Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,180
- 7,355
Najua yapo mambo mengi ya kuandamana kwa sasa. Hata hivyo mi nadhani hili la bunge kuendeshwa ki-hovyo hovyo na Spika Makinda ni kubwa na jambo la hatari sana kwa maendeleo ya taifa letu. Nawashauri CHADEMA, na wote wanaokerwa na mama huyu, wafanye maandamano nchi nzima au sehemu kadhaa za nchi, kulaani uendeshaji mbovu wa bunge unaofanywa na spika. Ingawa najua haitafanya aondolewe madrakani, naamini itamoa msg, na itamfanya ajue kuwa anachokifanya bungeni kinawaudhi wengi. Mi nadhani kwa sasa anadhani kuwa hajashtukiwa kuwa anaendesha bunge visivyo, so akiona maelfu wameandamana kumlaani, atapata funzo fulani/
------------------------------------------------------------------------------------

UPDATE
Nimefuatilia kwa karibu jinsi mama huyu anavyoendesha kikao cha bajeti, na ukisoma taarifa ya jinsi anavyomkingia kifua Pinda, naona bado haya maandamano hayaepukiki.