kwa kweli ambao wamewahi kuishi na waswahili mathalani katika mwambao wa pwani hususani mombasa kenya utapata kuna kiswahili aina flani hutumiwa cha kuchakachua karibu kila sentensi..kwa mfano jamaa wakisema wewe ni MTI wanamaana kuwa wewe ni shujaa,shupavu umekomaa kwa fani flani lakini hapo tena utapata mwingine anasema usiniite mti.kwa kuwa mti hupandwa,hutiwa maji,huparagwa,hukatwa ambapo katika kiswahili cha mtaa pwani ya kenya hayo nliotaja kuhusu mti hutumiwa kama matusi.hivyo ndivyo kiswahili huchezewa katika jamii tofauti..kwa kumalizia chukulia neno shoga.kwa wabongo ni rahisi kuita mwenzio shoga wangu kumaanisha rafiki yangu.hebu kenya jaribu kuita rafiki yako hivyo.kitakachotokea sijui.nawasilisha.