Matumizi ya picha yasiyo sahihi huweza kusababisha upotoshaji

JamiiCheck

Member
Nov 3, 2023
55
45
IMG_20231223_102232_879.jpg


Kuambatisha picha katika habari yoyote ni muhimu katika kuongeza uelewa na kufafanua tukio au taarifa fulani.

Ili kutumia picha katika kutoa taarifa kuhusu jambo fulani, unapaswa kuzingatia uhalali wa hiyo picha, uwiano wa picha hiyo na tukio unalokusudia kulitolea taarifa au kulifafanua.

Uchaguzi usio sahihi wa picha unaweza kusababisha upotoshaji au usambaaji wa taarifa isiyo sahihi kwa watu. Hizi ni baadhi ya njia ambazo Matumizi ya picha isiyo sahihi yanaweza kusababisha upotoshaji:

Kubadilisha Muktadha
Picha inaweza kutumika kwa muktadha tofauti na ile iliyokusudiwa, hivyo kuwafanya watazamaji wapate maana isiyokuwa sahihi.

Kutumia Picha za Zamani
Kuchukua picha za zamani na kuzitumia kama vile zinahusiana na tukio la sasa, hivyo kuwadanganya watu kuhusu mwendelezo wa matukio.

Kuchanganya Picha
Kuunganisha picha mbalimbali ili kuunda taswira mpya ambayo inaweza kuwa ni uongo au inaweza kuchochea hisia za uongo.

Kupotosha Maelezo
Kutoa maelezo yasiyofaa au ya uongo kuhusu picha ili kutoa tafsiri inayopendelea au inayopotosha habari.

Matumizi mabaya ya picha yanaweza kuwa kama zana ya kudanganya na kutoa taarifa zisizo sahihi, na hivyo kuhatarisha uaminifu wa vyombo vya habari na kusababisha watu kuelewa mambo kwa njia isiyo sahihi.

Hivyo, ni muhimu kutumia picha sahihi kulingana na taarifa unayoitoa sambamba na kuitolea ufafanuzi endapo picha hiyo imepigwa siku ya tukio au ina uhusiano gani na wewe kuitumia kwenye taarifa yako.

Zaidi, tembelea Jukwaa la JamiiCheck kwa kubofya HAPA.
 
Back
Top Bottom