Maamuzi ya idadi ya watoto ni ya nani?

Kama ni mwanamke alie ajiriwa ni vyema mwanaume uwe msikivu kwa mwenzako pale anaposema mzae kwa mpango...koz wanawake wanapitia changamoto nyingi sana anapokua na watoto wengi huku pia kazi zinamsubiri, huwezi kumwambia mkeo akae nyumbani tu akuzalie kuna kesho unaeweza ukaondoka hapa duniani ukamuacha kwenye kipindi kigumu ...mwanaume muelewa ataelewa hili
Ni kweli kabisa.
 
Wanajf kuna jambo limenifanya niilete hii mada kwenu.

Kuna kaka alihitaji na alipendelea kuwa na watoto watatu, na walikubaliana na mkewe wawe na watoto watatu Mungu akiwajaalia.
Baada ya mkewe kujifungua mtoto wa pili akamwambia mumewe asingeweza kwenda leba tena(alijifungua kwa njia ya kawaida na hakukuwa na complications zozote).

Mume alihisi ni kwavile ametoka kujifungua ndio maana anasema hivyo, lakini baada ya miaka mi4 kupita bado msimamo wa mkewe ni uleule, amemwambia ikiwa ni lazima apate huyo mtoto wa tatu anamruhusu kwa roho safi tu akamtafute.

Naomba kuwauliza haswa wanandoa, maamuzi ya idadi ya watoto mnaohitaji kuwa nao huwa ni ya nani? And how if kila mmoja akawa na idadi yake ya watoto anaohitaji inayotofautiana na mwenzie?

Na wanawake utafanya nini ikiwa mumeo anahitaji idadi kubwa ya watoto tofauti na matakwa yako?
[/QUOTE
Niliwahi sikia yakuwa kipindi cha ujauzito mpaka kujifungua kina mama wanapitiaga mengi hivyo hatuwezijua kwann anagoma kuongeza huyo wa 3, na kibaya mtoa bandiko hajatwambia huyo Mrs anatoa sababu zipi ... Tungejua hizi sababu ingekuwa rahisi kushauri
 
Mwanaume ndie anaepanga idadi ya watoto lakini pia sio mbaya kushauriana mana wote ni kitu kimoja ila kuna jambo moja la kifedha kama kipato chenu kina ruhusu sio mbaya unaweza kuzaa tu watoto wengi mana watoto wanaitaji matunzo na vingine vingi
 
Ya wote wawili washauriane huku wakiangalia sana gharama za maisha na kipato chao. Ile dhana ya kila mtoto atakuja na riziki yake ni dhana ya jalalani kwani mtoto anapozaliwa haji na bulungutu lake.
Ilikuwa dhana za wazee wetu, walifyatua tu na ardhi ilikuwa na neema tele wakati huo.

Kuna wanaume hawapo tayari kwa makubaliano, anachokitaka yeye ndio hicho hicho.
 
Mwanaume ndie anaepanga idadi ya watoto lakini pia sio mbaya kushauriana mana wote ni kitu kimoja ila kuna jambo moja la kifedha kama kipato chenu kina ruhusu sio mbaya unaweza kuzaa tu watoto wengi mana watoto wanaitaji matunzo na vingine vingi
Unahisi ni kwanini mwanaume ndio anapaswa kupanga idadi aitakayo yeye?
 
Ilikuwa dhana za wazee wetu, walifyatua tu na ardhi ilikuwa na neema tele wakati huo.

Kuna wanaume hawapo tayari kwa makubaliano, anachokitaka yeye ndio hicho hicho.
Watoto wakiwa wazuri lazima uzidi kushawishika katika kuongeza uzao
 
Ni mwanamme ndio atapanga idadi ya watoto watakaopatikana, I mean there is no objection from the husband side if the wife need more and more kids. There will always be objections from the wife's side if a husband wants more and more kids, if you know what I mean!

You can't just tell me utazaa watoto watatu eti because unataka umaintain umbo lako, that's crap! Give me the acceptable reasons like health reasons.

I will get the number of kids I want with you, or without you! In my world, I make the money, i make the rule.......
Apa kama vile umeweka mfumo dume haya mambo ni watu wawili sio mwanaume tu kumbuka we unatoa mbegu tu
 
Back
Top Bottom