Maamuzi ya idadi ya watoto ni ya nani?

Habun

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
71,735
2,000
Wanajf kuna jambo limenifanya niilete hii mada kwenu.

Kuna kaka alihitaji na alipendelea kuwa na watoto watatu, na walikubaliana na mkewe wawe na watoto watatu Mungu akiwajaalia.
Baada ya mkewe kujifungua mtoto wa pili akamwambia mumewe asingeweza kwenda leba tena(alijifungua kwa njia ya kawaida na hakukuwa na complications zozote).

Mume alihisi ni kwavile ametoka kujifungua ndio maana anasema hivyo, lakini baada ya miaka mi4 kupita bado msimamo wa mkewe ni uleule, amemwambia ikiwa ni lazima apate huyo mtoto wa tatu anamruhusu kwa roho safi tu akamtafute.

Naomba kuwauliza haswa wanandoa, maamuzi ya idadi ya watoto mnaohitaji kuwa nao huwa ni ya nani? And how if kila mmoja akawa na idadi yake ya watoto anaohitaji inayotofautiana na mwenzie?

Na wanawake utafanya nini ikiwa mumeo anahitaji idadi kubwa ya watoto tofauti na matakwa yako?
 

Habun

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
71,735
2,000
Mwanaume ndio anatakiwa kupanga idadi ya watoto kulingana na kipato chake.

Kama mwanamke analazimisha idadi ndogo na mme anataka idadi kubwa basi uchumi wa familia uwe ndio kigezo cha maamuzi ya mwisho.
Kwahiyo uchumi ukiwa unatosheleza idadi anayoitaka mwanaume na mke hayuko tayari kwa idadi kubwa?
 

ni ngumu

JF-Expert Member
Sep 25, 2016
4,137
2,000
Wote wawili ingawa mimi napenda wawili Sitaki mke wangu achoke sababu ya kuzaa , outing nitatoka na Nani.SI wengine tunapenda sifa unatoka outing na mwanamke yupo in shape anavutia sifa na pata Mimi kidume...

Mke wa jamaa ni mashine safiiiiiiii ndo nataka hivyo, heshima.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom