Maandamano ya UKUTA yasipofanyika...

Maandamano ya UKUTA yasipofanyika...

Kama UKUTA wakinywea na mwishowe kutokufanya hayo maandamano yao ambayo wamepanga kuyafanya hiyo tarehe 1 mwezi ujao, basi mheshimiwa MWENYE ENZI, MTUKUFU rais Magufuli atakuwa amepata ushindi mkubwa sana.

Hayo maandamano yasipotokea atakuwa kafanikiwa kuwatisha wananchi katika kutofanya yale ambayo hayampendezi yeye.

Na huu ndo utakuwa mwanzo tu. Huko mbeleni ikitokea kuna jambo ambalo halimpendezi yeye binafsi basi hatosita kutumia vyombo vya dola kuwatisha watu ili waache kufanya walichokuwa wamepanga kufanya.

Hiyo ndo Tanzania mpya. Tanzania ya MWENYE ENZI, Mtukufu rais John Pombe Joseph Magufuli [nahisi pia tutalazimishwa kuyatumia majina yake yote manne la sivyo wataokiuka watatafutwa na kuadhibiwa, hata kama wapo mitandaoni].

Na nyie wachora vikatuni nahisi dawa yenu inakorogwa huko maabara. Kama mkiendelea kumchora vibaya MWENYE ENZI, MTUKUFU rais John Pombe Joseph Magufuli basi siku zenu zinahesabika.

Yakiwatokea ya kutokea msije lalama eti sikuwaambia! Shauri yenu.

UPDATE:

Raundi 1.

Magufuli 1, UKUTA 0.
hilo ndio lengo la ukuta kubainisha ukandamizaji,ikiwa ukandamizaji unabainika kwa nini tukubali watu wafe wakati unaona dhairi kuna watu wamejitayarisha kutoa roho za watu na watu wengene wamejitayarisha kufuraia mauaji?
 
Kughairisha maandamano kunafanya wanachama wasiwaamini Tena viongozi wao Kwa ahadi zozote...!!

Jamani mbona hili lilikua wazi. Wengi humu walishaambiwa Lowassa hawezi kushinda Urais 2015, wakabisha. Lowassa hakushinda.

Kamati kuu ya chadema ilipokaa kikao cha siku 4 wakaja na ukuta, wakaambiwa hiyo ni wrong move haiwezi kufanikiwa, wakabisha. Ukuta ume melt.

Chadema ni chama mfu kwa sas, cuf ni chama mfu. TLP, UDP na NCCR hoi bin taaban.

ACT wataweza?
 
Jamani mbona hili lilikua wazi. Wengi humu walishaambiwa Lowassa hawezi kushinda Urais 2015, wakabisha. Lowassa hakushinda.

Kamati kuu ya chadema ilipokaa kikao cha siku 4 wakaja na ukuta, wakaambiwa hiyo ni wrong move haiwezi kufanikiwa, wakabisha. Ukuta ume melt.

Chadema ni chama mfu kwa sas, cuf ni chama mfu. TLP, UDP na NCCR hoi bin taaban.

ACT wataweza?
nitachukua kadi ACT
 
Vyama Vya Upinzani (VVU ) wanadhani watakwenda Ikulu kwa kuota ndoto.
Ni rahisi zaidi mbwa kupiga mswaki kuliko VVU kwenda Ikulu.
 
Back
Top Bottom