Mimi ninasupport maandamano ingawaje sio a quick solution lakini pole pole tutafika....ninachosema ni kuwa...Huwa ninafuatilia hii forum lakini ukweli ni kuwa tutokage huku na kuspread news za mambo mengi kwenye social networks nyingine pia. Kuna wengi hawajui hii forum na kuna wengine wameshapeleka habari kuwa huku ni wahuni tu ndio wako basi mambo mengi yanaishia huku bila kufika au kujulikana na watu wengi. Hivyo tujitahindi kwenda na msg hixi hizi kwenye social networks nyingine ili watu wengi wapate huu ujumbe. Nadhani ni watu wachache sana wanaofahamu kuhusu haya maandamano.. Mimi mwenyewe nimeyafahamu kuwa yattakuwapo week hii sasa ujue ni wanagapi wangependa kuhudhuria lakini hawana habari ya haya maandamano? Na unajua kuna bloggers hawapost haya mambo....
Na kingine tukienda kwenye hizo social networks nyingine tutumie majina yetu kamini na watu watujue ni nani? Mimi niko kwenye twitter na utashangaa nikipost kitu watu kinachowagusa wengi badala ya watu kupost nao mawazo yao wanavyofikiria ni kunitumia personal emails na kusupport hoja au kuadd kitu kingine juu ya hoja. Kwa nini ni watu wachache wanaopenda kujulikana hadharani ni vipi wanafikiria kuhusu mambo fulani? Ni uoga au unafiki tulionao...Tukiwa AKA anonymous tunajidai tuna hasira na uchungu na nchi yetu lakini kwenye sehemu ya watu wanao kufahamu wewe ni nani uko kimya...Au ni fasadi within us...leo unakosoa watu kesho unapokea rushwa...TUjivue na sisi magamba ya anonymous bila hivyo hatutafika kwa vile hatujui nani anatetea mafisadi, nani anakula nao sahani moja.
Ni hayo tu together we can....My 2 cents