Naombeni mnikumbushe tena maana ya maisha

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,861
Huenda mimi ni mmoja kati ya wale watu wanaosahau mambo haraka, kwa jinsi mambo yanavyosonga ni wazi kabisa nakosa maana halisi ya neno Maisha. Navurugwa na kupata mtungo wa maswali ndani ya kichwa change, nakosa majibu nabaki nakuna kichwa kwa mishangao mikubwa mikubwa.

Unaweza kupata mgonjwa ambaye anahitaji michango kwaajili ya kumudu gharama za matibabu na asipate kutokea hata mmoja n ahata akitokea basi kiwango kipatikanacho kinakuwa hakikidhi gharama za matibabu yake, pindi mtu huyo huyo anapopoteza Maisha yake na kuiaga dunia hii utashangaa watu watakavyoanza kujali na kutoa huduma zote bila kusita sita.

Nafikiri wengi wenu mmesikia Habari za msanii wa Nigeria anayefahamika kama MohBad, Stori kuhusu kijana huyu ambaye tayari ameshaiga dunia akiwa na umri wa miaka 27 tu. Kifo chake na historia yake imejaa sana utata ambao kila mmoja anazungumzia tukio la kufariki kwake kama kitu ambacho kilipangwa muda mrefu kutokea. Ndugu msomaji tafadhali naomba macho yako na hisia zako japo kwa ufupi nikupitishe katika mkasa huu wa kusisimua unaomuhusu kijana huyu Mohbad.
Mohbad alikuwa ni msanii wa kuimba na kufokafoka, Juni 8 mwaka 1996 huko Ketu, Lagos na wazazi wake wakampokea kwa bashasha na kumpa jina la Ilerioluwa Oladimeji Aloba. Baada ya kuku ana kuanza harakati za muziki akajipachika jina la MohBad au Imole,mwaka 2019 Kipaji chake kikaonekana na wengi mara baada ya kuona vipande vya video akiwa anaimba kwa mtindo huru na kufikia hatua ya kumvutia mkali Naira Marley naye hakufanya ajizi kuingia naye mkataba katika lebo yake ya Marlian Music Na rasmi MohBad akawa msanii mpya wa lebo hiyo. Kazi zikafanyika na akapata kutajwa na tuzo mbalimbali mwaka 2020.

Maisha yakasonga na mwaka 2022 baada ya kudumu kwa muda wa miaka miwili na ushei akaamua kuondoka katika lebo hiyo ya Marlian Music. Chanzo kimoja wapo kikiwa ni maslahi madogo kulingana na kazi nayoifanya, baada ya kuondoka katika lebo hiyo kijana huyu akaamua kuanzisha lebo yake aliyoipa jina la IMOLENIZATION akiwa na maana ya MWANGAZA. Show za ndani nan je ya nchi zikaanza kuchipua kama chemchem isiyokoma na hapo akaanza kupokea vitisho vingi vya kila aina akidai kuwa boss wake wa zamani anamtishia sana na Maisha yake yapo hatarini, akaongeza kuwa kama ikitokea amepoteza Maisha basi Naira Marley awe ndo mshukiwa wa kwanza kwa mambo anayomfanyia. Mara kadhaa alikuwa akiomba ulinzi kwa polisi kuhusu kuwa na mashaka na usalama wake lakini hakuna lolote lililofanyika juu yake, akawa anatuma vipande vifupi vya video na kutoa lawama juu ya watu wanaomtishia Maisha. Siku moja akiwa location ana rekodi video ya wimbo anatokea jamaa mmoja kwa jina Sam- Huyu ni rafiki mkubwa sana wa msanii Naira Marley, jamaa huyu anaanza kumpiga na kuamrisha waache kufanya walichokuwa wanakifanya haraka.

Maisha ya MohBad au Imole yakawa katika mashaka makubwa kwani kila alilokuwa akifanya ni kama alikuwa anawindwa. Kuna kipindi MohBad na rafiki zake walikamatwa na shirika moja linalojihusisha na upambanaji wa dawa za kulevya kwa jina DI NATIONAL DRUG LAW ENFORCEMENT AGENCY (NDLEA) wakidai kwamba vijana hawa wanajihusisha na dawa za kulevya na bangi.

Tarehe 12 mwezi wa 9 mwaka 2023 inasambaa taarifa ya kusikitisha juu ya kifo cha msanii huyu nah apo mambo ndipo yalipobadilika na kunifanya mimi niikamate vyema kalamu hii na kukuandikia Makala haya kutaka kukumbushwa juu ya maana halisi ya Maisha. Kwanini mwanzo wakati kijana huyu anaomba msaada hawakumzingatia na kwasasa amefariki ndo wanakuja juu kutaka kuweka sawa Sakata Lake, kweli Maisha ndo tumefikia huku? Hata wale ambao wanaifuata akaunti yake na kumposti mara nyingi kuliko hata alivyokuwa hai ni kweli wanaonyesha upendo kwake, Na vipi kuhusu nyimbo zake mabazo zilikuwa hazipati muda wa kutosha na kwa sasa zinabamba katika chati kibao za kitaifa na kimataifa ni kweli tulisubiri mpaka apoteze Maisha ndipo tuonyeshe sapoti hii?

Tazama sasa polisi wanahangaika kufukua kaburi lake kwaajili ya uchunguzi Zaidi, nawaza najiuliza kipindi anawaandikia barua polisi kuomba ulinzi mbona hawakujishughulisha naye na kipindi anatoa malalamiko yake juu ya Naira Marley na kuhusu kukamatwa na NDLEA-Ikumbukwe katika shirika hili Naira ni kama balozi wao, na kisha kupewa kinywaji asichokifahamu na kunywa huku akilazimishwa baadhi ya mambo kusema kwanini hawakumtilia maanani?, Vipi vile vipande vya video alivyokuwa anabandika katika mitandao yake ya kijamii akilia na kulalamika juu ya usalama wake kuwa hatarini. Vipi mashabiki ambao hata walikuwa hawapakui nyimbo zake leo wanavyozipakua na kumuweka katika mitandao ya kijamii ikiwa ameshatutoka yaani tunasubiri mtu aondoke ili tuonyeshe kuwa tunampenda na kumsapoti au ndo yale yale ya marehemu hasemwi vibaya na marehemu hupendwa na kila mtu? Bado nauliza na naomba kukumbushwa tena nini maana ya Maisha?

Kulia napangusa chozi, kushoto linanidondoka. Nainama chini napenga kamasi ambazo tayari zilikuwa zimeanza kubusu tundu za pua zangu, nakumbuka juu ya Sakata la Haitham Kim aliyetutoka hivi karibuni kwa ugonjwa wa kushindwa kupumua. Kipindi yupo hai wapo watu walikuwa hawatoi sapoti wala kuonyesha kujali juu ya uwepo wake, Wapo watu wa media walikuwa hata hawapigi nyimb zake hata angetoa wimbo mzuri vipi. Nasisimka mwili, nywele zinasimama napo kumbuka kipindi anaumwa ni watu wangapi walitoa kauli chafu juu yake mara walipotangaza anahitaji msada wa kuchangiwa pesa, siku alipofariki ndipo watu wakaanza kumzingatia na kutia huruma za kinafki hapo nyimbo zake zikafahamika kila kona hata yule asiyekuwa akimfahamu basi alimfahamu daah! Kweli ndo Maisha haya mbona sipati maana kabisa?

Mwili unaniisha nguvu napokumbuka juu ya Charming Charles, kijana aliyekuwa na ndoto kubwa lakini akazimika kama mshumaa uliotelekezwa baharini. Kipindi cha uhai wake ni wangapi walimuonyesha upendo na kumsapoti katika kile anachofanya? Alipofariki uliona namba zakekatika mitandao zilivyopanda, uliona watu walivyokuwa bize kumlilia alipotutoka. Hivi upendo huu tunaouonyesha watu wakipoteza Maisha kwanini tusiwape wakiwa bado wako hai?
Nguvu hii tunayoionyesha kipindi hawapo ni bora tungekuwa unawaonyesha ingali wakiwa hao nao wakapata kutimiza yale wanayoyatamania katika Maisha yao, lakini hiki kinachofanyika ninaona kama mchezo Fulani wa kuigiza na sijui hata mwisho wake utakuwa ni nini?
Hili sio mara ya kwanza limetokea sana kwa watu na naona linaendelea kutokea, jamani mimi naomba mkipata majibu mnijuze juu ya maana halisi ya Maisha, namba yangu ni ile ile mkipata majibu msisite kunitumia ujumbe.

WAKO NINAYEKUJALI
MHAYA
 
Binadamu huwa tunapuuzia mambo na tuna take easy karibu kila kitu, Nakumbuka my late uncle wakati anaumwa Nilimtembelea Nyumbani kwake,

Aliniambia Uncle naumwa sana huku akiniangalia usoni, Nikimchek Uncle namuona yuko vizuri tu na kwakuwa tulikuwa tunaonana mara kwa mara nikachukulia Poa sana na wala sikichukulia u-serious coz namjua uncle na nimemzoea

Guess what! Siku ambayo napewa taarifa za msiba ndio nikajua kwamba kumbe Uncle alikuwa anaumwa kweli kweli ile kabisa yaani ambayo ilitakiwa niwe Serious nae na utani ningeeka pembeni by that time

Dah niliumia sana coz nilijua ni homa ya kawaida tu ambayo atapona mda si mrefu, Nilijilaumu sana kwanini nilichukulia ugonjwa wake ki-masihara masihara na wakati ilitakiwa niwe namuona mara kwa mara kutokana na kuumwa kwake

Baada ya taarifa za msiba ndio uhalisia nikauona kama kweli I fcked up ...
 
Binadamu huwa tunapuuzia mambo na tuna take easy karibu kila kitu, Nakumbuka my late uncle wakati anaumwa Nilimtembelea Nyumbani kwake,

Aliniambia Uncle naumwa sana huku akiniangalia usoni, Nikimchek Uncle namuona yuko vizuri tu na kwakuwa tulikuwa tunaonana mara kwa mara nikachukulia Poa sana na wala sikichukulia u-serious coz namjua uncle na nimemzoea

Guess what! Siku ambayo napewa taarifa za msiba ndio nikajua kwamba kumbe Uncle alikuwa anaumwa kweli kweli ile kabisa yaani ambayo ilitakiwa niwe Serious nae na utani ningeeka pembeni by that time

Dah niliumia sana coz nilijua ni homa ya kawaida tu ambayo atapona mda si mrefu, Nilijilaumu sana kwanini nilichukulia ugonjwa wake ki-masihara masihara na wakati ilitakiwa niwe namuona mara kwa mara kutokana na kuumwa kwake

Baada ya taarifa za msiba ndio uhalisia nikauona kama kweli I fcked up ...
Dah.... Pole sana Kaka
 
Mhaya maisha ni fumbo
Maisha ni CODE
Unaweza kuzani umepata kumbe umepotea
Maisha ni upepo unaweza kukosea na ukapendwa cc mandonga mtu kazi

Maisha ni kitabu kuna kurasa haziwezi kusomwa mpaka ufariki.....

Maisha sio hisia, masikini sio kuwa hawajitumi na kuwa tajiri sio lazima ufanye kazi sana. Maisha ni zaidi ya ngekewa
 
Thats the way it is man... Mi nshaomba sana ndugu wanibusti mtaji wa biashara wakagoma Hadi nimeachana nao kabisa... Lakini najua nikioa au kufa basi hela watatoa za kumwaga sana yani... Ndo maisha bro hayana maana Wala nn Kuna mwanangu mmoja hivi anasema sisi ni kama mbuzi tu yani Kuna wahuni flani huko juu wanatufuga
 
Mhaya maisha ni fumbo
Maisha ni CODE
Unaweza kuzani umepata kumbe umepotea
Maisha ni upepo unaweza kukosea na ukapendwa cc mandonga mtu kazi

Maisha ni kitabu kuna kurasa haziwezi kusomwa mpaka ufariki.....

Maisha sio hisia, masikini sio kuwa hawajitumi na kuwa tajiri sio lazima ufanye kazi sana. Maisha ni zaidi ya ngekewa
Umenitafakarisha sana mkuu
 
Back
Top Bottom