Maandamano ya UKUTA yasipofanyika...

Maandamano ya UKUTA yasipofanyika...

Kama UKUTA wakinywea na mwishowe kutokufanya hayo maandamano yao ambayo wamepanga kuyafanya hiyo tarehe 1 mwezi ujao, basi mheshimiwa MWENYE ENZI, MTUKUFU rais Magufuli atakuwa amepata ushindi mkubwa sana.

Hayo maandamano yasipotokea atakuwa kafanikiwa kuwatisha wananchi katika kutofanya yale ambayo hayampendezi yeye.

Na huu ndo utakuwa mwanzo tu. Huko mbeleni ikitokea kuna jambo ambalo halimpendezi yeye binafsi basi hatosita kutumia vyombo vya dola kuwatisha watu ili waache kufanya walichokuwa wamepanga kufanya.

Hiyo ndo Tanzania mpya. Tanzania ya MWENYE ENZI, Mtukufu rais John Pombe Joseph Magufuli [nahisi pia tutalazimishwa kuyatumia majina yake yote manne la sivyo wataokiuka watatafutwa na kuadhibiwa, hata kama wapo mitandaoni].

Na nyie wachora vikatuni nahisi dawa yenu inakorogwa huko maabara. Kama mkiendelea kumchora vibaya MWENYE ENZI, MTUKUFU rais John Pombe Joseph Magufuli basi siku zenu zinahesabika.

Yakiwatokea ya kutokea msije lalama eti sikuwaambia! Shauri yenu.

Jamaa washaufyata Mkia hahahahah
 
Hicho cha mtema kuni kikiwa ndani ya katiba hata hakimtishi mtu lakini kikitekelezwa kinyume na utaratibu sio cha kufurahia. Watu wengi hapo kabla waliamini kuwa kutumia siasa wangeliweza kuachieve walichotaka lakini kwa hivyo vi-'mtema kuni' uenda kukatokea ideology mpya za watu kufikiri ni jinsi gani ya kufanya kazi chini ya vitisho badala ya katiba. Tuombee Mungu tusifike huko maana aina hii ya fikira ni sawa na nyoka wa sumu ambaye anadhuru kiumbe bila hata kujishibisha!
Sijamalizia kusoma utumbo wako, ila katiba ya nchi yeyote hairuhusu kufanya maandamano yasiyo na kikomo. Hasa maandamano ya kutaka kupindua nchi. Hata USA waliwahi kutaka kuandamana kumtoa Obama, ila wewe uliona walichofanywa hao waandamanaji, walipigwa sana. Same hata kwa Tz lazima mgepigwa sana maana katiba hairuhusu.
 
Hebu cheki huko kwingine jinsi watu wasivyowaogopa polisi.

Mtu zinaingia kitaa kuzipiga na polisi.

Watanzania tunayaweza haya?

Tunaomba utuwekee qualifications za hao wanaomwaga washa washa hapo tulinganishe!
 
Hebu cheki huko kwingine jinsi watu wasivyowaogopa polisi.

Mtu zinaingia kitaa kuzipiga na polisi.

Watanzania tunayaweza haya?

mkuu.....hao polisi mbona wastaarabu sana

Hapo zingeshatumika Shaba...huwezi kuwasogelea kihivo huku Bongo....Kwa Bongo wewe mtu unapigwa tu kama swala anavyowindwa
 
Hata USA waliwahi kutaka kuandamana kumtoa Obama, ila wewe uliona walichofanywa hao waandamanaji, walipigwa sana. Same hata kwa Tz lazima mgepigwa sana maana katiba hairuhusu.

Hmm...wewe lini hiyo?

Lini watu waliandamana ili kumtoa Obama na wakapigwa sana?

Naomba niwekee vyanzo, tafadhali.
 
Sijamalizia kusoma utumbo wako, ila katiba ya nchi yeyote hairuhusu kufanya maandamano yasiyo na kikomo. Hasa maandamano ya kutaka kupindua nchi. Hata USA waliwahi kutaka kuandamana kumtoa Obama, ila wewe uliona walichofanywa hao waandamanaji, walipigwa sana. Same hata kwa Tz lazima mgepigwa sana maana katiba hairuhusu.
Sijui mimi ni mjinga kiasi gani lakini mtu yeyote akiongelea mambo ya Tanzania alafu akatoa mfano wa USA daima namfananisha na wale jamaa wanaosemaga eti "hata Bakhresa alianzia kwenye kushona viatu...". Endelea bwana nisikuvunje moyo!
 
Nimenunua mask, nimenunua buti mpyaa nimechoka na vijimsemo watanzania n9 waoga wa mabomu, ninayo experience yaliyo tokea soweto Arusha na mimi nilikuwa miongoni wa walio nusurika, iwe mvua iwe jua Mimi binafsi lazima nishiriki maandamano, now nipo Arusha na tumejipanga vya kutosha, hatuta leta vurugu, tutakuwa na vitambaa vyeupe kumaanisha maandamano ni ya amani, pia hatuta pita mainroad tutatumia service road ili kuepuka msongamano.

Mtakuwa mnazungusha mikono pia??
 
Hebu cheki huko kwingine jinsi watu wasivyowaogopa polisi.

Mtu zinaingia kitaa kuzipiga na polisi.

Watanzania tunayaweza haya?

Kwa hiyo unataka kuona Ukuta wakipigana na polisi
Hebu cheki huko kwingine jinsi watu wasivyowaogopa polisi.

Mtu zinaingia kitaa kuzipiga na polisi.

Watanzania tunayaweza haya?

[/QUOTE Ni kwa vile kuna camera na vyombo vya habari,polisi wa China wanatoa kichapo Cha mbwa ka hamna camera.
 
Kama UKUTA wakinywea na mwishowe kutokufanya hayo maandamano yao ambayo wamepanga kuyafanya hiyo tarehe 1 mwezi ujao, basi mheshimiwa MWENYE ENZI, MTUKUFU rais Magufuli atakuwa amepata ushindi mkubwa sana.

Hayo maandamano yasipotokea atakuwa kafanikiwa kuwatisha wananchi katika kutofanya yale ambayo hayampendezi yeye.

Na huu ndo utakuwa mwanzo tu. Huko mbeleni ikitokea kuna jambo ambalo halimpendezi yeye binafsi basi hatosita kutumia vyombo vya dola kuwatisha watu ili waache kufanya walichokuwa wamepanga kufanya.

Hiyo ndo Tanzania mpya. Tanzania ya MWENYE ENZI, Mtukufu rais John Pombe Joseph Magufuli [nahisi pia tutalazimishwa kuyatumia majina yake yote manne la sivyo wataokiuka watatafutwa na kuadhibiwa, hata kama wapo mitandaoni].

Na nyie wachora vikatuni nahisi dawa yenu inakorogwa huko maabara. Kama mkiendelea kumchora vibaya MWENYE ENZI, MTUKUFU rais John Pombe Joseph Magufuli basi siku zenu zinahesabika.

Yakiwatokea ya kutokea msije lalama eti sikuwaambia! Shauri yenu.
Kashinda kwa kishindo....
 
Back
Top Bottom