Patra31
JF-Expert Member
- Apr 24, 2020
- 6,934
- 13,954
😂😂😂 Ebu angalia tena kwa umakiniWote ni wafungwa lakini mmoja ni nyampala
😂😂😂 Ebu angalia tena kwa umakiniWote ni wafungwa lakini mmoja ni nyampala
Ujinga mzigo
Hii picha nimeipenda kwa sababu naona ujumbe wake uko wazi ila kwa haraka haraka mtu anaweza kuukosa.Ni kama huyu jamaa ana rasilimali lakini hajui kuzitumia...View attachment 2033627
Umenena vyema KingoHii picha nimeipenda kwa sababu naona ujumbe wake uko wazi ila kwa haraka haraka mtu anaweza kuukosa.
Ujumbe hapa ni kuwa wingi wa rasilimali aina moja tu haitoshi kwa mafanikio. Unahitaji kuwa na vitu kadhaa viendane ndo mafanikio yaje.
Tukiangalia picha... Huyo mtu ana matairi kibao yasiyo na rim, hivyo hawezi kuyatumia kubadilisha tairi bila kuwa na namna ya kuvalisha tairi jipya kwenye rim yake na hiyo siyo shughuli ndogo kama vifaa vya kazi hiyo hana. Walio wahi kuvalisha tairi kwenye rim watajua kuwa hivyo vifaa si vya kawaida kuwa navyo kwenye gari.
Kwa mifano.....kuwa na akili nyingi sana za darasani bila kujua namna ya kuishi na watu hufanya watu wengi wenye akili kukosa mafanikio. Kuwa na degree bila 'connection' ya kazi imefanya wengi wakose kazi na kusota mtaani. Kuwa na kipaji flani (e.g. kuimba) bila kuwa na confidence ya kukionyesha hicho kipaji na kukigeuza kuwa fursa ya ajira/kipato inasababisa wengi kufa na vipaji vyao/masikini. Hivyo kuwa na kipaji ni vizuri ila haitoshi, ni vizuri zaidi ukiwa na ujasiri wa kukionyesha na kukitumia la sivyo hautafanikiwa na kipaji hicho.
Na hili nalo ni fumbo?,
Cha kwanza nikiiangalia hii picha inaonyesha hii ni familia yenye maisha duni maana mpka kitambaa kilichotandikwa mezani kina viraka... ila kwenye hii picha pia kitu kingine hatumuoni baba tunamuona mwanamke tu na watoto wawili wakisubiria mama apike kiwekwe mezani tule ila kumbe nyuma ya panzia ni kwamba mama kwa ajili ya ku provide kwa watoto wake hata uhai wake yuko tayari kuutoa kwa ajili ya wanae.. na hapo mezani nadhani viti viko viwili tu sijui hata mama atakaa wapi akishaweka huo msosi mezani😭😭
Nyuma ya mafanikio ya waliofanikiwa kuna kushindwa kwingi na kutokuta tamaa ndio kumewafanya wao leo kua washindi.. huyo mtu anaonekana yuko mbele ya umati mkubwa wa watu wakiangalia anachokifanya kwa ustadi mkubwa ila kumbe mpk kufika level hio kulikua kuna majaribio kadhaa aliyafanya na akashindwa ila ngazi zinapanda juu zikimaanisha hakusita kuendelea kupambana mpaka mwisho akawa bora
Dunia na watu wake wasio na huruma😢 wamemgonga mzee wa watu na baiskeli yake kadondoka chini na vitu vyake vimemwagika ila waliomgonga wanashuka kwenye gari na kuanza kukagua gari lao badala ya kuenda kumuangalia waliemgongoa wanahangaika na michuma.
Kwa mara kadhaa nimekuwa nikikutana na picha au michoro mbalimbali ambayo wakati fulani ni vigumu sana kuelewa maana yake. Karibu na wewe uweke picha ambayo unadhani mpaka leo imekusumbua sana kuielewa au haujaielewa.
Wadau tusaidiane kutafuta maana...Mimi nitashare kadhaa kuanza na hii hapa [emoji116][emoji116]View attachment 2030550