SoC02 Maamuzi ya kisheria kwa wale wote wanaovunja sheria yatekelezwe kwa kufuata sheria zilizowekwa

Stories of Change - 2022 Competition

Theb

JF-Expert Member
Jan 25, 2019
3,927
7,273
Andiko hili litakua katika sehemu tatu. Moja utangulizi ambao utelezea maana ya sheria. Mbili, hapa nitaonesha baadhi ya maamuzi ya kisheria yenye kuleta utata katika jamii zetu, ya kiuchumi, kisiasa, kijinsia na michezo na burudani
SHERIA
Ni mfumo wa kanuni ambazo hutekelezwa au hufuatwa katika kuliongoza kundi fulani. Inaweza kuwa familia, ukoo, chama cha siasa, taasisi, au serikali fulani.

SHERIA ZA NCHI
Hizi ni kanuni zilizotungwa na kuwekwa kikatiba ili zitumike katika kuliongoza taifa husika. Tanzania inaogozwa kwa mujibu wa sheria zilizopo kwenye katiba.

BAADHI YA MAAMUZI YA KISHERIA YALIYOZUA, YANAYOZUA UTATA NCHINI

1. KESI YA SABAYA NA WENZAKE MPAKA KUACHIWA KWAO

Aliye kuwa mkuu wa wilaya ya hai Sabaya alisimamishwa kazi na Mhe Raisi Samia Suluhu Hasan mnamo Mei 13, 2021 kupisha uchunguzi. Sabaya alishutakiwa kwa makosa yaliyotajwa
Lengai Ole Sabaya (34) na walinzi wake watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha wakikabiliwa na makosa mbalimbali likiwemo la uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kupokea rushwa.
Waendesha mashtaka wa Serikali, Tumaini Kweka, Abdallah Chaula na Tresla Garvas mbele ya Hakimu Mfawidhi, Martha Mahumbuga na Hakimu Mkazi Mkuu, Salome Mshasha wamesema Sabaya na wenzake walitenda makosa hayo Januari 20 na Februari 9, 2021.

Kweka amesema "Sabaya na wenzake watano anatuhumiwa kwa makosa ya kuunda genge la uhalifu, uhujumu uchumi, kujipatia fedha kwa njia ya rushwa na utakatishaji fedha ambapo Sabaya alijipatia Sh90 milioni kutoka kwa mfanyabiashara, Francis Mroso mkazi wa kwa Mromboo ambaye alikuwa anatuhumiwa kwa makosa ya ukwepaji kodi ili amsaidie jambo ambalo ni makosa".
(chanzo cha habari hii Mwananchi)

Hukumu hii ya sabaya bado wananchi hawaelewi wale mashahidi na CCTV Camera kweli havitoshi kudhibitisha makosa yake..?

2. HUKUMU YA MANARA YA MIAKA MIWILI NA FAINI YA MILIONI 20 (miaka 2 ya kutojihusisha na masuala ya michezo ndani na nje ya nchi).
Wapo wanaokataa adhabu aliyopewa manara ila sheria haiangalii umaarufu wa mtu.

Kamati ya Maadili ya TFF, imemfungia Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara kutojihusisha na masuala ya soka ndani na nje ya nchi kwa miaka miwili na faini ya Sh20 milioni kwa kosa la kumtolea maneno yasiyofaa Rais wa TFF, Wallace Karia katika mechi ya fainali ya kombe la Azam iliyochezwawa Jijini Arusha
Manara anatuhumiwa kusema maneno haya
"Wewe unanifatafata sana, hii ni mara ya tatu, sikuogopi kwa lolote,kwa chochote na huwezi kunifanya chochote. Nina uwezo wa kukufanya chochote na huna cha kunifanya" Kauli hizi zimekua za kujirudia kutoka kwa manara hivyo sheria iheshimiwe. (Chanzo cha habari Mwananchi).

3. SUALA LA WABUNGE 19 WA CHADEMA
Wabunge hawa inasemekana waliapishwa kimakosa kwa maana chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) hakikuhusika. Hili nalo maamuzi yake wananchi hawayaelewi yamejaa utata mwingi. Je sheria inasemaje kuhusu hilo.? Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilisha wafukuza. Ripoti ya
Baraza Kuu la Chadema limeunga mkono uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho wa kuwafukuza uanachama wabunge 19 wa viti maalum, miongoni mwao ni pamoja na aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la wanawake BAWACHA Halima Mdee (Chanzo cha habari BBC Swahili).

Mahakama itoe hukumu yenye kuzingatia misingi ya sheria katika hili la wabunge 19 wa CHADEMA itasaidia kuondoa sintofahamu na migogoro iliyopo kisiasa.

4. WAHUJUMU UCHUMI
Zilipigwa kelele nyingi awamu ya tano kuhusu wahujumu uchumi ila cha ajabu hatukuona jambo lakueleweka katika kuitekeleza sheria. Taarifa ya BBC Swahili,
Rais wa Tanzania John Magufuli amesema zaidi ya watu 700 waliokuwa wakishutumiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi, ikiwemo utakatishaji wa fedha , wamekiri kutenda makosa hayo wakiomba kusamehewa, huku wengine zaidi ya 100 wakiachwa huru. (Chanzo cha habari BBC Swahili).

5. WAFANYAKAZI WASIO WAADILIFU, WABADHILIFU WA MALI ZA UMMA PAMOJA NA WALA RUSHWA
Hili nalo lina zua utata miaka nenda wapo wafanyakazi wa umma wenye shutuma za kuliibia au kulitia taifa hasara kubwa lakini sheria haijawachukulia hatua. Wapo wafanyakazi wamehusishwa na kula rushwa lakini wananchi wanauliza mbona sheria inawaaacha tu.

6. MATENDO YA UBAKAJI ULAWITI NA UKATILI WA KIJINSIA.
Yapo matukio ya watu waliohusika kufanya ubakaji, ulawiti na ukatili wa kijinsia katika jamii zetu nchini. Tabia hizo zimekua zakujirudia rudia kiasi kwamba zina ogopesha. Sheria iweke wazi adhabu zao na ziwe kali ili kusaidia kupunguza na kutokomeza tatizo hili. Taarifa iliyotolewa na Dewtsche Welle inasema
Tukio la mkazi wa Iringa, kudaiwa kumlawiti mtoto wake wa kambo na shemeji yake.
Kadhalika, liliripotiwa tukio lililobeba vichwa vingi vya habari la mtoto wa miaka 14 mkazi wa Iringa, kuwalawiti watoto wenzake 14 wote wa kiume. Kadhalika Mei 18 kuliripotiwa tukio la mkazi mmoja wa Arusha tuhumiwa kuwalawiti wanafunzi takribani 22 wa shule ya msingi Mkonoo, jijini Arusha. Kwa matukio hayo yaliyoripotiwa kati ya Januari na Mei, inatosha kusema kuwa watoto hawapo salama.Matukio ya hivi karibuni ni pamoja na lile la Januari 19, ambapo Shukrani Kamwela mwenye umri wa miaka 16, mkazi wa Ileje mkoani Songwe alimuua kwa kumchoma kisu mke wake aitwaye Subira Kibona mwenye umri wa miaka 16 aliyekuwa ni mjamzito. Tukio lingine ni lile la Desemba 27, la mwalimu wa Sekondari mkoani Singida, Simon Roman aliyefariki baada ya kuchomwa moto na mkewe sababu ikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

(Chanzo cha habari Dewtsche Welle idhaa ya kiswahili)

HITIMISHO LANGU
Wananchi au jamii kwa ujumla inapata wakati mgumu kuzielewa baadhi ya hukumu za watu waliokuwa maarufu wa kisiasa au wenye hali ya ukwasi kifedha na wenye umaarufu katika michezo na burudano je wao sheria haiwahusu.? Wanakosea wanavunja sheria ni lazima wachukuliwe hatua tena kwa ukali maama wanajiita vioo vya jamii. Makundi ya watu nilio waorodhesha hapo juu kwangu mimi naona hao ndio wawe wa kwanza kuchukuliwa hatua tena za haraka na zenye kuegemea kwenye misingi ya sheria zilizowekwa itasaidia kulijenga taifa katika kuziheshimu sheria zetu.

Sheria iwe msumeno kweli kweli iguse na kuhukumu kila anaekosea. Awe kiongozi, tajiri, masikini au yoyote yule atakae fanya jambo linaloivunja sheria ya nchi hainabudi kuhukumiwa kwa kuitumia sheria iliyopo.

Pia viongozi wasipende kutumia kauli zao kuwa sheria, hili linaleta sintofahamu zaidi katika baadhi ya hukumu zinazohutaji sheria kufuata. Mfano kionzogozi mkuu wa awamu ya tano alipenda saaba kutoa kauli za kutisha na zenye kuingilia sheria zilizopo
 
Hapo juu umetwambia sababu mojawapo ya Kuwaita wabunge 19 kuwa hawana vigezo vya ubunge kwamba ni kwenda mahakamani. Nikuulize Kwani mbunge yoyote akiingia mahakamani anakuwa siyo mbunge ?
Naona umeninukuu vibaya au niseme dhamira yangu hauja ielewa kwa usawa kama nilivyo kusudia acha nikuelezea tena hapa labda utanielewa. Nimeandika kuwa baadhi ya hukumu zinaleta sintofahamu kwa wanajamii kwa maana wenye chama wanasema hawawatambui na wakasema wamepeleka barua ya kuwavua uanachama ndani ya chama chao(CHADEMA) hivyo kinachoendelea kinaleta mgogoro pia kinaleta hali ya mshangao kwa wananchi. Mahakama ifanye maamuzi yake ijulikane nani mwenye kosa ili kuondoa mgogoro na sintofahamu iliyopo katika jamii juu ya hili.
 
Naona umeninukuu vibaya au niseme dhamira yangu hauja ielewa kwa usawa kama nilivyo kusudia acha nikuelezea tena hapa labda utanielewa. Nimeandika kuwa baadhi ya hukumu zinaleta sintofahamu kwa wanajamii kwa maana wenye chama wanasema hawawatambui na wakasema wamepeleka barua ya kuwavua uanachama ndani ya chama chao(CHADEMA) hivyo kinachoendelea kinaleta mgogoro pia kinaleta hali ya mshangao kwa wananchi. Mahakama ufanye maamuzi yake ijulikane nani mwenye kosa ili kuondoa mgogoro na sintofahamu iliyopo katika jamii juu ya hili.
Kwahiyo wabunge 19 wa upinzani mpaka sasa bado ni wabunge au siyo wabunge ?
 
Kulingana na zuio lililowekwa na mahakama bado ni wabunge japo wana lakukibu. Hivyo lolote linaweza kutokea tujipe muda na kuzidi kuipa mahakama muda wa kulitolea uamuzi sahihi hili. Kwa ujumla maamuzi ya mwisho ya kisheria ndiyo yatakayo toa mwanga kuwa wabaki kuwa wabunge au wafurushwe
 
Kwahiyo unajua hapa tunajadiri nini ? Kwamba wabunge 19 mda huu ni wabunge halali au sio halali ?
Kwa kuwa shauri kao lipo mahakamani hatuwezi kusema ni halali au sio halali bali tuone hukumu yao itaamua nini hatima ya ubunge wao. Acha tuone maamuzi ya kisheria juu ya hili la wabunge 19 yata semaje. Ndipo tutawaita ni halali ama batili
 
Jibu swali moja wabunge wa upinzani 19 ni halali au siyo halali
 
Bado sio halali maana yapo masuala yanaleta utata. Acha tuone mahakama itafanya maamuzi gani. Ikiwa chadema wanakiri walisha wafukuza uanachama acha tuone. Ila kulingana na maelezo ya chadema walitiaminisha kuwa wabunge 19 wamewafukuza uanachama kulingana na kukiukwa wa mambo mbali mbali waliyo yasema.
 
Asante sana
 
Mifumo ya sheria ipo balance kwenye paperwork tu lakini kiuhalisia uwabeba wenye nguvu
 
Karibu. Kweli kama usemavyo mifumo ya kisheria wanalalamika wananchi kuwa ina wabeba wenye nguvu. Andiko langi lime lenga pale pale ili kuweka usawa kwa wote ikiwa wamekosea inapaswa sheria ifuatwe kwa usahihi kwa wote bila kujali mi kiongozi tajuri, ama mwasiasa maarufu au mtu yeyote yule
 
Hili limeweze

Hili limewezekana kwenye Jamii zilizostaarabika mfano ulaya na USA au staarabishwa kwa lazima mfano China na nchi za Sheria za kiislamu, sheria za kiislamu uifungaamanisha sheria na imani Ili ziweze leta matokeo chanja.
 
Mfano kwetu jela ni kwa ajili ya watu masikini ukiiba kidogo utafungwa miaka mingi sana lakini ukifisadi kingi utalipa faini kiduchu Sana Ili utoke.
 
Mfano unakuta wapigaji wakubwa wao awachukuliwi hatua bali wale wadogo ndio uchukuliwa hatua kama Ili kutafuta kiki ya kumake headline. Mfano unakuta Waziri anajifanya kuona uchungu ufisadi wa ujenzi wa chumba cha milioni 11 wakati yupo kwenye v8 la Milioni 450 lisilo na tija kwa mlipa kodi akiwa na msururu wa msafara plus gharama za mafuta na posho isiyozidi jumla milioni 5.
Hizi sheria utekelezwa kwa watu wa chini tu
 
Andiko hili litakua katika sehemu tatu. Moja utangulizi ambao utelezea maana ya sheria. Mbili, hapa nitaonesha baadhi ya maamuzi ya kisheria yenye kuleta utata katika jamii zetu, ya kiuchumi, kisiasa, kijinsia na michezo na burudani
SHERIA
Ni mfumo wa kanuni ambazo hutekelezwa au hufuatwa katika kuliongoza kundi fulani. Inaweza kuwa familia, ukoo, chama cha siasa, taasisi, au serikali fulani.

SHERIA ZA NCHI
Hizi ni kanuni zilizotungwa na kuwekwa kikatiba ili zitumike katika kuliongoza taifa husika. Tanzania inaogozwa kwa mujibu wa sheria zilizopo kwenye katiba.

BAADHI YA MAAMUZI YA KISHERIA YALIYOZUA, YANAYOZUA UTATA NCHINI

1. KESI YA SABAYA NA WENZAKE MPAKA KUACHIWA KWAO

Aliye kuwa mkuu wa wilaya ya hai Sabaya alisimamishwa kazi na Mhe Raisi Samia Suluhu Hasan mnamo Mei 13, 2021 kupisha uchunguzi. Sabaya alishutakiwa kwa makosa yaliyotajwa
Lengai Ole Sabaya (34) na walinzi wake watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha wakikabiliwa na makosa mbalimbali likiwemo la uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kupokea rushwa.
Waendesha mashtaka wa Serikali, Tumaini Kweka, Abdallah Chaula na Tresla Garvas mbele ya Hakimu Mfawidhi, Martha Mahumbuga na Hakimu Mkazi Mkuu, Salome Mshasha wamesema Sabaya na wenzake walitenda makosa hayo Januari 20 na Februari 9, 2021.

Kweka amesema "Sabaya na wenzake watano anatuhumiwa kwa makosa ya kuunda genge la uhalifu, uhujumu uchumi, kujipatia fedha kwa njia ya rushwa na utakatishaji fedha ambapo Sabaya alijipatia Sh90 milioni kutoka kwa mfanyabiashara, Francis Mroso mkazi wa kwa Mromboo ambaye alikuwa anatuhumiwa kwa makosa ya ukwepaji kodi ili amsaidie jambo ambalo ni makosa".
(chanzo cha habari hii Mwananchi)

Hukumu hii ya sabaya bado wananchi hawaelewi wale mashahidi na CCTV Camera kweli havitoshi kudhibitisha makosa yake..?

2. HUKUMU YA MANARA YA MIAKA MIWILI NA FAINI YA MILIONI 20 (miaka 2 ya kutojihusisha na masuala ya michezo ndani na nje ya nchi).
Wapo wanaokataa adhabu aliyopewa manara ila sheria haiangalii umaarufu wa mtu.

Kamati ya Maadili ya TFF, imemfungia Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara kutojihusisha na masuala ya soka ndani na nje ya nchi kwa miaka miwili na faini ya Sh20 milioni kwa kosa la kumtolea maneno yasiyofaa Rais wa TFF, Wallace Karia katika mechi ya fainali ya kombe la Azam iliyochezwawa Jijini Arusha
Manara anatuhumiwa kusema maneno haya
"Wewe unanifatafata sana, hii ni mara ya tatu, sikuogopi kwa lolote,kwa chochote na huwezi kunifanya chochote. Nina uwezo wa kukufanya chochote na huna cha kunifanya" Kauli hizi zimekua za kujirudia kutoka kwa manara hivyo sheria iheshimiwe. (Chanzo cha habari Mwananchi).

3. SUALA LA WABUNGE 19 WA CHADEMA
Wabunge hawa inasemekana waliapishwa kimakosa kwa maana chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) hakikuhusika. Hili nalo maamuzi yake wananchi hawayaelewi yamejaa utata mwingi. Je sheria inasemaje kuhusu hilo.? Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilisha wafukuza. Ripoti ya
Baraza Kuu la Chadema limeunga mkono uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho wa kuwafukuza uanachama wabunge 19 wa viti maalum, miongoni mwao ni pamoja na aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la wanawake BAWACHA Halima Mdee (Chanzo cha habari BBC Swahili).

Mahakama itoe hukumu yenye kuzingatia misingi ya sheria katika hili la wabunge 19 wa CHADEMA itasaidia kuondoa sintofahamu na migogoro iliyopo kisiasa.

4. WAHUJUMU UCHUMI
Zilipigwa kelele nyingi awamu ya tano kuhusu wahujumu uchumi ila cha ajabu hatukuona jambo lakueleweka katika kuitekeleza sheria. Taarifa ya BBC Swahili,
Rais wa Tanzania John Magufuli amesema zaidi ya watu 700 waliokuwa wakishutumiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi, ikiwemo utakatishaji wa fedha , wamekiri kutenda makosa hayo wakiomba kusamehewa, huku wengine zaidi ya 100 wakiachwa huru. (Chanzo cha habari BBC Swahili).

5. WAFANYAKAZI WASIO WAADILIFU, WABADHILIFU WA MALI ZA UMMA PAMOJA NA WALA RUSHWA
Hili nalo lina zua utata miaka nenda wapo wafanyakazi wa umma wenye shutuma za kuliibia au kulitia taifa hasara kubwa lakini sheria haijawachukulia hatua. Wapo wafanyakazi wamehusishwa na kula rushwa lakini wananchi wanauliza mbona sheria inawaaacha tu.

6. MATENDO YA UBAKAJI ULAWITI NA UKATILI WA KIJINSIA.
Yapo matukio ya watu waliohusika kufanya ubakaji, ulawiti na ukatili wa kijinsia katika jamii zetu nchini. Tabia hizo zimekua zakujirudia rudia kiasi kwamba zina ogopesha. Sheria iweke wazi adhabu zao na ziwe kali ili kusaidia kupunguza na kutokomeza tatizo hili. Taarifa iliyotolewa na Dewtsche Welle inasema
Tukio la mkazi wa Iringa, kudaiwa kumlawiti mtoto wake wa kambo na shemeji yake.
Kadhalika, liliripotiwa tukio lililobeba vichwa vingi vya habari la mtoto wa miaka 14 mkazi wa Iringa, kuwalawiti watoto wenzake 14 wote wa kiume. Kadhalika Mei 18 kuliripotiwa tukio la mkazi mmoja wa Arusha tuhumiwa kuwalawiti wanafunzi takribani 22 wa shule ya msingi Mkonoo, jijini Arusha. Kwa matukio hayo yaliyoripotiwa kati ya Januari na Mei, inatosha kusema kuwa watoto hawapo salama.Matukio ya hivi karibuni ni pamoja na lile la Januari 19, ambapo Shukrani Kamwela mwenye umri wa miaka 16, mkazi wa Ileje mkoani Songwe alimuua kwa kumchoma kisu mke wake aitwaye Subira Kibona mwenye umri wa miaka 16 aliyekuwa ni mjamzito. Tukio lingine ni lile la Desemba 27, la mwalimu wa Sekondari mkoani Singida, Simon Roman aliyefariki baada ya kuchomwa moto na mkewe sababu ikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

(Chanzo cha habari Dewtsche Welle idhaa ya kiswahili)

HITIMISHO LANGU
Wananchi au jamii kwa ujumla inapata wakati mgumu kuzielewa baadhi ya hukumu za watu waliokuwa maarufu wa kisiasa au wenye hali ya ukwasi kifedha na wenye umaarufu katika michezo na burudano je wao sheria haiwahusu.? Wanakosea wanavunja sheria ni lazima wachukuliwe hatua tena kwa ukali maama wanajiita vioo vya jamii. Makundi ya watu nilio waorodhesha hapo juu kwangu mimi naona hao ndio wawe wa kwanza kuchukuliwa hatua tena za haraka na zenye kuegemea kwenye misingi ya sheria zilizowekwa itasaidia kulijenga taifa katika kuziheshimu sheria zetu.

Sheria iwe msumeno kweli kweli iguse na kuhukumu kila anaekosea. Awe kiongozi, tajiri, masikini au yoyote yule atakae fanya jambo linaloivunja sheria ya nchi hainabudi kuhukumiwa kwa kuitumia sheria iliyopo.

Pia viongozi wasipende kutumia kauli zao kuwa sheria, hili linaleta sintofahamu zaidi katika baadhi ya hukumu zinazohutaji sheria kufuata. Mfano kionzogozi mkuu wa awamu ya tano alipenda saaba kutoa kauli za kutisha na zenye kuingilia sheria zilizopo
Thread nzuri
 
Back
Top Bottom