Maandamano ya UKUTA yasipofanyika...

Maandamano ya UKUTA yasipofanyika...

Ni bora CDM warudi nyuma na UKUTA ili waje kivingine...!
Ila ishu itakuwa kwa CCM na serikali yake. Hawatakaa watulize akili zao..!!
 
Hayo maandamano yasipotokea atakuwa kafanikiwa kuwatisha wananchi katika kutofanya yale ambayo hayampendezi yeye.

Na huu ndo utakuwa mwanzo tu. Huko mbeleni ikitokea kuna jambo ambalo halimpendezi yeye binafsi basi hatosita kutumia vyombo vya dola kuwatisha watu ili waache kufanya walichokuwa wamepanga kufanya.

Mimi nilidhani Chadema watakuwa a bit serious
 
Kama UKUTA wakinywea na mwishowe kutokufanya hayo maandamano yao ambayo wamepanga kuyafanya hiyo tarehe 1 mwezi ujao, basi mheshimiwa MWENYE ENZI, MTUKUFU rais Magufuli atakuwa amepata ushindi mkubwa sana.

Hayo maandamano yasipotokea atakuwa kafanikiwa kuwatisha wananchi katika kutofanya yale ambayo hayampendezi yeye.

Na huu ndo utakuwa mwanzo tu. Huko mbeleni ikitokea kuna jambo ambalo halimpendezi yeye binafsi basi hatosita kutumia vyombo vya dola kuwatisha watu ili waache kufanya walichokuwa wamepanga kufanya.

Hiyo ndo Tanzania mpya. Tanzania ya MWENYE ENZI, Mtukufu rais John Pombe Joseph Magufuli [nahisi pia tutalazimishwa kuyatumia majina yake yote manne la sivyo wataokiuka watatafutwa na kuadhibiwa, hata kama wapo mitandaoni].

Na nyie wachora vikatuni nahisi dawa yenu inakorogwa huko maabara. Kama mkiendelea kumchora vibaya MWENYE ENZI, MTUKUFU rais John Pombe Joseph Magufuli basi siku zenu zinahesabika.

Yakiwatokea ya kutokea msije lalama eti sikuwaambia! Shauri yenu.
Kweli wewe nyani.
 
Mimi nilidhani Chadema watakuwa a bit serious

Deep down mimi nilikuwa na feeling hayo maandamano ilikuwa ni tishia nyau tu.

Watanzania ni watu waoga mno.

Walio tayari kupigwa virungu huenda hata 10 hawafiki.

Wengi wetu ni majasiri wa kwenye mitandao tu.
 
Tuna tatizo kubwa sana kuwa taifa la waoga na wanafiki

we will never accomplish anything

Kwa sababu hata Katiba ambayo ndio msingi wa yote huwezi kuletewa tu bila struggles tena struggles za kuumizwa na kuuawa....
 
Ulidhani mi kima?
Nyani Ngabu siyo tu rais kapata ushindi, bali pia viongozi wenu wa chama mfu wamekosa muelekeo. Wewe unagombana na mkeo, halafu unakuja kusema eti jirani alikua kuniomba tumalize ugomvi mke wangu hivyo nimemsikiliza, huo ni woga wa chadema. Na mgeandamana mge kipata cha mtema kuni, ila kwa nyie wabeba mabox hakuna noma kwanza na IP zenu mnaficha ndiyo maana kiburi chenu kipo juu
 
Na the worst part ili kuwa kuwaachia CHADEMA only
i mean hata asasi za kiraia wako kiimya
vyombo vya habbari vinafungiwa...vinatetemeka

now CHADEMA wakidhibitiwa ndo watu milioni 50 wote kwisha
 
Wanasiasa wamecheza na akili zao,jeshi la wananchi kufanya mazoezi tarehe moko ni mchezo wa kisaikolojia na Watanzania wanaogopa sana mavazi yenye mabakamabaka,JWTZ halipo kisiasa bali limetumiwa kisaikolojia na wanasiasa Game over.
 
Na ameshafanikiwa...CHADEMA walibaki peke yao kidogo..sasa na wao wamekubali Ku surrender kijinga kabisa

CUF nawalaumu zaidi
wangesogeza mbele ishu zai ili hii ishu ipite
wao wamejifanya kufanya mkutano...wakaharibiwa kabisa
now wana mgogoro...huku CHADEMA wako alone wakitishiwa
 
Hivi maandamano yanazuiwa kwa sababu gani tena??
Bado ni ile ya kuhisi kutakuwa na uvunjifu wa amani?
Kama ni hiyo bado nadhani waandaaji wa hayo maandamano waende wakaongee na hao wenye kuyazuia wapange namna ya kuyaboresha ili yawe ya amani kama hayo yanayoruhusiwa
 
Nimenunua mask, nimenunua buti mpyaa nimechoka na vijimsemo watanzania n9 waoga wa mabomu, ninayo experience yaliyo tokea soweto Arusha na mimi nilikuwa miongoni wa walio nusurika, iwe mvua iwe jua Mimi binafsi lazima nishiriki maandamano, now nipo Arusha na tumejipanga vya kutosha, hatuta leta vurugu, tutakuwa na vitambaa vyeupe kumaanisha maandamano ni ya amani, pia hatuta pita mainroad tutatumia service road ili kuepuka msongamano.
 
Na the worst part ili kuwa kuwaachia CHADEMA only
i mean hata asasi za kiraia wako kiimya
vyombo vya habbari vinafungiwa...vinatetemeka

now CHADEMA wakidhibitiwa ndo watu milioni 50 wote kwisha
Na ameshafanikiwa...CHADEMA walibaki peke yao kidogo..sasa na wao wamekubali Ku surrender kijinga kabisa

Nilipomsikia Zitto anasema wao ACT watachangia damu, basi!

Nikajua CHADEMA wapo peke yao.

Halafu, nilipomuona Lowassa kwenye ile sherehe ya Mkapa, nikahisi huenda kuna jambo hapo.
 
CUF nawalaumu zaidi
wangesogeza mbele ishu zai ili hii ishu ipite
wao wamejifanya kufanya mkutano...wakaharibiwa kabisa
now wana mgogoro...huku CHADEMA wako alone wakitishiwa

So far nawapongeza CHADEMA...Wamefanya kazi kubwa.....Kupambana na tawala kandamizi ni kazi kubwa sana

Hata sisi huku Jamiiforum hatuko salama.....Kwa sasa hatupaswi kukosoa asilani

Kama CHADEMA wa-me/ki surrender...Kinachofuatia ni kibaya zaidi
 
Nyani Ngabu siyo tu rais kapata ushindi, bali pia viongozi wenu wa chama mfu wamekosa muelekeo. Wewe unagombana na mkeo, halafu unakuja kusema eti jirani alikua kuniomba tumalize ugomvi mke wangu hivyo nimemsikiliza, huo ni woga wa chadema. Na mgeandamana mge kipata cha mtema kuni, ila kwa nyie wabeba mabox hakuna noma kwanza na IP zenu mnaficha ndiyo maana kiburi chenu kipo juu
Hicho cha mtema kuni kikiwa ndani ya katiba hata hakimtishi mtu lakini kikitekelezwa kinyume na utaratibu sio cha kufurahia. Watu wengi hapo kabla waliamini kuwa kutumia siasa wangeliweza kuachieve walichotaka lakini kwa hivyo vi-'mtema kuni' uenda kukatokea ideology mpya za watu kufikiri ni jinsi gani ya kufanya kazi chini ya vitisho badala ya katiba. Tuombee Mungu tusifike huko maana aina hii ya fikira ni sawa na nyoka wa sumu ambaye anadhuru kiumbe bila hata kujishibisha!
 
Nilipomsikia Zitto anasema wao ACT watachangia damu, basi!

Nikajua CHADEMA wapo peke yao.

Halafu, nilipomuona Lowassa kwenye ile sherehe ya Mkapa, nikahisi huenda kuna jambo hapo.

Kwa Lowasa inaweza ikaeleweka...Jamaa alikuwa anaangalia uwezekano wa kuwa na mazungumzo kuepusha tatizo zaidi...alikuwa anatuma ujumbe wa Amani zaidi....

kuwe na win win situation.....Wanasiasa pia wafanye kazi zao

Ili nchi iende vyema tunahitaji pia hoja kinzani...sio vyema kuwa silenced wote
 
Tuna tatizo kubwa sana kuwa taifa la waoga na wanafiki

we will never accomplish anything

Kwa sababu hata Katiba ambayo ndio msingi wa yote huwezi kuletewa tu bila struggles tena struggles za kuumizwa na kuuawa....

Hebu cheki huko kwingine jinsi watu wasivyowaogopa polisi.

Mtu zinaingia kitaa kuzipiga na polisi.

Watanzania tunayaweza haya?

Back
Top Bottom