi wale wote wanaohisi kuonewa kupitia imani zao tukajenga uadui wa kudumu. Tanzania ni moja na watanzania hatuna budi kubakia wamoja forever!
Mi sioni shida kuishi na watu wenye imani tofauti na mimi na wala sipendi kujadili juu ya dini ya mtu kwa sababu huenda kama nami ningezaliwana wa imani ile ningekuwa kule. Ebu tufikiri zaidi juu ya neno IMANI ni nini?
Na uenda ni imani tu ndo zinatutofautisha lakini Mungu na Mitume wake ni wale wale labda tofauti zilitokana na Lugha za makabila ya kipindi kile mfano matamshi ya Kiswahili na Kingereza ni tofauti ndo maana ukifuatilia hizi dini zinaamini kwamba eti:-
YESU ndiye ISSA
JOSEPH ndiye YUSUF
ABRAHAM ndiye IBRAHIM, (2mention a few)
Tusijiingize kwenye vita, bila kukumbuka kwamba Historia inatuambia kwamba dini zilienezwa na Wamisionari ili iwe rahisi kututawala. Hapo sina uhakika kama ni kweli, maana watu wanaweza kuhisi mi Mpagani, lakini nami nina imani tena kali sana kwenye mojawapo kati ya hizo mbili kuu na ninaamini kabisa kuwa YESU KRISTU NI MFALME, NI MFALME WETU KWELI, NI MFALME MILELE.