SI KWELI Maandamano ruksa au fiksi za AI?

SI KWELI Maandamano ruksa au fiksi za AI?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Wajameni hii ni AI ya RC wa Dar Chalamila, inayosambaa mitandsoni?
Au?

1782393255611.png
 
Tunachokijua
Madai

Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kumekuwa na video inayosambaa ikimuonesha mkuu wa Dar es salaam Albert Chalamila akisema kuwa maandamano ni ruksa kuandamana ila watu waandamane kwa amani na hata hivyo Rais Samia pia ameruhusu maandamano hayo.

"Kwa hiyo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja pia na viongozi wote, wamesema waache watu waandamane wafikishe ujumbe wao panapostahili." - Chalamila

Video hiyo imeambatanishwa na ujumbe unaosomeka;

"Samia amesema acha watu waandamane 7/7 wafikishe ujumbe wao"

Uhalisia wa video hiyo

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejirirdhisha kuwa video hiyo ni halisi na maneno hayo pia yalizungumzwa na kiongozi huyo.

Je, ni video ya hivi karibuni? Alikuwa akiongelea maandamano ya 7/7?

Video hiyo ilirekodiwa katika maandamano ya chama cha demokrasia na maendeleo mwaka 2024 ambapo Albert Chalamila alikutana na waandamaji hao na kuwapa ujumbe huo. Ambapo video hiyo ilichapishwa na vyanzo mbalimbali ikiwemo Chanel za Youtube.

Chaneli moja ilichapisha video hiyo Januari 24, 2024 na ujumbe uliosomeka;

"Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amekutana na baadhi ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) eneo la Mbezi wakijiandaa kwa maandamano.

Kabla ya kuanza kwa maandamano hayo, Chalamila amewaomba kutunza amani kwa kuwa Jiji la Dar es Salaam lina kila kitu zikiwamo huduma za afya na mzunguko wa biashara hivyo kila mmoja anapaswa kulinda amani."


Maandamano ya 2024 yalikuwa yanahusu nini?

Chadema walifanya maandamano kwenye mkoa wa Dar es alaam yenye ujumbe wa kutaka mabadiliko ya sheria ya uchaguzi, kupunguza gharama za maisha na kushinikiza kuwepo kwa katiba mpya.

Taarifa ya Chalamila kuelekea maandamano ya 7/7

Chalamila amefanya mkutanao na waandishi wa haabri Juni 25, 2026 na kuonya wale wanaohamasisha maandamano Dar es salaam. Vyombo mbalimbali viliripoti tukio hilo ikiwemo.

Vyanzo hivyo vinaeleza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amekutana na baadhi ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) eneo la Mbezi wakijiandaa kwa maandamano.
Au ni AI? Confirm JF please

Hii video inamuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akisema Rais Samia amesema watu waache waandamane na wafikishe ujumbe wao.

Je hii video ni ya lini kihualisia?

 
Hiyo ya zamani ambayo hats yeye alishiriki na Muliro waloshiriki. Ya sasa hivi amesema itatumika nguvu mara mia zaidi ya ile ya 29.10.2025 kuyazuia.
 
AI anasema hivi:-

Hii video inamwonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, akizungumza kuhusu kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan kuruhusu maandamano ya amani (hasa yale yaliyokuwa yamepangwa na chama cha upinzani cha CHADEMA).

Hotuba hii alitoa mnamo Januari 2024, kuelekea maandamano ya CHADEMA yaliyofanyika tarehe 24 Januari 2024 jijini Dar es Salaam.

Ingawa maandishi kwenye video yanataja tarehe "7/7" (Saba Saba), muktadha halisi wa hotuba hii ya Chalamila kuhusu kuruhusu maandamano na maridhiano ya kisiasa unatokana na matukio ya mapema mwaka huo (Januari 2024).
 
Back
Top Bottom