Hii si mara ya kwanza suala hili kusemwa humu jamvini kuhusu kutowajibika kwa kitengo cha Habari cha CHADEMA. Ama ni kwa uzembe wa makusudi, au ni wa bahati mbaya, yaliyotokea jana kuhusu maandamano ya Mbeya ni uthibitisho tosha wa kutowajibika huko.
Taarifa ya maandamano imeletwa humu mapema sana, kupitia Mh. Mbunge Regia kama ilivyo ada, ikawa kusubiria picha na maendeleo (updates) ya nini kinaendelea,lakini badala yake haikuwa hivyo. Kilichotokea ni watu kusikiliza kila aina ya habari (ama za uzushi, ama za kweli, propaganda) kuhusu nini kilikuwa kinaendelea Mbeya, hadi mwishoni sana baada ya huo mkanganyiko wa maelezo, ndipo zilipoletwa picha, ambapo hata hivyo, hapajaletwa issues zilizojadiliwa katika mkutano na maandamano hayo.
Kwa dunia ya sasa inayoamini zaidi katika habari, tena zinazotolewa kwa muda husika, ni aibu kwa Chama kama CHADEMA kutotumia forum kama hii kuweka matukio na habari zinazojiri kama maandamano hayo. Habari imeshakuwa hitaji mojawapo la muhimu katika maisha ya watu kuwafanya watambue kinachoendelea katika maisha yao na mazingira yanayowazunguka. Habari ni nyenzo muhimu katika kufanya maamuzi sahihi,kujua ukweli na uongo, na mengine mengi.
Kuwahabarisha watu ni mojawapo ya wajibu mkubwa kwa kiongozi au viongozi ili kuonesha uwajibikaji wao kwa uwazi. Na wanaoongozwa wana haki ya kupata habari kwa viongozi wao kama njia ya kufahamu viongozi wao wanawajibika vipi. Kushindwa kulishughulikia suala hili, ni faulure ya utekelezaji wa jukumu mojawapo la uongozi ambalo ni kuwajulisha watu unafanya nini. Kwa mtindo huu, ipo siku CDM itashindwa kuwahabarisha watu kuhusu mambo makubwa zaidi yanayohitaji utekelezaji wa haraka zaidi.
Wakati duniani kote watu wanaendelea kuhangaikia uvumbuzi wa njia mbalimbali zilizoboreshwa zaidi kuhusu namna ya kupashana habari, kwa kuwa habari imeonekana kuwa silaha yenye nguvu ziadi katika kufanikisha masuala anuai, wengine wamelala usingizi kwa kutegemea kuwa 'watu watajua tu'! Tujifunze kwa wenzetu ambao kwa kupashana habari, wameweza kuleta mapinduzi makubwa, yawe ya kijamii,kisiasa au kiuchumi.
Ni aibu kwa CDM kutolitilia maanani suala hili.Mdharau mwiba.....