Maandalizi muhimu kabla ya uchaguzi ili kuepuka kusema umeibiwa kura Chama chako kinaposhindwa

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,603
Hii ni kwa vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi ,uwe uchaguzi mdogo, uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu. Kila chama ni muhimu kufanya maandalizi ili kuepuka kutupa lawama kusikostahili.

Kwanza, Kila chama kinatakiwa kihakikishe kina wanachama wafia chama ambao watakuwa pamoja na Chama nyakati zote. Mtaji wa wanachama wafia chama ni hakikisho sahihi la chama kushinda kirahisi.

Pili, Kila chama kihakikishe kinakuwa na mpangokazi wa muda mrefu wa mipango, mikakati na mbinu za ushindi. Chama kushiriki uchaguzi bila kuwa na mpangokazi wa ushindi ni kufanya jaribio la kushindwa.

Tatu, wakati wa kampeni Kila chama kijielekeze kwenye sera na sio lawama Kwa sababu unapotumia muda mwingi kulaumu utakosa muda wa kutangaza sera.

Nne, ahadi zinazotekelezeka. Wapigakura wanatamani kusikia na kuahidiwa vinavyotekelezeka hata kama Ahadi zisizotekelezeka zinaweza kuwa tamu zaidi. Kwa mfano, mmoja kuahidi watu kusema Bure mpaka chuo kikuu na mwingine kuahidi watu kusoma Bure Hadi kidato Cha nne, atachaguliwa aliyeahidi kusomesha Bure Hadi kidato Cha nne hata kama kusomeshwa Bure Hadi chuo kikuu ni vizuri zaidi lakini utekelezaji wake sio rahisi.

Tano, Kila chama kihakikishe wanachama wake wenye umri wa kupigakura wameandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapigakura. Kuwa na wananchi wengi lakini hawaandikishwa ni kazi bure maana hawatakuwa na uwezo wa kupiga kura.

Sita, Chama kisimamishe wagombea wanaouzika kirahisi ili iwe ni rahisi kuwanadi wakati wa kampeni. Wagombea wenye kashfa za rushwa, ufisadi n.k itahitaji kusafishwa kwanza ili wanadiwe. Kipindi cha kampeni ni kifupi kufanya yote hayo.

Saba, Kila chama kihakikishe kinaweka mawakala wa kusimamia upigaji na kuhesabu kura.

Nane, vyama vinavyoshindwa vikubali kushindwa na kusonga mbele, warekebishe kasoro zilizopelekea kushindwa na wajipange vema Kwa uchaguzi ujao. Kukaa miaka mitano unalalamika umeibiwa kura, inakufanya uoneshe udhaifu mkubwa ulionao wa kutokukubali matokeo na Hilo litapelekea kushindwa kesho na kesho kama usipoweza kurekebisha.
 
CCM Ina mbinu 36 za kuiba kura na uchaguzi.
*Mbinu na. 24: baada ya kuona mgombea wa ccm amepata kura chanche kuliko wa upinzani na wafuasi wa upinzani wamepandwa na midadi kweli kweli huku wakiimba na kucheza .

Mkurugenzi anajitokeza akiwa kazungukwa na polisi anawataka watulie, watawanyike ili taratibu za kutangaza matokeo zifanyike. Hivyo anawasihi wafuasi warudi hapo ofisini kesho asubuhi na mapema kusikiliza matokeo.

Halafu kwa makusudi kabisa mkurugenzi anatangaza matokeo saa 6 za usiku mbele ya kamera na microphone moja tu ya TBC1.
 
Hizi mbwembwe umeweka hapa wala sio zinazotoa mshindi kwenye chaguzi zetu kwa sasa. Kinachoendelea kwenye chaguzi zetu ni tofauti na hizi nadharia zako. Na kama hizi nadharia zako zingekuwa zinafuatwa kwenye chaguzi zetu, leo hii ccm isingekuwa madarakani.

Katafute watu wajinga ndio uwaambie hizi porojo zako, maana kinachoendelea kwenye chaguzi zetu tunakifahamu, na ziko wazi mno. Siku za nyuma mlifanikiwa kuongopea watu kuwa hayo uliyoweka ndio huleta ushindi, lakini hayo yote yamefanyika na tunachokiona kwenye box la kura ni vitendo vya aibu, na vinatia kinyaa. Hii ndio imepelekea watu kulipuuza box la kura maana imekuwa ni kupotezeana muda.
 
Back
Top Bottom