Maamuzi ya Prof Ndalichako yanashangaza

Maamuzi ya Prof Ndalichako yanashangaza

Anasema eti kuelekea Tanzania ya viwanda Sayansi ni lazima
nimejiuliza USA na China huko kote walilazimisha wanafunzi wote kusomea Sayansi?
au hii yetu ni 'ubunifu mpya'?
Shule sio mwisho form 4, watachagua wanapoenda form 5, tena hii itawapa nafasi kubwa wanafunzi kuendelea. watu wengi wanajuta kuacha masomo ya science form two.
 
Nyie mnaoleta na kutetea thread za namna hii tumeshawajua ni wamiliki wa vyuo binafsi na wale wenye watoto wasio na ufahulu mzuri. Vyuo vyenu binafsi mliwategemea sana wanafunzi wenye ufahulu hafifu ili mneemeke lakini ndo hivyo tena hakuna janja janja tena huku mkijifanya mnawatetea watoto masikini wakati huwa hawaji kwenye hivyo vyuo vyenu vyenye gharama kubwa.
 
Ingawa bandiko lako umelijaza Kiingereza bila ya sababu za msingi kuna hoja hapa umeianzisha naona na mimi nichangie. Kwenye mfumo wetu wa kufundishia darasani kuna tatizo kidogo. Mwalimu inaaminika anajua kila kitu wakati mwanafunzi anachukuliwa ana ubongo ulio wazi wa kujazwa kila kitu toka kwa mwalimu. Aina hii ya ufundishaji iko mpaka kwenye vyuo vyetu vikuu.

Wanafunzi wengi wanaosoma masomo ya mchepuo wa sanaa wanafeli zaidi kuliko wale wanaosoma masomo ya mchepuo wa sayansi, na sababu yake ni rahisi kueleweka. Masomo ya Mchepuo wa Sanaa ni rahisi lakini mitihani yake ni migumu wakati masomo ya sayansi ni magumu lakini mitihani yake ni rahisi. Na ndiyo maana mara nyingi wanaoshika nafasi kumi za kwanza kitaifa kwa Mitihani ya Kidato cha Nne na cha Sita huwa wanatoka kwenye mchepuo wa Sayansi.
Sio kweli, kila mchepuo unakuwa na namba moja wake kitaifa ,huwezi kukuta mtu aliyesoma sayansi akawekwa kundi moja na aliyesoma sanaa.Huwa wanawapanga wanafunzi bora waliongoza sanaa, sayansi pamoja na biashara katika makundi tofauti, ila wale wa sayansi ndo huwa wanapewa promo kubwa ingawa unaweza ukakuta aliyeongoza masomo ya sanaa ana point 3 alaf yule wa sayansi ana point 4 au 5
 
Akili ndogo inaongoz akili kubwa.... hii kauli si ya kupuuza. Mtoto ana akili kuliko baba na baba ndio mwenye final say...unategemea nin hapo kama sio mtoto kutekeleza ili aendelee kulipiwa ada. Wateule wa rais wanapokosea ni pale wanapochukuwa kila tamko la mkuu wao ni sheria, halijadiliwi wala kukosolewa. Wanathamini position zao kuliko yale wayatendayo.
 
brigedia mafia hakuna ufaulu wa jumla kwa wanafunzi kitaifa?

pic+mtoto.jpg

Huyu alikuwa wa kwanza Kitaifa kwenye mitihani ya kidato cha sita mwaka 2015. Anaitwa Ramadhamani Gembe. Alisoma Fizikia Kemia na Bailojia (Physic, Chemistry and Biology - PCB)
 
MAMA NDALICHAKO YUKO SAHIHI 100 %. KWANI TATIZO MNALOLIONA HAPO NI LIPI?

MIMI NIMESOMA MASOMO YOTE TISA(9) O LEVEL, nothing i lost. ADVANCED LEVEL nikasoma mchepuo wa Arts yaani HGE.
namshukuru MUNGU C ya mathematics na Ds za physics, chemistry na biology (biology na chemistry siyo sana) ila applications zake nimezitumia sana mpaka university wakati nasoma bachelor ya ECONOMICS.
Mwenye reason ya kusema tamko hilo ni wrong atueleze.
Wapo walioko vyuoni walikimbilia arts o level leo wanatamani warudi wakasome mathematics na physics tena.
Acheni wasome yote kama mimi atakaye feli masomo ya science kama mimi hata razimishwa kuyasoma advance.
Lakini atakuwa na knowledge kama yangu tofauti na aliyekimbia kabisa kama mnavyowashauri.
 
Ana shida sana ya exposure! Sio bure! Viwanda vidogo na veta ndio muhimu zaidi pia zile shule za technical waziendeleze!!! Mule ndio ma engineer walitengenezwa!! Sio kulazimisha!!! Kila mtu asome sayansi! Hata kama dream zako ziko biashara au arts unalazimisha tu!? Hakuna mavitu ya nguvu bila akili!!
Anasema eti kuelekea Tanzania ya viwanda Sayansi ni lazima
nimejiuliza USA na China huko kote walilazimisha wanafunzi wote kusomea Sayansi?
au hii yetu ni 'ubunifu mpya'?
 
Kama ni kwa o' level tu namuunga mkono. Ku-opt masomo katika ngazi za chini ni tatizo. Kuna shule wana chagua msomo bila mpangilio mwisho mtoto anamaliza form four anakosa muunganiko wa comb. Pia science inafanya akili ya mtoto iwe active. Wasome yote. Akifika form five atasoma anayoyataka. Pia wengi wana-opt kwa kufuata mkumbo akifika form four ndo anagundua alichemka na ndo hawezi kurudi nyuma tena.
Hakuna somo linalo mtaka mtoto kuwa na tafakari na ubunifu ( thinking) kama hisabati,lakini najua matokeo yake unayajua. Sasa niambie huyo mtoto atakae weza physics na chemistry wakati hata zile basics za hesabu hawezi,hiyo itakuwa physics au chemistry gani? Hapa nachoweza sema nikuwa tunatafuta masomo yatakayo kuwa pacha wa hesabu kwa idadi ya watakao feli.
 
Kuna kitu nimenotisi.
Mojawapo ya maamuzi mabovu kabisa kutolewa kuhusu elimu yetu ni wakati wa Mkapa na Mungai wake.
Sasa hivi tunaye mkuu ambaye many of us knows jinsi alivyoibuliwa na kukuzwa na kuwa kipenzi cha Mkapa.Sasa tunashuhudia aina ile ile ya maamuzi ya hatari kwenye elimu yanayolenga kumwekea vikwazo vingi mtoto wa maskini kufika elimu ya juu na kupata elimu bora kwa ujumla.
Je,hii ni coincidence au ndio system ile ile imerudi hewani na mambo yao yale yale?
Kwanini wakiingia madarakani huwa wako bize sana na changes kwenye mfumo wa elimu na yale wanayoanzisha mengi huwa yanaivuruga sana elimu?ni kukurupuka kutafuta sifa au hii ni AGENDA?Hawataki wasomi wengi Tanzania?Hawataki watanzania wengi waelimike na kuwa na taifa la wasomi baadae?Ni kweli wasomi aina ya viongozi wetu hawaoni vitu hivi ambavyo sisi wa kawaida tu tunaviona au wana ajenda zao?Is this a conspiracy?
Nashangaa sana!
 
Bila shaka wewe utakuwa kat ya wale watu waliokimbia kusoma PHYSICS o'level
 
Watakuja yakana matamko yao yote yaliyo chongo kwa kusema watanzania hawakumuelewa au wamemtafasiri tofauti utazani ua wanatumia lugha ya kigeni wakati wa kutoa matamko
 
Nishasema ndani ya miaka hii 5 tutashuhudia mengi sana tena ya ajabu katika serikali hii ya mwendokasi
 
Back
Top Bottom