Maandamano ya CHADEMA Mbeya yaruhusiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maandamano ya CHADEMA Mbeya yaruhusiwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MsandoAlberto, May 5, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Taarifa zilizopatikana ni kwamba RPC Mbeya amepiga marufuku maandamano ya CDM kwa sababu ya taarifa za kiintelligensia.

  Kwa mara nyingine tena watawala wanaingia woga na kuweweseka wakiwafikiria CDM. Kwa nini CDM wawe chanzo cha vurugu? Watu Wa-Mbeya wavuruge amani yao wenyewe?

  Au wanataka yarudie ya tarehe 5 January huko Arusha?
   
 2. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wanataka watu wafe tena.
   
 3. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nilikua nahisi kitu kama hicho kitatokea. Kuna thread ilidokeza tetesi hizo kama siku mbili zilizopita. Jamaa waliojivua magamba wanahofia wasichunwe ngozi.
  Chadema wameamuaje? Tuhabarishe pliiz.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kama ni kweli Kazi ya Shitambala inaonekana!
   
 5. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  CDM walipewa kibali cha maandamano ? kama hawakupewa basi RC yuko right kwani ndio boss wa mkoa
   
 6. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  RPC hana mamlaka ya kutoa kibali. Na yeye haombwi kibali bali anapewa taarifa.GB wewe uko katika karne gani? Ama kweli Watanzania wengine hawajijui kama wapo Tanzania.
   
 7. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Kwnn haya yanatokea?? Mimi inanigusa hakuna mfano. Cjui nijinyonge,Naombeni ushauri wenu plz!
   
 8. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Jana Regia Mtema alikua anatuhabarisha hapa jamvini kuwa maandalizi yote yako tayari. Kwangu mimi maandalizi makubwa ya maandamano ni pamoja na mchakato wa vibali, hivyo nilitarajia hilo lisiwe tatizo. Labda kwa kuwa ni sababu za "Kiintelijensia"

  Hata hivyo kama alivyosema Gurtu, RPC haombwi kibali bali anataarifiwa ndani ya saa 48 kabla ya muda wa kuanza maandamano, ili atoe ulinzi kwa waandamanaji. Sasa inaonekana hawa watu wamegeuza neno taarifa kuwa maombi na kujifanya kuwa wao ndio wenye mamlaka ya mwisho.

  Yote kwa yote huyo RPC ameagizwa afanye hivyo kama ambavyo aliagizwa Andengenye.
   
 9. F

  Froida JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Tungoje viongozi wa Chadema watatujuza,maandamano ni haki ya watanzania kama wanataka ya Uganda yaje hapa nchini wazuie maandamano ninavyo wajua watu wa Mbeya wale akili zao wanazijua wenyewe
   
 10. L

  LAT JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0


  Kama kawaida yako ...kudandia dandia .... unasoma mada kwa ushabiki .....mwambie muajiri wako mpya BW. Mukama akufundishe tofauti ya RC na RPC
   
 11. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ahaaaaaah, aise kumbe watu wanadandia hawajui wasemalo.
   
 12. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Unajua Tanzania sheria inasema kitu tofauti na mambo yanatendwa tofauti. Fikiria sheria inasema Chama cha Siasa kinapotaka kufanya mkutano au kuitisha maandamano kitoe taarifa kwa maandishi (siyo kuomba ruhusa) kwa kamanda mkuu wa polisi wa eneo husika katika muda usiopungua saa 48. Kama CDM wametoa taarifa kadiri ya matakwa ya sheria, na mpaka siku ya mkutano au maandamano inafika ndo polisi wanaibuka na taarifa za kiintelijensia, kasoro ipo kwa nani? Bahati mbaya kwa yale yaliyotokea Arusha, polisi hawakutoa kizuio kwa maandishi bali aliibuka mtu mwingine anayazuia kwa kutumia TV(siyo maandishi) na wala hakuwa kamanda wa polisi wa eneo husika. Hivyo, Tanzania bado mambo hayajakaa sawa.
   
 13. W

  WildCard JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mambo kama haya ndio yanaifanya CHADEMA ionewe huruma na kila mtu. Ipendwe sana. Serikali hii kweli ni ya CCM? Kuna kila dalili kwamba vyombo vya dola vimeichoka CCM. Ngoja waisaidie CCM kuanguka haraka.
   
 14. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #14
  May 5, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,198
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Nilidokeza kuhusu uwezakano huo siku mbili zilizopita. Hata hivyo jana nilihudhuria japo kwa kuchelewa kikao cha CDM Mbeya mjini kikwa chini ya Mh Wilfred Lwakatare tukahakikishiwa kuwa RPC ameruhusu maandamano japo kwa masharti, sasa huyu Mwakipesile amepata wapi hizo Intelijensia? Ndio maana tunasema hakuna haja ya wakuu wa Mikoa maana kazi ni kuibeba CCM
   
 15. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #15
  May 5, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,630
  Likes Received: 1,386
  Trophy Points: 280
  watuambie hizo sababu za kiintelijensia ni zipi
   
 16. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #16
  May 5, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Nimeongea na Regia kwa simu sasa hivi akiwa njiani kuelekea Mbeya, anasema wao kama squad ya Uongozi hawana habari na taarifa hizo,wanaendelea na safari yao, na niweke wazi kuwa imemshitua kidogo nilipomuuliza.
  Sijui Kiongozi MsandoAlbert kapata wapi taarifa za tetesi hili!
   
 17. W

  WildCard JF-Expert Member

  #17
  May 5, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Ni RPC sio RC. All in all huu ni ujinga tu. Maandamano kama haya yamefanyika kungine Tanzania. Huko Mbeya kuna nini?
   
 18. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #18
  May 5, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Tanzania will continue to perish under the control of these tyrannts .Do we still have a democracy when we ignore the will of the people only to pander to the selfish will of the few??
  We should not tolerate a repressive regime that cant stand freedom of Expression.
   
 19. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #19
  May 5, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Yana mwisho haya
   
 20. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #20
  May 5, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wametishwa na kushtushwa mno na hii habari, lakini hawajui ndiyo kwanza wanakoleza!!!!!!

  Egypt's ex-interior minister sentenced
  Habib al-Adly, the face of the crackdown on pro-democracy protesters, convicted for money laundering and profiteering.  Egypt's former interior minister, Habib al-Adly, has been sentenced to 12 years in jail for money laundering and profiteering, according to judicial sources.

  Habib al-Adly, hated for the brutality of his police by the protesters who ousted President Hosni Mubarak in February, is one of the most senior Mubarak-era ministers to be put on trial.

  His conviction in a Cairo court - coming as Mubarak and his sons are being quizzed for abuse of office - highlights the desire of the generals who now rule Egypt to show their commitment to cracking down on abuse of power and corruption.
  Al Jazeera's Rawya Rageh, reporting from Cairo, said the charges were "really at the heart of the request by the protest movement; protesters had been urging the prosecution of these men - former regime officials - in what has been described as a cleansing campaign of state institutions".

  "This is going to be welcomed by the protest movement," said our correspondent.

  "But still the country's new military leaders despite [their] attempts to bring back the money that was squandered by these men, and to hold these officials acountable, they're still being criticised for moving a little bit too slowly for the protesters' taste."

  Al-Adly has been accused of selling land to an interior ministry contractor "illegally and received more than $700,000 dollars in kicks", our correspondent said.

  "On Thursday the judge ordered that amount confiscated and also ordered the former interior minister to return more than $2.3m that he had illegally acquired in just three months before the revolution [which toppled Mubarak," she said.

  "He was interior minister for 14 years and despite repeated campaigns against him by activists over a lot of accusations and not least of which is brutality and overseeing systematic torture al-Adly was never questioned and managed to retain his position for all these years."

  Many Egyptians had been closely watching the fate of Adly, one of the most controversial members of the administration of Hosni Mubarak, because of the crackdown by his police force during the uprising.

  Abdallah Schleifer, professor emeritus at the American University in Cairo, told Al Jazeera from London that the charges people are more concerned about involved ordering "security forces to open fire on unarmed demonstrators".

  Schleifer said the former minister was "responsible for setting up snipers", adding that "basically the charges he has yet to stand trial for are far more serious".

  Source:
  Al Jazeera and agencies
   
Loading...