MAANA YA JINA "JEMBE" ni ipi hasa?

Vitendo

JF-Expert Member
Oct 23, 2009
582
103
Wadau naomba mnisaidie maana ya jina JEMBE ..maana kuna kisa kimetokea juzi na nashindwa kupata jibu.
Kisa kilikuwa hivi;
."aah usiniite JEMBE tena,mie sio jembe..JEMBE lina tobo na hutiwa mpini"nimemsikia jamaa akilalamika..je utakubali mshkaji ako akikuita JEMBE ?
 
Mi najua maana mbili tu za neno JEMBE,maana ya kwanza ni mtu mshamba mgeni wa town na maana ya pili ni mtu shupavu,mpiga kazi wa kutegemewa.Mheshimiwa spika naomba kuwasilisha hoja.
 
jembe ni aina ya kivumish cha sifa yan ni mtu shupavu ,ni mtu ambaye anafanya kaz kwa umakini
 
for sure maana ya jembe ni mtu anae toka kijiji..! auuuuuu! ila nilikua napita tu msinifkirie vibaya
 
kimjinimjini jembe ni mtaji(pesa).huwezi kufanya biashara kama huna jembe.maana nyingine ni mtu shupavu.kijijini jembe ni kifaa kinachotumika kulimia.mia
 
Mie nafahamu JEMBE kama kifaa kinachotumiwa katika shughuli zakilimo, hususani na wakulima wadogowadogo ambao hutumia kilimo cha mkono.
 
any hard working guy...kwa aspect yoyote!!ni kati ya maneno yanayojitokeza ktk jamii kwa msim fulani, na kupita.
 
Ni msimu, ambao niuelewavyo mimi jembe ni mtu unayeweza kumuamini na kumtegemea kama vile ambavyo mkulima hupata kipato chake chote kwa kutegemea jembe jatika kilimo.

Ni kama "bestfriend" hivi. huyo aliekataa kuitwa hivo kwa madai eti jembe lina tobo ni wale wenye mawazo yaelekeayo upande mmoja tu. yaani kila neno atataka aligeuze tusi.
 
Jembe ni kama essien enzi zile...namnukuu morinyo akimsifia kwamba anaweza kucheza dk 90 hata kama ni majeruhi...na bado akapangwa mechi ijayo
 
kwa kweli ambao wamewahi kuishi na waswahili mathalani katika mwambao wa pwani hususani mombasa kenya utapata kuna kiswahili aina flani hutumiwa cha kuchakachua karibu kila sentensi..kwa mfano jamaa wakisema wewe ni MTI wanamaana kuwa wewe ni shujaa,shupavu umekomaa kwa fani flani lakini hapo tena utapata mwingine anasema usiniite mti.kwa kuwa mti hupandwa,hutiwa maji,huparagwa,hukatwa ambapo katika kiswahili cha mtaa pwani ya kenya hayo nliotaja kuhusu mti hutumiwa kama matusi.hivyo ndivyo kiswahili huchezewa katika jamii tofauti..kwa kumalizia chukulia neno shoga.kwa wabongo ni rahisi kuita mwenzio shoga wangu kumaanisha rafiki yangu.hebu kenya jaribu kuita rafiki yako hivyo.kitakachotokea sijui.nawasilisha.
 
Ni msimu, ambao niuelewavyo mimi jembe ni mtu unayeweza kumuamini na kumtegemea kama vile ambavyo mkulima hupata kipato chake chote kwa kutegemea jembe jatika kilimo. <br />
<br />
Ni kama &quot;bestfriend&quot; hivi. huyo aliekataa kuitwa hivo kwa madai eti jembe lina tobo ni wale wenye mawazo yaelekeayo upande mmoja tu. yaani kila neno atataka aligeuze tusi.
<br />
<br />

Nami ndo navoelewa, jembe ni sawa na kusema mwana, hommie, mshikaji, mkuu, mchizi wangu nk
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom