Maana ya Vitendo vya Rushwa, Ubadhirifu na Udanganyifu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Kwa mujibu wa “Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa na Mpango wa Utekelezaji wa Awamu ya Tatu 2017-2022 (NASCAP III)”, vitendo vya rushwa vinatafsiriwa kuwa ni kutoa, kupokea au kushawishi moja kwa moja kutolewa au kupokelewa kwa kitu chochote cha thamani kwa maslahi au matumizi binafsi, ili kupindisha utaratibu uliopo katika utoaji wa maamuzi, au kupata faida ya kitu au jambo ambalo hakustahili.

Rushwa ni jambo ambalo limejadiliwa na kuwekewa mikakati katika ngazi mbalimbali za kidunia, kikanda na hata katika nchi moja moja. Kwenye Ajenda 2063 ya Afrika Tuitakayo, Lengo namba 3 inalenga kuwa na Afrika yenye utawala bora, demokrasia, inayoheshimu haki za binadamu, usawa na utawala wa sheria.

Kwa mujibu wa Viwango vya Kimataifa vya Ukaguzi, “ISA 240, ISSAI 1224, pamoja na ISSAI 1315” udanganyifu na ufisadi vinaelezwa kuwa ni “kitendo au vitendo vya makusudi kinachofanywa/vinavyofanywa na watu au mtu kwa ajili ya kupata faida binafsi kwa njia haramu au isiyo ya haki”.

1689148990524.png

Ripoti ya Tume ya Rais ya Kupunguza Kero za Rushwa (1996), ilibainisha namna rushwa inavyoweza kujidhihirisha kupitia njia kuu mbili ambazo ni:

Rushwa katika Mifumo ya Utawala (Rushwa Uchwara)

Hii inatokana na watumishi wa Serikali na mawakala kudai rushwa wakati wa kuhudumia wananchi. Taarifa hiyo imeeleza kuwa aina hiyo ya rushwa uchwara inasababishwa na viwango vidogo vya mishahara vinavyotolewa kwa wafanyakazi ambavyo havikidhi mahitaji yao.

1689149056147.png


Rushwa Kabambe (Rushwa Kubwa)
Aina hii ya rushwa imebainishwa kuhusisha viongozi wa ngazi za juu Serikalini, wenye mamlaka ya kutoa maamuzi kupitia sera na mikataba. Taarifa hiyo ilibainisha kuwa, sababu kubwa ya rushwa hiyo ni ulafi uliokithiri na tamaa ya kujilimbikizia mali.

1689149127204.png

Vigezo Vilivyotumika Kubainisha Viashiria vya Rushwa, Ubadhirifu na Udanganyifu

Katika uchambuzi wa ripoti za CAG za mwaka wa fedha 2021/22, yapo maeneo ambayo yanaonesha uwepo wa viashiria vya rushwa, ubadhirifu na udaganyifu katika usimamizi wa rasilimali za umma. WAJIBU imetumia vigezo vifuatavyo kuainisha maeneo hayo:

1. Mapato kutopelekwa benki,
2. Kukosekana kwa hati za malipo,
3. Kwenda kinyume na sheria, kanuni na taratibu za usimamizi wa rasilimali za umma,
4. Malipo ya huduma na bidhaa ambazo hazijatolewa au hazijapokelewa,
5. Matumizi mabaya ya nafasi au cheo,
6. Kupokea huduma au bidhaa isiyo sahihi au ambayo haikukidhi mahitaji,
7. Huduma au bidhaa iliyo chini ya kiwango,
8. Kupokea huduma au bidhaa mbadala bila makubaliano halali,
9. Miradi ya maendeleo iliyochelewa kukamilika, iliyotekelezwa kwa viwango vya chini au miradi iliyokamilika lakini haitumiki kwa kipindi kirefu, na
10. Makusanyo yaliyofanyika nje ya mfumo wa GePG.


Kwa kutumia vigezo vilivyoainishwa hapo juu, ripoti za CAG za mwaka wa fedha 2021/22, zinaonesha kuwepo kwa mambo mbalimbali yanayoashiria vitendo vya rushwa, udanganyifu na ubadhirifu kama yalivyochambuliwa katika ripoti hii.
 
Back
Top Bottom