Maandamano haya yanaweza kubadili uelekeo na kuwa sababu ya kumtoa Trump madarakani

MakinikiA

JF-Expert Member
Jun 7, 2017
5,011
6,542
MAANDAMANO HAYA YANAWEZA KUCHANGE DIRECTION NA KUWA SABABU YA KUMTOA TRUMP MADARAKANI

Melfu ya watu wamejitokeza kote New York kwa maandamano yaliyoendelea usiku kucha juu ya kifo cha George Floyd

Maelfu ya watu wamejitokeza kote New York kwa maandamano yaliyoendelea usiku kucha juu ya kifo cha George Floyd
Maandamano juu ya kifo cha raia mweusi wa Marekani George Floyd bado yanaendelea kwa usiku wa nane mfululizo.
Kifo cha Floyd kilichotokea Mei 25, mikononi mwa polisi huko Minneapolis kimesababisha maandamano makubwa katika maeneo mbalimbali nchini huko.

Waandamanaji wameamua kukiuka hatua ya kusalia ndani iliyowekwa katika miji mbalimbali.
Katika eneo la Fort Worth, Texas, inasemekana kundi dogo la watu lilisalia nje hata baada ya kuanza kwa muda wa kutoka nje saa mbili usiku.

Waandamanaji katika mji wa New York pia nao walikiuka hatua ya kutoka nje iliyowekwa kuanzia saa mbili usiku.
Meya wa mji alisongeza mbele muda huo kwa usiku wa pili mfululizo baada ya waandamanaji kupora eneo la kibiashara la Manhattan Jumatatu.

Wanajeshi wa Marekani wakiwa mitaani kuzuwia maandamano

Wanajeshi wa Marekani wakiwa mitaani kuzuwia maandamano
Na katika mji wa Washington DC, kundi kubwa la watu limeendelea kukusanyika nje hata baada ya kuanza kwa muda wa kutoka nje saa moja usiku.

Aidha, Takriban wanajeshi Taliban1,600 wamepelekwa katika maeneo ya mji wa Washington DC.

Msemaji wa serikali amesema vikosi vilikuwa katika tahadhari ya juu.

Katika jimbo la Minnesota waandamanaji wamewasilisha kesi mahakamani dhidi ya polisi kwasababu ya kifo cha Floyd. Gavana Tim Walz ameambia vyombo vya habari kwamba uchunguzi wa kifo hicho utalenga kumaliza tatizo la ubaguzi wa rangi ambalo limedhihirika kuwa sugu.

Katika Los Angeles, mabango yaliyoandika Black Lives Matter - vuguvugu lililo katika maandamano ya kupinga mauaji ya polisi dhidi ya watu weusi
Katika Los Angeles, mabango yaliyoandika Black Lives Matter - vuguvugu lililo katika maandamano ya kupinga mauaji ya polisi dhidi ya watu weusi

Mwanaume mmoja na mtoto wake wa mwaka mmoja walikua miongoni mwa waandamanaji katika jiji la Californian la Pasadena
Mwanaume mmoja na mtoto wake wa mwaka mmoja walikua miongoni mwa waandamanaji katika jiji la Californian la Pasadena

Vilevile, watu wameendelea kukutana katika mji wa Floyd, Houston, Texas, na kufanya maandamano ya amani na familia ya marehemu Floyd. Watu hadi 20,000 wanatarajiwa kushiriki maandamano hayo, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya eneo.

Roxie Washington, Mke wa George Floyd akizungumzia mtoto wao wa kike wa miaka sita aliyeachwa bila baba, Gianna, katika mkutano na wanahabari huko Minneapolis, "Gianna hana tena baba," alisema."Baba yake hata muona tena akikua, akihitimu shule, wala kumshika mkono siku ya harusi yake. Ikiwa ana tatizo lenye kumuhitaji baba yake, hayupo tena duniani.

"Niko hapa kwa ajili ya mtoto wangu na mume wangu George kwasababu ninataka haki itendeke. Ninataka haki itendeke kwasababu alikuwa mtu mzuri haijalishi mwengine anafikiria nini."

Maafisa wa usalama wakipiga goti pamoja na waandamanaji Atlanta

Maafisa wa usalama wakipiga goti pamoja na waandamanaji Atlanta

Maafisa wa polisi na jeshi wamejitokeza katika miji tofautitofauti wakipiga goti pamoja na waandamanaji kama ishara ya kuonesha mshikamano.

Katika mji wa Los Angeles, waandamanaji walikuwa wanashabikia wanajeshi pale walipopiga goti.
Waandamanaji waliwataka wanajeshi kufanya maandamano nao, lakini wakasema kwamba wanahitaji kusalia sehemu moja.

Mwandishi wa BBC Phoebe Frieze alikuwa katika kumbukumbu ya Lincoln Washington DC kabla tu ya kuanza kwa muda wa kutotoka nje saa moja jioni ambapo mamia ya waaandamanaji walikuwa wamepiga magoti mbele ya sanamu la Lincoln na kukaa kimya, huku vikosi vya taifa vilivyojihami vikiwa vimepanga mstari mbele vikitazama waandamanaji.
Barabara nyingi zinazoelekea kwenye kumbukumbu hiyo zilikuwa zimefungwa na vizuizi vya polisi na pia helicopter inayoshika doria ilisikika kwa juu.

Waandamanaji walitaja majina ya watu wengine waliokufa kwa njia tatanishi mikononi mwa polisi kama vile Tamir Rice, 12, aliyeuawa Cleveland, Ohio, 2014.

Waandamanaji walitawanywa kwa gesi za kutoa machozi muda wa amri ya kutotoka nje ulipoanza

Waandamanaji walitawanywa kwa gesi za kutoa machozi muda wa amri ya kutotoka nje ulipoanza
Ni katika ukumbi wa Lincoln mwaka 1963 ambapo Martin Luther King Jr alitoa hotuba yake maarufu ya "I have a dream" yaani nina ndoto.

Dakika 15-20 kabla ya muda wa kusalia ndani kuanza waandamanaji walianza kuondoka.

Chanzo: BBC Swahili
 
Unaandamana na mtoto, akipigwa tu kesi inazidi kuwa kubwa. Trump kaingizwa katika mtego mbaya sana, asipokuwa makini asahau Uraisi.
 
Trump atashinda tena tarehe 3 november na atarudi ofisini. Nashangaa watu mnaomuhukumu Trump kwa case za ubaguzi
Kaka yenu baraka amekaa miaka 8 amefanya nini.

Kwenye nyanja mbali mbali hapo US wapo watu weusi wamefanya nini. America for trump ni Rais wao mzuri uchumi wao upo mzuri unemployment ya chini kabisa.

Watanzania tufanye mambo yetu tuna mengi sana ya kukemea mbona
 
Ila jamii zinatofautiana Sana yaani. Hivi Kwa nchi kama yetu hii, polisi wanavyopenda kupiga watu na kutumia mabavu kila mahali sijui wangefaidi kiasi gani kupiga watu ingekuwa ni huku. Wangepiga Hadi wangechoka. Lakini hebu angalia polisi na Askari hao wa.USA jinsi wanavyojichanganya na waandamanaji

Nikiwaza polisi, serikali na hata mahakama walivyochukulia kesi ya Akwirina napata wakati mgumu Sana moyoni mwangu.

Anyways, RIP dada Akwirina.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Busara itumike tuu lasi hivyoo hayaa maandamano hayataisha leo wala kesho.
Alietaka haya maandamano yafikie hapa yalipofikia ni TURAMPET huwezi ukawatishia watu jeshi huku unadai taifa lako watu wanauhuru wakuandamana

Na hivi kashaliingiza jeshi barabarani asahau maandamano kuisha leo na kesho US wajiandae tu kisaikolojia maana hakuna namna sasa.....
 
... demokrasi ya hali ya juu sana kuwahi kushuhudiwa duniani! Hongera zao kwa kweli kwa uhuru mkubwa wa kujieleza, kukutanika, na kuonesha hisia zao. Huu ndio uhuru unaohitajika duniani.
Utahitajika sana huu uhuru mwaka huu hasa katika kipindi hiki

Mpaka Trump apige goti yeye si anajifanya mropokaji mzuri .....
 
Utahitajika sana huu uhuru mwaka huu hada katika kipindi hiki

Mpaka turampet apige goti yeye si anajifanya mropokaji mzuri .....
... tulia ujifunze how democracy is practiced; kama ulifundishwa shuleni kwenye makaratasi, shuhudia kwa vitendo. Watu wanapata uhuru wa kujumuika, kupaaza sauti zao pale wanapohisi kunyanyaswa au kuonewa, n.k. Ingekuwa kule kwingine hata hiyo video usingeiona maana cha kwanza internet ingezimwa nchi nzima na kila taarifa inayoingia au kutoka "kukaguliwa" na serikali!
 
... tulia ujifunze how democracy is practiced; kama ulifundishwa shuleni kwenye makaratasi, shuhudia kwa vitendo. Watu wanapata uhuru wa kujumuika, kupaaza sauti zao pale wanapohisi kunyanyaswa au kuonewa, n.k. Ingekuwa kule kwingine hata hiyo video usingeiona maana cha kwanza internet ingezimwa nchi nzima na kila taarifa inayoingia au kutoka "kukaguliwa" na serikali!
Yote hayo utayaona katika taifa linalojiita lakidemokrasia tuupe muda kazi yake kwanza.....
 
Alietaka haya maandamano yafikie hapa yalipofikia ni TURAMPET huwez ukawatishia watu jeshi huku unadai taifa lako watu wanauhuru wakuandamana

Nahv kashaliingiza jeshi barabarani asahau maandamano kuisha leo nakesho US wajiandae tu kisaikolojia maana hakuna namna sasa.....
Labda tungerudi nyuma kwanza sababubya yeye kuimpose jeshi ni nini? Je hata kama watu wanauhuru wa kuandamana lakin ile kuvunja magari kuchoma moto majengo n.k hiyo sio Demokrasia tena hapo kuna uharifu. Sasa hutaona tena majengo yakichomwa kiboya.

Na labda tujikumbushe tena Rais wa US anapatikanaje? Je,Sanate na Congress wanasapoti kuchoma magari na kuvunja maduka ya watu? Jibu ni Hapana. Wanachofanya akina Biden ni siasa tu lakini hakuna Rais anayeweza kuacha maandamano ya fujo kuendelea nankatika kumchagua Rais raia kura zao sio Alfa omega.
 
Labda tungerudi nyuma kwanza sababubya yeye kuimpose jeshi ni nini?Je hata kama watu wanauhuru wa kuandamana lakin ile kuvunja magari kuchoma moto majengo n.k hiyo sio Demokrasia tena hapo kuna uharifu.Sasa hutaona tena majengo yakichomwa kiboya.
Na labda tujikumbushe tena rais wa US anapatikanaje?Je,Sanate na Congress wanasapoti kuchoma magari na kuvunja maduka ya watu? Jibu ni Hapana.Wanachofanya akina Biden ni siasa tu lakini hakuna rais anayeweza kuacha maandamano ya fujo kuendelea nankatika kumchagua rais raia kura zao sio Alfa omega.
Yes

Katika hali ambayo ilikuepo RAIA walikua wana munkari nahasira katika jambo ambalo limetokea

Alichotakiwa kufanya TRUMP nikama ugomvi wafamalia (NDANI YA US) ikitokea katumia jeshi watakao umia niwa US

Alichotakiwa kufanya TRUMP angehubiri kwanza amani na meza ya DUARA watuwakae chini wayamalize

Yeye anatokea anapotoka anatishia watu jeshi (baada yakutishia watu jeshi maandamano yameisha ?! Nakama hayajaisha nini khatma yake ?)

Hali halisi ya US inaeleweka raia wengi wana silaha ikitokea raia wakaenda kama wanavyopelekwa wategemee nini?!


Upande mwengne ila huu naugusia tu nje ya mada husika-HONG KONG yalitokea maandaman kama haya fujo vurugu kauli ya US kuhusu maandamano ilikuaje ?!


Mwisho:- kiburi cha DT kinaweza kikafanya Huu mzozo usimalize kwaharaka nawakati wao wanamizozo yao shughuli nyingi zakiuchumi kijamii nahata zakisiasa zinazorota wanapoteza pesa mingi wakati huo wenzake wanatembea aache ujuaji mzee awe mpole pia kuhusu hao wengine mnaosema kama siasa je kama taifa kubwa nalakidemokrasia kama US limefikia huko kutia siasa katika mambo yamaana wanawafundisha nini wanaowaita hawana demokrasia ilio komaam...
 
Back
Top Bottom