Dumelambegu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 1,052
- 260
Wakuu,
Kuna baadhi ya 'vichwa ngumu' humu jamvini wanaotaka kuleta tafsiri mbaya juu ya maandamano yanayoendeshwa nchi nzima na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Ninachojua mimi ni kwamba chadema imetoa fursa kwa wananchi wanyonge wa nchi hii ya kujitokeza hadharani na kuonyesha hisia zao kwa serikali ya kutoridhika namna nchi inavyoendeshwa na Serikali ya CCM.
Wananchi badala ya kukaa vijiweni na wengine wakinung'unika mioyoni mwao wakifura kwa hasira, sasa kupitia chadema wanapata fursa ya kujitokeza hadharani na ku-release tension wakiwa na mabango yenye maneno yanayobainisha hisia kali dhidi ya watawala wao (siyo viongozi wao).
So, ningekuwa kiongozi wa chama cha magamba in a way ningeunga mkono maandamano kwani yanasaidia kupunguza hasira ya wapinzani wangu.
Kwa upande mwingine pia, chama cha magamba (nasikia yameanza kunuka) kingekuwa kinaongozwa na great thinkers kisingebeza hata kidogo ujumbe unaotolewa kwenye maandamano hayo.
Hii ni kwa sababu wanaojitokeza kwenye maandamano unaweza ukashangaa kwamba wengi wao siyo wanachama wa chadema kwa maana ya kuwa na kadi ya chadema.
Kwa hiyo, jambo muhimu lingekuwa ni kujiuliza kwa nini wanaojitokeza kwenye maandamano ni wananchi wengi kiasi hicho! Kulikoni!
Mimi nawapongeza sana viongozi wa chadema kwa kazi nzuri ya kuhamasisha wananchi wanyonge wa nchi hii kuonyesha hisia zao.
Kama ccm haioni nguvu ya umma kwenye maandamano hayo, basi hilo ni sikio la kufa. Hatuhitaji kupoteza muda na fedha yetu kutafuta dawa.
Shime wanaJF tuendelee kuhamasisha umma kukikataa chama cha magamba ili nacho kikae pembeni. Vinginevyo, wananchi (siyo nchi) wataendelea kuwa maskini milele.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
Aluta Kontinua, Mapambano Hayana Budi Kuendelezwa Mikoa Yote ya Nchi Hii Mpaka Kieleweke!!!