@Mkandara
Kwanza nitazungumzia haya maandamano ya Washingtona DC, BBinafsi nayaona ni waste of time - I dont think so mate. Maandamano huko WEST hayatazamwi kwa jicho la kupuuza kama huku.
Labda nirudie tena kusema kwamba kwa kila maamuzi tunayoyafanya muhimu zaidi ni kutazama WATU na MAZINGIRA.
wewe umesema Huko west maandamano hawayatazami hivyo? unaelewa unachokisema au unazungumza tu maanake huko west ndiko NAKOISHI..Huku maandamano yanaweza kufanywa na mtu yeyote hupinga kitu chochote na wakati wowote pasipo kuwa big deal kabisa na mara zote maandamano huwa yanapinga kitu fulani na kuonyesha kilicho bora. Unaweza andamana kutetea kuvuta bangi na hata kutembea uchi ni haki yako pia kujieleza...
Kwa mfano unaweza andamana kupinga matumizi ya gari na mafuta ya Petrol kwa kuonyesha nadhara ya gari ktk kuharibu mazingira, hewa, kuleta maradhi na kadhalika..Ni maandamano mabayo hakuna mtu atashtuka nayo ila unatumia haki yako ya kimsingi kujieleza. Sema tu kwa maandamano ya DC hakuna FFU wala mtu kupigwa virungu...
Watanzania wenzangu inabidi tufike mahala tujitazame sisi wenyewe na kujiuliza tunaifanyia nini Nchi yetu - Tunadai good governance, kwa mawazo kwa maneno na kwa vitendo. What else do you want people to do?
Your suggestion: Safu ya washauri Magogoni, wachukilie hili kama changamoto na kuanza haraka kukabiliana na mambo yanayodaiwa na wananchi. Hatua kumi huanza na moja! Wasipuuze kelele za wananchi hata kidogo, wako vijana wengi mno hawana kazi na wala hawajui kesho watakula nini let alone maisha yao yatakuwaje huko mbeleni. Na kwa population ya Tanzania vijana ndio wanaounda sehemu kubwa ya population. Ni vizuri kuchukuwa hatua za haraka....
Umeona basi Your suggestion inarudi kwa serikali na sio wewe utafanya nini zaidi ya kuandamana huko nje ya nchi! kwa nini unashindwa ku suggest kitu cha kufanya wewe kama mwananchi maanake tumelalamika toka Mwinyi, Mkapa na sasa hivi JK.. matatizo ndio yanazidi tu mwaka hadi mwaka.. why is it so special leo wewe unaandamana nchi za nje ili iweje? kwanza ni ikitendo ambacho hakitatambuliwa, hakina mvuto na labda nikwambie tu kwamba wakati wa mikutano ya UN nchi zaidi ya 20 huwa na wananchi wanaoandamana na mabango kuzipinga serikali zao. Hutokea nini zaidi? hakuna lolote unless nchi hiyo ina mahusiano mabaya ya Marekani.
Tazama sasa Marekani baada ya kuona wanashindwa Libya sasa hivi kimyaaa wamegeuza macho yao kuelekea Syria na wanawaacha wananchi vijana waliojitoa mhanga kupigana na Ghadhaff kwenye mataa. Umesikia CNN au BBC hivi karibuni wakiweka nguvu kutangaza habari za kumwondoa Ghadaffi na Libya kama zamani?...Je, umejiuliza kwa nini Marewkani na UK wamejitoa kiulainiii.. Kwa hiyo nachotaka kusema tunapeleka message to the wrong people kwa sababu Marekani na Tanzania hasa utawala wa CCM ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa..
My suggestion:- Wewe na Watanzania woote wenye kutaka mageuzi acheni tabia ya kuruka matatizo. Ni wakati wa kuya face wazungu wanasema take the bull by the horns!...na sio kutegemea Mungu, ipo siku moja sijui tumerogwa na kadhalika. Get up! stand up! Bob katwambia 20+ yrs ago.. simameni ktk mikutano na mwambie JK mbele ya wananchi wenzako kwamba ameshindwa kuongoza nchi... Acheni kuijificha nyuma ya majina bandia kama kweli nyie mnataka kuleta mabadiliko nchini. Simama na wakilisha hoja yako sehemu ambayo una hakika utapata matokeo bora zaidi na sio kuruka viunzi..