Maandamano ya CHADEMA Mbeya yaruhusiwa

Maandamano ya CHADEMA Mbeya yaruhusiwa

Unajua Tanzania sheria inasema kitu tofauti na mambo yanatendwa tofauti. Fikiria sheria inasema Chama cha Siasa kinapotaka kufanya mkutano au kuitisha maandamano kitoe taarifa kwa maandishi (siyo kuomba ruhusa) kwa kamanda mkuu wa polisi wa eneo husika katika muda usiopungua saa 48. Kama CDM wametoa taarifa kadiri ya matakwa ya sheria, na mpaka siku ya mkutano au maandamano inafika ndo polisi wanaibuka na taarifa za kiintelijensia, kasoro ipo kwa nani? Bahati mbaya kwa yale yaliyotokea Arusha, polisi hawakutoa kizuio kwa maandishi bali aliibuka mtu mwingine anayazuia kwa kutumia TV(siyo maandishi) na wala hakuwa kamanda wa polisi wa eneo husika. Hivyo, Tanzania bado mambo hayajakaa sawa.

Ndugu!!
Tambua jambo moja kwamba:- Dalili moja wapo ya umaskini ni watu kutofuata sheria. Kwa hivo sishangai kuona serikali yenyewe inavunja sheria kwani ni halali kwa nchi isiyopiga hatua kama tulivyo Tanzania!
 
Jamani naomba kutofautiana na wengi Alberto Msando ni Diwani wangu na kiongozi wa CDM lakini kwa nini huwa nawasiwasi naye?
 
NA EMMANUEL LENGWA

Lwakatare(3).jpg

Mwenyekiti wa Mkoa wa Kagera, Wilfred Lwakatare

Baadhi ya viongozi wa Juu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema) wameanza kuwasili mkoani hapa kwa ajili ya kuongoza maandamano ya chama hicho yaliyopangwa kufanyika kesho, jijini hapa.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Mbeya, Eddo Mwamalala, alisema hadi kufikia jana timu moja ya viongozi kutoka Dar es Salaam ikiongozwa na Mwenyekiti wa Mkoa wa Kagera, Wilfred Lwakatare, imeshawasili na kuwa viongozi wengine wanatarajiwa kuwasili leo.
Mwamalala alisema tayari wamewasilisha maombi ya kibali cha maandamano katika Ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi.
Alisema maandamano hayo yanatarajiwa kuanzia maeneo ya Iyunga na kuishia maeneo ya Rwandanzovwe katika viwanja vya Dk. Slaa.
Alizitaja njia zilizopendekezwa na Chadema kupitiwa na waandamanaji kuwa ni barabara Kuu ya Tanzania- Zambia (Tanzam) kuanzia Iyunga hadi Meta kuelekea kwenye mnara wa Sabasaba kisha kushika barabara ya Sokoine hadi maeneo ya Uhindini.
Alisema waandamanaji wataibukia maeneo ya Sinde na kupitia Mwanjelwa, Soweto, Mama John na kunyoosha moja kwa moja hadi Rwandanzovwe kwenye viwanja vya Dk. Slaa ambapo utafanyika mkutano mkubwa utakaoongozwa na viongozi wa kitaifa wa Chadema.
Kwa mujibu wa Mwamalala watu wataanza kukusanyika tangu asubuhi na maandamano hayo yataanza majira ya saa 5:00 asubuhi na inatarajiwa kuwa ifikapo saa 8:00 mchana waandamanaji watakuwa wamefika viwanjani kwa ajili ya kuanza mkutano.

CHANZO: NIPASHE
 
Sheria unayosema ifuatwe inasemaje? Ili tuache bla bla mimi na wewe jaribu kujibu hili
 
Quinine, nadhani swali ungelielekeza kwangu ili kwanza nipate fursa ya kujibu kuhusu wasiwasi ulio nao kwangu. Nipo hapa na unaweza kuweka jamvini wasiwasi wako dhidi yangu bila kunga'ata neno lolote.
 
Ndugu zangu wana Mbeya tusigeuzwe mtaji wa kisiasa na hawa Wachaga wa Chadema, zindukeni wacheni kulala wana Mbeya tutakuja kujuta tusipokuwa makini, Ebe jiulizeni kama kweli nyie ni chadema, kati ya Wabunge (25) wa viti maalum wa Chadema Mbeya hakuna hata Mbunge mmoja wengi wamepewa wachaga wenzao ndio wengi wakati Mbeya ndio mmempa Dk Slaa kura nyingi za Urais, Mwanza ikishika nafasi ya pili wenyewe wamepewa kiti kamoja tu, wana Mbeya susieni hayo maandamano ya mafisadi Chadema, WANA MBEYA ZINDUKENI ACHENI KUJIPENDEKEZA CHADEMA HATA MBUNGE MMOJA WA VITI MAALUM MMENYIMWA NA HAWA WACHAGA WA CHADEMA:amen:

Hatudanganyiki.
Peeeeeeeeeeeeeople's Pawaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
 
Jamani mbona hizi habari za kuzuia maandamano ya Chadema nimezisikia toka mwezi March nikiwa bado Bongo?...Viongozi wa serikali walikutana na ma RPC wote ktk mkutano maalum uliofanyika Arusha au Moshi (sina uhakika) na maamuzi yaliyofikiwa ni kutowaruhusu Chadema kufanya maandano kwa nguvu zote - Amri ilitolewa na nguvu ya dola itumike pindi ikibidi..

Sasa nashangaa kusikia Chadema bado wanataka kufanya maandamano hali wanajua fika kwamba serikali inawasubiri kwa hamu na maamuzi yamekwisha pitishwa kuhakikisha hakuna ruksa ya maandamano ya aina yeyote hasa kutoka Chadema kwa visingizio vya Usalama wa taifa. Ndiuo maana mkaona vongozi wengi wa CCM wakifuatia kusema ovyo kuhusu maandamano ya Chadema na Mzee Wasira kusema Chadema wakijaribu watashughulikiwa akijua wazi maamuzi ya mkutano ule.

Mimi nadhani Chadema hawana sababu ya kufanya maandamano kwa sasa ila wafanye mikutano ktk viwanja kwani hakuna tofauti kubwa sana baina ya maandamano na mikutano ktk kuwataarifu wananchi. Kweli maandamano yanaweza kuleata picha ya hatari kwa CCM maana nijuavyo mimi maandamano mara zote hutakiwa kuishia pale unapolenga malalamiko yako... lakini kuandamana wakati mnakwenda uwanja wa mpira kufanya mkutano inaweza kuwa njia nzuri ya kuvuta watu lakini pia inawatisha zaidi CCM kwa sababu wanajua fika kwamba leo hii wananchi wana hasira nao..Kila maandamano yanapofanyika jezi za kuvaa CCM ni hatari kwa maisha yako uwe mwana CCM au sio..

Kutokana na sababu kama hizi, badala ya CCM kujiuliza kwa nini wananchi wanawachukia na kukubali makosa wanayoyafanya ili wapate kujirekebisha, wao wataendelea kumtafuta mchawi wao na hakuna zaidi isipokuwa Chadema. Hivyo vita yao badala ya kuelekeza ktk mapungufu yao watakusanya nguvu zao kupambana na Chadema, na sisi wananchi hatukuwa tumefanikiwa kwa lolote zaidi ya kuangalia vita ya vyombo ambavyo tunavitegemea kisiasa. Yale yale na Hamas na Fatah kule Palestine yamewadhoofisha zaidi ya kuwajenga..
 
Baada ya mvutano mkali kati ya RPC na Waheshimiwa Josephy Mbilinyi na David Silinde hatimaye RPC ameruhusu maandamano yaliyopangwa.

Thank You to you RPC kwa kuwa muelewa na kujali demokrasia.

Aluta Continua

Ahsanteh dad Regi kwa taarifa. Peeeepoooooooooooooooooooooz Pawaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
 
Quinine, nadhani swali ungelielekeza kwangu ili kwanza nipate fursa ya kujibu kuhusu wasiwasi ulio nao kwangu. Nipo hapa na unaweza kuweka jamvini wasiwasi wako dhidi yangu bila kunga'ata neno lolote.

Labda(hisia zangu) ana wasiwasi na mwenendo wako.....

Mfano kumtetea Diwani wetu wa CCM mahakamani...

Kuleta thread hii ambayo kwa namna moja ama nyingine ingeweza kuathiri mahudhurio ya maandamano hapo kesho kwani watu wengi watajua maandamano yamezuiwa na Polisi kitu ambacho si kweli....

Ni mtazamo tu...

Bala.
 
Ukitaka kuona jinsi timu inavyofungwa ni pale ambapo dakika zote mpira huwa unakuwa upande mmoja,hapa mabeki ujitahidi kuzuia lakini nao uchoka,faulu hushika kasi na baadae uzaa goli,ama kwa frii kiki,piga nikupige ama kwa penati na shughuri huwa imeisha maana jahazi uzama kwenye kina kirefu ...sahvi CCM wamebaki na nguvu kdogo za kuzuia na beki zote (polisi,media,Mashehe,wapinzani wanandoa,DCs RC,s n.k) zishafunguka zinacheza rafu kila kona,natabili kuchoka huku karibu CDM wanapata gori ama kwa frii kiki ama kwa penati (literary)....
 
You Great Thinkers....! what's wrong with You? imekuaje mmeanza kuchangia hoja ambayo chanzo chake hakijulikani? watu wengine wapo hapa kwa maslahi ya wenyewe! hapa wanachokonoa hisia za watu kwa taarifa za kushtusha kama hiyo halafu wanajiweka pembeni na kuona mnavyoparanganyana!

taarifa kama hii ni ya kuignore...! CDM haijathibitisha kuzuiwa kufanya maandamano sasa wasiwasi wa nini hapa jamvini? tujadili mambo mengine wakuu!
 
Baada ya mvutano mkali kati ya RPC na Waheshimiwa Josephy Mbilinyi na David Silinde hatimaye RPC ameruhusu maandamano yaliyopangwa.

Thank You to you RPC kwa kuwa muelewa na kujali demokrasia.

Aluta Continua
CCM sasa inambinu mpya za kutawala kwanza wanapenyeza habari fulani alafu wanapima upepo wakiona unaenda vibaya wanabadilisha maamuzi.Mfano kuhusu utaratibu wa mabadiliko ya katiba,mkanganyiko kuhusu usanii wa kujivua magamba na mabo mengine mengi hali hii ni hatari kwani inaweza kusababisha vurugu,MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Hizi topic za tetesi sio za kutolewa na kiongozi,...unatakiwa kujibu juu ya tetesi!
 
Nilidokeza kuhusu uwezakano huo siku mbili zilizopita. Hata hivyo jana nilihudhuria japo kwa kuchelewa kikao cha CDM Mbeya mjini kikwa chini ya Mh Wilfred Lwakatare tukahakikishiwa kuwa RPC ameruhusu maandamano japo kwa masharti, sasa huyu Mwakipesile amepata wapi hizo Intelijensia? Ndio maana tunasema hakuna haja ya wakuu wa Mikoa maana kazi ni kuibeba CCM

Inasikitisha intelijensia kwenye maandamano ufisadi unafanyika wanakuwa wapi? magamba yanawasumbuwa
 
Quinine, nadhani swali ungelielekeza kwangu ili kwanza nipate fursa ya kujibu kuhusu wasiwasi ulio nao kwangu. Nipo hapa na unaweza kuweka jamvini wasiwasi wako dhidi yangu bila kunga'ata neno lolote.
MsandoAlberto

Labda nianze na hii habari, kweli umenisikitisha sana, wewe kama kiongozi wa ngazi ya juu wa Chadema (Diwani) inakuwaje utoe taarifa hii ya tetesi bila kuzingatia athari zake, hata kama zilikuwa habari za kweli haraka namna hiyo ilikuwa ya nini tena bila kushauriana na viongozi wenzako kuangalia athari zake? huoni kwa kutoa taarifa hii ya tetesi umepoteza baadhi ya watu waliopanga kuja kwenye maandamano? nitakutofautishaje na kina Malaria Sugu na GeniusBrain wanaoleta habari za tetesi ili kupotosha wana JF na kumfurahisha Mukama? je kwa kufanya hivyo kwa kuwa wewe ni kiongozi huoni watu wataanza kutokuamini habari zako na kupelekea kutowaamini viongozi wa juu wa chama kuwa ni wazushi kama wewe? kwa tukio la leo utakataa baadaye ukihusishwa na kuvuja kwa siri za vikao vya chama kabla ya kikao kwisha? ni hayo tu kwa sasa.
 
Polisi hawahusiki hapo, chanzo mtakuwa nyie kama mlivyo fanya arusha. Wao wameisha waambia maandamano yenu ni marufuku, sasa mkitaka kufanya kwa nguvu dola haita waachia


Waliofyatua risasi na kuuwa riaa huko Arusha ni police. get your facts right. Police hawana mamlaka kisheria ya kuzuia mikusanyiko ya vyama vya siasa. Kitendo cha police kujiingiza kwenye shughuli za kisiasa kinyume kwa kisingizio cha 'habari za kiiteligensia' si tu kinaashiria utawala wa kimabavu bali kinaanika uwoga wa hao wanaotuma.
 
Arusha walitustukiza hatukuwa tumejiandaa japo siku ya mazishi tulikuwa kamili Kama mbwa wenye vichaa wangekuja kutung'ata,mimi mwenyewe nilikula kitako cha bunduki sema mbio na mbinu zilinisaidia kuwatoka mbwa wenye vichaa kuning'ata..Watanzania wenzangu mlio Mbeya Kama Polisi walishindwa kufanya intelijensia ktk"UPOTEVU WA MABILIONI YA WALIPA KODI EPA,RICHMOND to DOWANS,KAGODA,UBINAFSISHAJI MIGODI,MISHAHARA HEWA ILIYOLIPWA(bilioni48 kwa mwaka mmoja)na nyingine nyingi msikubaliane nao sbb hao Polisi watakuwa wametumwa na Chama cha magamba asilani abadani kataeni.

Ninavo wafahamu mbalizi mlowo bira kuwasahau boda ya wajanja tunduma kwa sauti ya simba silinde ata kova anawafahamu au mama jk anawafaham walisha pinda
 
CCM sasa inambinu mpya za kutawala kwanza wanapenyeza habari fulani alafu wanapima upepo wakiona unaenda vibaya wanabadilisha maamuzi.Mfano kuhusu utaratibu wa mabadiliko ya katiba,mkanganyiko kuhusu usanii wa kujivua magamba na mabo mengine mengi hali hii ni hatari kwani inaweza kusababisha vurugu,MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Yuo are very right Advocate Jasha na watu wanaotumika lazima wawe wanaoamika ili habari ionekane kuwa ya kweli.
 
Back
Top Bottom