Sakata la Mbunge Mpina na uchambuzi wa ndani zaidi kisiasa na maamuzi ya spika wa bunge Nini hasa bunge litaathiri kwa mzawa huyu

Emmanuel38

New Member
May 30, 2024
2
0
Na; Bk

Leo, Jumanne Juni 18.2024 mapema asubuhi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson ameagiza Mbunge wa jimbo la Kisesa Mheshimiwa Luhaga Mpina kufikishwa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa kuwasilisha ushahidi wa tuhuma zake kuhusu Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Hussein Bashe kulidanganya Bunge mbele ya vyombo vya habari kabla ya uamuzi wa Spika

Kwa muujibu wa kanuni za kudumu za uendeshaji wa Bunge, Spika wa Bunge akiomba taarifa kutoka kwa Mbunge yeyote ama Kamati ya Bunge ikielekezwa na Spika wa Bunge kupeleka taarifa yoyote kwake ama tuhuma au ushahidi wa jambo lolote lile, hiyo taarifa sio taarifa ya umma bali ni taarifa ya Spika ama taarifa ya Kamati ya Bunge hivyo haipaswi kutolewa nje na mpeleka taarifa bali kwa idhini ya Spika mwenyewe ama mamlaka ambayo Spika atakuwa amekasimisha Kwa wakati huo

Hivyo basi kwa muujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge Mheshimiwa Luhaga Mpina anaweza kupatikana na hatia na kwa kweli mimi napendekeza ashughulikiwe kwa muujibu wa sheria na kanuni za Bunge ili kuweka nidhamu na kuliheshimisha Bunge, lakini swali ambalo tunapaswa kujiuliza sisi wananchi ambao sio Wabunge, je Mpina hakujua kwamba kwenda kusambaza huo ushahidi wake dhidi ya kile alichodai kuwa ni uongo wa Waziri Hussein Bashe mbele ya vyombo vya habari na kupelekea ushahidi huo kusambazwa nchi nzima kama ni kosa kwa muujibu wa kanuni za Bunge?

Mpina amekuwa mbunge karibu miaka 20 sasa, haiingii akilini kuwa hafahamu kufanya hivyo ni kutenda kosa, kama alikuwa anajua, je kwa nini alitenda kosa ambalo alijua mwisho wa siku atakumbana na adhabu kali?, mimi nadhani Luhaga Mpina amefanya kosa hili kwa sababu moja tu kubwa, hakuwa na imani na Bunge letu kwamba linaweza kutekeleza wajibu wake wa kuisimamia serikali, hivyo ikabidi akimbilie kwenye Mahakama ya umma (wananchi), Mahamaka ambayo anadhani akifanikiwa kuishawishi kukubaliana na hoja zake, atakuwa ametimiza wajibu wake kwa sehemu kubwa kuliko kupeleka ushahidi wake ule Bungeni ambapo kwa hali ya kawaida anadhani kungetokea mambo ya kulindana hata umma usingepata kujua nini kimetokea na ukweli wa sakata hili la ubadhirifu wa mabilioni ya shilingi ambazo kimsingi ni fedha za walipa kodi wa Tanzania

Swali la kujiuliza hapa ni kwamba nini faida na hasara ya Luhaga Mpina kuamua kutumia njia aliyoitumia kwenye hili sakata lake na Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Hussein Bashe, tuanze na hasara, kwanza hasara itampata yeye binafsi kwa kuadhibiwa na Bunge, hata ikitokea amesamehewa (ingawa kwa mtazamo wangu sioni akisamehewa) basi atakuwa amepunguzwa nguvu kwa kitendo cha yeye kushindwa kufuata kanuni na taratibu za kushughulikia matatizo akiwa mwakilishi wa wananchi, na hatimaye Bunge linaweza kutumia mwanya huo kukoroga ushahidi wake kwa sababu tu amelidharau Bunge na hatimaye mtuhumiwa kukwepa kitanzi hata kama kweli alitenda makosa hayo

Kwenye upande wa faida hapa Luhaga Mpina amegeuka kuwa mtetezi wa Watanzania dhidi ya watendaji wa serikali wazembe ambao wameshindwa kushughulikia matatizo ya wananchi hatimaye wamejikita kufanya biashara kwenye ofisi za umma, ushahidi alioutoa Mheshimiwa Luhaga Mpina hata kama hautafanyiwa kazi na Bunge, lakini umma wa Watanzania umepata kujua nini hasa kilichojili kwenye sakata la uagizaji wa Sukari na jinsi ambavyo biashara ya sukari ilivyo na ushawishi wa fedha kiasi kwamba inawezekena kabisa sheria za nchi zikawekwa pembeni na watumishi wa umma ambao wamekula kiapo cha kulitumikia Taifa hili kwa uadilifu.

(fuatilia Uzi huu)

Pia soma

- Spika Tulia amburuza Luhanga Mpina Kamati ya maadili
 
Binge letu linafanya kazi kwa maelekezo ya CCM kutetea ufisadi ili kunenepesha matumbo yao,hakuna bunge pale ni kikundi cha masela wanaonufaika na Kodi za wananchi!!
Bunge hili haliwezi kufanya jambo lolote kwa maslahi ya nchi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom