Maana ndani ya picha - njoo tutafute maana

?
IMG_20211203_121150_686.jpg
 
Kwa mara kadhaa nimekuwa nikikutana na picha au michoro mbalimbali ambayo wakati fulani ni vigumu sana kuelewa maana yake. Karibu na wewe uweke picha ambayo unadhani mpaka leo imekusumbua sana kuielewa au haujaielewa.

Wadau tusaidiane kutafuta maana...Mimi nitashare kadhaa kuanza na hii hapa View attachment 2030550
hatua za kujiua ua n nguvu inayotoka nje na kuanza kuharbu ndan pole pole mwshowe utimza adhma yako
 
Maoni yangu:
Naiona hii kama madhara ya 'self-solation na self-absorption' inayo changiwa au kusababishwa na technology.

Mtu anakuwa na ukaribu na jamii ya mtandaoni lakini physically hana ukaribu na mtu. Anajikuta mpweke ingawa yuko 'connected' sana tu online (labda ana followers kibao, threads anazoshiriki jf, etc). Jamii iliyomzunguka huyo kijana imewakilishwa na hayo 'madudu'. Iwe ni nduguze, jamaa, marafiki, nk, wanajaribu ku'connect' naye ila hawafanikiwi. Kisaikolojia amejitenga nao kiasi kwamba kwake hawana sura zao halisi tena, anawaona kama ni viumbe flani hivi vinavyomzingira na kumzingua. Sura za hao viumbe zimejaa huzuni Hili naliona likioneshwa kwa jinsi wote wanaelekea direction moja, wakimsindikiza aendako ingawa yeye 'anawachukulia poa'. Mwsiho wa siku hakuna aliye na furaha.

Kwa urahisi wa kurelate, huenda kuna baadhi yetu humu wenye ndugu wa karibu (kaka, dada, etc) ambaye yeye ni kutwa na simu yake hata hawezi kuongea nae wakaelewana.
 
Sasa mjumbe kwa hali hii si tutabasti vichwa maana hatujatafakari hii unabandika nyingine

Hapo nimeipenda hiyo ya akina sayari wanamshuhudia mjumbe mwenzao akiwa taabani kitandani nao wasijue wanamsaidia vipi (na ndiyo niliyoielewa pekee)
 
Sasa mjumbe kwa hali hii si tutabasti vichwa maana hatujatafakari hii unabandika nyingine

Hapo nimeipenda hiyo ya akina sayari wanamshuhudia mjumbe mwenzao akiwa taabani kitandani nao wasijue wanamsaidia vipi (na ndiyo niliyoielewa pekee)
Kila moja anaweza kuwa ameielewa moja tofauti na mwenzake...Sio kwamba wote tunatafakari picha moja...wewe umeielewa hiyo ya sayari kuna wengine wamezielewa nyingine....na wengine watazielewa nyingine watusaidie maana.
 
Back
Top Bottom