Maandamano Kumpinga Kikwete

Mbona leo unakwenda kinyume nyume?

Nafikiri weye ndio umebehave hivi hapa!

Hapa JF wazo likianikwa, linachangiwa kutokea kona mbalimbali.
Walioko kinyume na mada hawalazishwi kukaa kimya.Hata kuonyesha tofauti ya mawazo ni mawazo.
Cha msingi acha tuipeleke mada vyovyote, kwani kuna wanaotuelewa.
Tukiendeleza kubishana, tutapoteza lengo la uwanja huu.

Hakuna mtu anakataza kuijadili hoja kwa mtazamo hasi, lakini kama unaweza kufanya hivyo basi utoe hoja za msingi za kukisupport unachokisema.....! Kwa mfano,hao wanaompinga JK wanasababu zao....sasa na wewe kama unamuunga mkono basi toa sababu za kufanya hivyo ili na wengine waweze kupima na kuamua either kumpinga au kumuunga mkono muungwana!
 
Lini wana JF tusioridhishwa na utawala wa JK tutashika mabango na kuandamana kuupinga utawala huu ulioshindwa kufanya kazi tukimtaka aondoke pale magogoni? Aachie ngazi.
Kaniki ndugu yangu, unakuwa kama ile nguo ya zamani bana.

enewei Idea Kuntu ila fahamu kupanga ni kuchagua
 
Lini wana JF tusioridhishwa na utawala wa JK tutashika mabango na kuandamana kuupinga utawala huu ulioshindwa kufanya kazi tukimtaka aondoke pale magogoni? Aachie ngazi.

Kaniki,
mawazo yako ni mazuri,
Lakini sina kumbu kumbu kama kunamaandano yoyote ambayo yamewahikuleta matokeo wazi chanya ya kisiasa katika nchi yetu.

Nikikumbushwa nitashukuru.
Emma.
 
Naona bora utafute nauli ukamuone Mjomba. Lakini pale mlangoni jamaa wanapiga sana uwe muangalifu. Maandamano hayatakufaa.
 
Hivi huoni kuwa wewe ndiyo unaongea tu na hufanyi vitendo?

ulitakiwa uje hapa na ushahidi kuwa umeandamana kupinga utawala wa JK, don't waste your time kwa kubishana hapa kwenye forum, nenda ukaombe kibali kwa Kova haraka tu.

Jamaa yuko Kigoma. akaombe kibali kwa Kova!!!!
 
Lini wana JF tusioridhishwa na utawala wa JK tutashika mabango na kuandamana kuupinga utawala huu ...

Huoni kama maandamano pia yaweza kuwa njia nzuri ya kuhamasisha asipigiwe kura 2010? i...

Ukiitisha maandamano ya wana JF, trust me utajikuta wewe, Invisible, Zitto, Slaa, Mbowe, Mkumbo, Mnyika, Kahangwa, Mrema, Lipumba, Seif, Halisi, Mpita Njia, Uwiano Maalum na wengine wachache.

Afadhali uite maandamo ya wananchi wote; kama ni ya wanaJF pekee hiyo haitatimia, hata tukibeba mawili mawili, kuna baadhi ya mabango yatakakosa wabebaji.

Samahani kwa niliowataja hapa, kwani nimewataja kwa mfano tu; hawajanipa idhini wala ishara kwamba wataandamana.

Aliyeko tayari kuandamana ajitaje, na orodha apewe bwana Kaniki, aiweke kwenye post yake ya kwanza, then maandamano yaandaliwe.

Kama maandamano ni ya humu ndani ya nyumba sawa kabisa!Hayo ya huko katika miji na majiji sijui kama kutapatikana waandamanaji.Kaniki & Co.haya...ongoza njia!
 
Ukiitisha maandamano ya wana JF, trust me utajikuta wewe, Invisible, Zitto, Slaa, Mbowe, Mkumbo, Mnyika, Kahangwa, Mrema, Lipumba, Seif, Halisi, Mpita Njia, Uwiano Maalum na wengine wachache.

Afadhali uite maandamo ya wananchi wote; kama ni ya wanaJF pekee hiyo haitatimia, hata tukibeba mawili mawili, kuna baadhi ya mabango yatakakosa wabebaji.

Samahani kwa niliowataja hapa, kwani nimewataja kwa mfano tu; hawajanipa idhini wala ishara kwamba wataandamana.

Aliyeko tayari kuandamana ajitaje, na orodha apewe bwana Kaniki, aiweke kwenye post yake ya kwanza, then maandamano yaandaliwe.

Mapema mno kuandamana.
Elimu tunayoitoa hapa inapaswa kwanza kupenya ktk mioyo ya Watanzania then hayo maandamano yataaandamana kila baada ya muda mfupi kwani sasa hivi hata polisi nao wanapaswa kuelimishwa.
Ops mawazo ya kilevi haya
 
Unakumbuka nini kilitokea South Africa last year kuhusiana na Thabo Mbeki? Unataka kuniambia wao hawakujua kuwa mwaka huu kuna Uchaguzi huko bondeni?

Mbeki aliondolewa na maandamano au chama chake? South Africa hakuna uchaguzi wa kumpigia kura mtu mmoja kupewa uraisi. Chama kina piga kampeni kikishinda wana pendekeza raisi bungeni then wabunge wanampigia kura. Kisa cha Mbeki kuondoka ilikua chama chake kumuondoa katika nafasi hiyo na wala siyo kweli kuwa wananchi waliandamana kumuondoa madarakani. Anyway siyo kuwa napinga maandamano ya JK ila nakupa facts the SA kuwa hawakuandamana kumuondoa Mbeki.
 
Mapema mno kuandamana.
Elimu tunayoitoa hapa inapaswa kwanza kupenya ktk mioyo ya Watanzania then hayo maandamano yataaandamana kila baada ya muda mfupi kwani sasa hivi hata polisi nao wanapaswa kuelimishwa.
Ops mawazo ya kilevi haya

Makonyagi,

Our time is now.......kuandamana pia ni njia ya kutoa elimu kwa tz watambue kuwa people are really serious on these issues!

BWT: Mkuu ulipotelea wapi......TDL walikufungia kny mabox ya kilaji nini (joke).......radha ilipotea ghafla hapa mkuu!
 
Kama kuandamana kushawishi watu wasimpigie kura JK mwakani sawa. Kama nilivyo sema kwenye post yangu ya kwanza kuwa kazi iwe kushawishi watu wasimpigie kura JK mwakani. Ila nikawa nasema maandamano tu halafu mwakani anapigiwa kura ina saidia nini? Kama mwakani wakimpigia kura ya kumrudisha madarakani utaandamana tena? Cha maana sasa ni kwamba 2010 siyo mbali, tuanze mapema kuandaa watu wasiipigie kura ya ndiyo utawala wa JK. Kama Kenya waiweza sisi tunashindwa nini?
 
Mbeki aliondolewa na maandamano au chama chake? South Africa hakuna uchaguzi wa kumpigia kura mtu mmoja kupewa uraisi. Chama kina piga kampeni kikishinda wana pendekeza raisi bungeni then wabunge wanampigia kura. Kisa cha Mbeki kuondoka ilikua chama chake kumuondoa katika nafasi hiyo na wala siyo kweli kuwa wananchi waliandamana kumuondoa madarakani. Anyway siyo kuwa napinga maandamano ya JK ila nakupa facts the SA kuwa hawakuandamana kumuondoa Mbeki.

Najua hivyo ndivyo ilivyokuwa, hoja yangu ni kuwa; Kama ANC walijua kuwa waliweza kumshinikiza Mbeki kuresign 1 year kabla ya term yake ya urais kuisha na wakijua wangeweza kufanya hivyo this year, kwa nini sisi tusubiri uchaguzi?

Hata kama chama chake cha sisiemu, hakitaki kufanya yaliyofanywa na ANC, sisi wananchi tunaweza kufanya yaliyofanywa na ANC kwa njia nyingine mkuu kama vile kuandamana etc!
 
Ok nimekuelewa sasa mkuu.
 
I still believe in the revolution of the vote. Kama tukiandamana bure halafu bado CCM mwakani inaingia madarakani tuta faidika vipi? Ufisadi ule ule si utaendelea tu chini ya mwingine? Cha kufanya ni kung'oa madarakani chama cha mafisadi kabisa. Tukimuondoa JK simply kumuondoa JK tu hao mafisadi ndani ya chama wata chagua tu mwanasesere mwingine kutuongoza. Ndiyo maana nikasema nguvu tuiwekeze katika kuondoa chama tawala madarakani mwakani. If Kenya na ukabila wote could do it so can we.
 
Mkuu,

You just made my day.....Wajinga ndio waliwao!!
 
I still believe in the revolution of the vote. Kama tukiandamana bure halafu bado CCM mwakani inaingia madarakani tuta faidika vipi? Ufisadi ule ule si utaendelea tu chini ya mwingine? Cha kufanya ni kung'oa madarakani chama cha mafisadi kabisa. Tukimuondoa JK simply kumuondoa JK tu hao mafisadi ndani ya chama wata chagua tu mwanasesere mwingine kutuongoza. Ndiyo maana nikasema nguvu tuiwekeze katika kuondoa chama tawala madarakani mwakani. If Kenya na ukabila wote could do it so can we.

Just for curiosity,... Mtoto akichukia au kama anadai kitu analia. Watazania kwa ujumla wao wanachukua hatua gani kama hawaridhiki na watawala wao??
 
Thailand waliandamana na kumng'a madarakani waziri mkuu na kumsikika kiongonzi wa upinzani kwa mbwembwe, lakini huyu mpya hakuchukua miezi 3 naye wakamgeuka asingetumia ubabe wa JESI angeong'oka, unaondoa JK je umesha mpata mrithi wake ambaye ni safi? vinginevyo tutakuwa tunapiga story tu as if tunataka muondoa rais wa DARUSO ?...hivi karibuni kuna nchi kadhaa zimetumia mtindo huo na kufanikiwa kuwang'o madarakani watawala, hata hivyo karibu wote wapya waliongia nao hawakukidhi matarajio....hi nikwasababu ya kukurupuka, normally kunakuwa naka tabia ya kuangalia zaidi udhaifu wa aliyeko madarakani kuliko huyo atakayerithi, mwisho wake unakuwa umebadiri chupa tu lakini mvinyo je?..Kama ni usanii, alianza Nyerere na waliomfuata. Vita vya mafisadi alianzisha Sokione, lakini je vilishia wapi baada ya shujaa huku kuaga dunia? Mafisadi yalainza ota mizizi baada ya Sokoine kuaga dunia.....Tatizo la TZ is more than JK, to be fair vyama vya siasa karibu vyote vinye nguvu vimeundwa na mafisadi with just few real men....Cabinet yetu imejaa Wasomi/ma-professor tena wa kueleweka sasa sijui nini kinatusibu ...inabidi tufanye utafiti wa kina kujua gonjwa letu....hizi kauli za maandamano sometimes zinatokana na watu kukata tamaa, na mtu akikata tamaa anaweza fukuza kipa ukaweka winger au mtu yeyote adake ()....I think cabinet nayo inatakiwa ijitume, isije kuna watu wana mtegea JK achemshe ili wao waingie kilaini...
 
Back
Top Bottom